Kwa hili jeshi la polisi shame on you, nimeamini vichwani hamnazo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa hili jeshi la polisi shame on you, nimeamini vichwani hamnazo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BASHADA, Nov 24, 2011.

 1. BASHADA

  BASHADA JF-Expert Member

  #1
  Nov 24, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 487
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Jamani wanajamvi, habari zenu. Katika hali ya kusikitisha, kuna mtu mmoja hapa Iringa amenusurika kuvunjwa miguu yote miwili na askari waliokuwa wanalinda benki ya NBC jana tarehe 23 November 2011 kwa ujinga na upunguwani wa askari hao.

  Ilikuwa hivi, jamaa mmoja alitumiwa cheque yake kutoka UDSM akaenda nayo NBC hapa Iringa mjini ili alipwe hela yake. Alipofika benki ikaonekana kuwa ile cheque ilitakiwa isainiwe na signatories wawili lakini ilisainiwa na mmoja (pia ikaonekana ilikuwa ni kimakosa).

  Yule jamaa akaomba azungumze na uongozi wa benki ili kuona kama kuna uwezekano wa kusaidiwa na kwa bahati akafanikiwa kwenda kwa meneja wa benki ambapo ilihitimishwa kuwa waifax ile cheque Dar es salaam ili nao wajibu kama ni sahihi watoe ukubali ili watu wa NBC iringa wamlipe mhusika. Katika michakato yote hiyo, meneja akamshauri yule jamaa atoke nje ya benki ili afanye mawasiliano (apige simu) ukizingatia hairuhusiwi kupiga simu ndani ya benk.

  Jamaa akatoka nje na alipomaliza kupiga simu akazuiliwa na wale askari kwa sababu muda umeisha (saa tisa na dk ishirini). jamaa yule akawaeleza kwa upole hali halisi na kilichomtoa nje na akawaambia kuwa hivi ninavyozungumza cheque yangu iko mezani kwa meneja kwa hiyo akawasihi aingie maana hawezi kuondoka akaacha cheque mezani kwa meneja.

  Wale askari wakamzuia na mmoja akawa anamtukana na kumwambia mambo ya cheque wao hawajui wanachojua ni kuwa hutoingia. Ikafikia yule mtu uvumilivu ukamshinda wa yale matusi na mbaya zaidi wakamkaba na kumwambia kuwa wanaweza wakamwita jambazi tena wakamtengua miguu kwa risasi.

  Mmoja wao akamkwida na kumkaba koo. Jamaa kuona hivyo uvumilivu ukamshinda naye akamshika, askari mwingine akakoki bunduki yake risasi tayari kwa kumpiga "kumtengua miguu yote miwili". Pakatokea patashika pale, wakati jamaa akijiandaa kupiga, mara Meneja wa benki akatokea, jamaa akajieleza kilichomkuta na wale askari wakaishia kutukanwa kama watoto wadogo na meneja wa benki.

  Jamani wana jamvi, huyu mtu ni msomi tena mwenye heshima zake anatendewa hivi je walala hoi ambao hawajui haki zao wanatendewaje? Mheshimiwa Said Mwema unafanya nini katika mazingira kama haya? Hawa askari walishamwona huyu mtu tangu saa tano asubuhi, akaingia ndani mpaka kwa meneja na kwa bahati akawa anafahamiana na meneja.

  All in all anatendewa hivi. Duh
   
 2. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #2
  Nov 24, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Akili za polisi wote nafikiri zinafanana! wanadhani jamaa alitaka kuandamana!

  Pumbavu zao Mwema na Mbwa zake!
   
 3. WAFU FM

  WAFU FM Member

  #3
  Nov 24, 2011
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hiyo ni kesi moja tu bado kuna kesi nyingi tu huku mitaani, kama wameweza kubaka waonjwa unategemea nini kwa askari kama hao ikiwa mabosi wao wanapiga pesa tu usiku kucha
   
 4. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #4
  Nov 24, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,626
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Very sad!
   
Loading...