Kwa hili January Makamba alishatuonesha tangu mapema kuwa EL ni mtu wa namna gani

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,531
Nafasi ya Urais ni nafasi ya hadhi na heshima kubwa. Unapoiomba hupaswi kufanya michezo ya kuigiza. Huu utaratibu wa kuratibu watu, kuwasafirisha, kuwapa posho na ubwabwa waje kukuomba kugombea ni michezo ya kuigiza ambayo ni aibu kubwa.

Kila mgombea ana uwezo wa kutengeneza watu wa kumuomba kugombea lakini wengine hatufanyi hivi kwasababu tunaheshimu nafasi tunayoiomba na tunaamini kwamba haipaswi kutafutwa kwa ulaghai na maigizo.

Ni aibu sana kutumia shida na njaa za watu kisiasa. Ni aibu sana kukusanya vijana na wazee wa watu na kuwapangia viti na mahema na kuwapa pesa halafu pesa na kuwapiga picha. Ukiona mtu anatafuta nafasi ya uongozi kwa ujanja na ulaghai ujue atatawala kwa ujanja na ulaghai.

Viongozi wanaokubalika na watu hawahangaiki kupanga Viti na mahema na kuwapiga picha watu wanaowakubali. Mgombea anayehaha na kutumia pesa nyingi kuonyesha anakubalika ukweli ni kwamba hajiamini. Kama unakubalika huwezi kuratibu makundi na kuyalipa na kuwapiga picha na kuita waandishi wa habari waje kushuhudia. Hizo ni mbinu za mfa maji.

Naamini Chama changu hakitatishwa na nguvu za maigizo. Tunataka uongozi safi unaomuogopa mungu. Tunataka uongozi wenye uadilifu na fikra mpya za kuisogeza mbele Tanzania. Tunataka viongozi watakaomaliza shida za Watanzania sio wanaozitumia shida hizo kisiasa
Hata Mzee Makamba, pamoja na umri wake wa miaka 75, leo akiwa na pesa za kumwaga anaweza kutengeneza makundi yakamuombe kugombea Urais.

Ifike mahali katika nchi yetu tuache hii michezo. Tukiendelea na mambo haya, tunatengeneza taifa linaloendeshwa kwa propaganda tu. Watu wanaotaka kuomba nafasi ya Urais wanapaswa kuwa na ujasiri na wanapaswa kujiamini na kusema wanataka nafasi hiyo na wana fikra gani mpya bila kutumia pesa kuonyesha kwamba wanagombea kwasababu wanahitajika na watu. Uongozi thabiti na shupavu hautokani na michezo ya kuigiza.

January Makamba

Jahazi hiloooooo linaanza kuzama kwani limesha tobolewa...Naona wasafiri wameamua kila mtu kunyakua ubao wake kiana....Na kuwa potelea mbali 'liwalo na liwe' kila mtu kivyake:)

I looooove this movie..Wacha nikanunue popcorn wazee narudi...
teh teh
 
Juzi nilisikia Muhongo anataka uraisi. Tena ndani ya CCM.
Then,that explains where is escrow money. Kapata wapi pesa za uchaguzi? Alikuwa hana kitu mwaka mmoja uliopita zaid ya hela ya mboga.
Zaidi, nashangazwa na raisi kutokemea hawa watu ambao hawafai anahangaika na lowassa.
Lowassa na Muhongo yupi bora?

Tanzania ni ya wamaskini wa fikra na viongozi na tutabaki hapa hapa.
 
January Makamba katika ubora wake

Kwanu Januzaj yeye hajawai kuhonga?, nilipata kusoma kwenye gazet la Mwananchi siku za nyuma kuna wajumbe aliwazawadia Smartphones,lakini pia Yule Mzee Ma-rope mkubwa mwaka 2010 aliibariki Rushwa,na huyu Januzaj hakutoa rushwa jimboni kwake?katika siasa zao watu wa CCM rushwa ni faradhi,asilielie
 
Aise huyu Januari ameninyang'anya tonge mdomoni.Nimekuwa najiuliza sana kwanini EL anatumia ujanja ujanja huu? Kwa nini hajiamini? Nani anamshauri? Anavyozidi kutumia fedha nyingi sana kujinadi ndivyo anavyozidi kupoteza kura..Mzee EL taratibu hii kasi wapiga kura watakshtukia, nguvu ya pesa imepitiliza.TUTAANZA KUJIULIZA MASWALI KWA NINI UNATUMIA NGUVU NYINGI KWENDA IKULU.Umesahau usemi wa J.K.Nyerere kuhusu mtu yeyote anayetumia nguvu sana na pesa kwenda Ikulu.........
 
