Kwa hili jambo nitamlaumu sana mama yangu hapa duniani

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,652
14,247
Mama yangu kiukweli toka nikiwa mdogo alikuwa anaonesha mapenzi makubwa sana kwangu na dada na wadogo zangu. Ingawa ilikuwa ngumu kubaini nani anapendwa sana ktk familia ya watu 5 wa kike 3 wa kiume wawili. Kila mtu aliamini anapendwa sana.

Tulipoanza kukua niligundua mama alikuwa akinipenda zaidi ingawa mwanzoni sikugundua hilo. Mara nyingi alipenda kunituma na kunipa kazi mbalimbali.

Mwanzoni nlihisi ananichukia. Kazi nyingi alipenda nifanye pamoja na kuwa na dada wa kazi yeye alitaka tufue nguo zetu wenyewe na vyombo alituwekea zamu wote kuosha wa kike na wakiume.

Mama alinifundisha kufanya kazi, kujiamini na kuamini nachoamini, kupenda shule, kuwa mtu mwema n.k

LINALONIFANYA NIMLAMU leo mama yangu ni kuwa katika mahusiano yetu kama mama na mwanaye hakunifundisha MATUSI. HILI KILA SIKU NIKIKAA NAWAZA SANA. Kwanini hakunifundisha matusi kama wenzangu wengi ambao walifundishwa na wazazi wao na jamii yao kwa ujumla?

Mpaka leo huwa nikitukanwa sijui kukasirika, sijui kutukana back...nacheka tu. Wakati wenzangu wanamwaga matusi kama maporomoko ya mafuriko kuelekea bondeni.

Namlaumu mama namlaumu pia baba. Baba simlaumu sana maana yeye alikuwa mtu wa safari za kikazi nje ya nchi. Tulibaki sana na mama.

Yeye kwanini hakuona umuhimu wa kunifundisha matusi?
 
...........LINALONIFANYA NIMLAMU leo mama yangu ni kuwa katika mahusiano yetu kama mama na mwanaye hakunifundisha MATUSI. HILI KILA SIKU NIKIKAA NAWAZA SANA. KWA nini hakunifundisha matusi