Angalau amempa za uso huyu jambazi sugu na fisadi papa lowasa. Yaani lowasa hawezi hata kutoa hoja yoyote yeye zinaongea pesa tu. Sijui ikulu kuna biashara gani mpaka atumie mavi lini.
Pamoja na hayo namtahadharisha makamba kuwa urais ni zamu ya wakristo na ni zamu ya wazanzibar, msiniulize tutapataje mzanzibari mkristo wa kuweza kuwa rais mi sijui itakuwaje
 
January makamba kwanza arudishe cheti cha watu alichotumia kuingilia form 5 baada ya kupata div 0 form 4

January Makamba japo ni mshirikina sana na ana kombinenga ya waganga lakini kutokana na Madhambi aliyofanya kipindi akiwa ikulu si rahisi wapitishe Jina lake, mtakumbuka kuwa aliupora mladi wa Sugu pia alikuwa akipiga 10% percent kwa kila kampuni ya uwekezaji wanataka kuja kuonana na Rais, watu wa ikulu wanajua dili zote za January mapungufu yake yapo bayana kamati kuu hawawezi kumpa nafasi kabsa, pia amekuwa akipokea pesa Haramu toka kwa mchepuko wa Mdogo wake Mwanvita ambaye anachepuka kule ikulu ya kenya pia na Rostam Aziz, haya ni machache tu huyo kijana ana vioja vingi ndiyo maana hata kule jimboni kwake hawamtaki kabsa.
 
Huyo kwanza anapaswa achunguzwe na takukuru amepiga dili nyingi kimya kimya na ana pesa nyingi sana anaziandaa kununua njia kisha kuzitumia kuchafua wengine sanjari na kutafuta waganga zaidi.
 
January makamba kwanza arudishe cheti cha watu alichotumia kuingilia form 5 baada ya kupata div 0 form 4

January Makamba japo ni mshirikina sana na ana kombinenga ya waganga lakini kutokana na Madhambi aliyofanya kipindi akiwa ikulu si rahisi wapitishe Jina lake, mtakumbuka kuwa aliupora mladi wa Sugu pia alikuwa akipiga 10% percent kwa kila kampuni ya uwekezaji wanataka kuja kuonana na Rais, watu wa ikulu wanajua dili zote za January mapungufu yake yapo bayana kamati kuu hawawezi kumpa nafasi kabsa, pia amekuwa akipokea pesa Haramu toka kwa mchepuko wa Mdogo wake Mwanvita ambaye anachepuka kule ikulu ya kenya pia na Rostam Aziz, haya ni machache tu huyo kijana ana vioja vingi ndiyo maana hata kule jimboni kwake hawamtaki kabsa.
 
Unatafuta miguu kwa nyoka? Ndani ya ccm hakuna mwenye hofu ya Mungu! Hata wewe mtoa mada, vinginevyo ungeshatoka! Maana ccm si mama yako!
 
kupingana huku kwa hoja kungekuwa ktk vyama vichanga tayari vingeshasambaratika na kuitana wasaliti, navishauri baadhi ya vyama.....viige mazuri ya CCM na wayatupilie mbali madudu ya CCM ambayo hayapaswi hata kidogo kukaribishwa. kwa kufanya hivi kutaimarisha umoja, mshikamano, demokrasia na kukubali na kukaribisha changamoto hai
 
Nafasi ya Urais ni nafasi ya hadhi na heshima kubwa. Unapoiomba hupaswi kufanya michezo ya kuigiza. Huu utaratibu wa kuratibu watu, kuwasafirisha, kuwapa posho na ubwabwa waje kukuomba kugombea ni michezo ya kuigiza ambayo ni aibu kubwa.

Kila mgombea ana uwezo wa kutengeneza watu wa kumuomba kugombea lakini wengine hatufanyi hivi kwasababu tunaheshimu nafasi tunayoiomba na tunaamini kwamba haipaswi kutafutwa kwa ulaghai na maigizo.

Ni aibu sana kutumia shida na njaa za watu kisiasa. Ni aibu sana kukusanya vijana na wazee wa watu na kuwapangia viti na mahema na kuwapa pesa halafu pesa na kuwapiga picha. Ukiona mtu anatafuta nafasi ya uongozi kwa ujanja na ulaghai ujue atatawala kwa ujanja na ulaghai.

Viongozi wanaokubalika na watu hawahangaiki kupanga Viti na mahema na kuwapiga picha watu wanaowakubali. Mgombea anayehaha na kutumia pesa nyingi kuonyesha anakubalika ukweli ni kwamba hajiamini. Kama unakubalika huwezi kuratibu makundi na kuyalipa na kuwapiga picha na kuita waandishi wa habari waje kushuhudia. Hizo ni mbinu za mfa maji.

Naamini Chama changu hakitatishwa na nguvu za maigizo. Tunataka uongozi safi unaomuogopa mungu. Tunataka uongozi wenye uadilifu na fikra mpya za kuisogeza mbele Tanzania. Tunataka viongozi watakaomaliza shida za Watanzania sio wanaozitumia shida hizo kisiasa
Hata Mzee Makamba, pamoja na umri wake wa miaka 75, leo akiwa na pesa za kumwaga anaweza kutengeneza makundi yakamuombe kugombea Urais.

Ifike mahali katika nchi yetu tuache hii michezo. Tukiendelea na mambo haya, tunatengeneza taifa linaloendeshwa kwa propaganda tu. Watu wanaotaka kuomba nafasi ya Urais wanapaswa kuwa na ujasiri na wanapaswa kujiamini na kusema wanataka nafasi hiyo na wana fikra gani mpya bila kutumia pesa kuonyesha kwamba wanagombea kwasababu wanahitajika na watu. Uongozi thabiti na shupavu hautokani na michezo ya kuigiza.

January Makamba

Ni kweli hata mimi nina hofu kubwa.
 
Back
Top Bottom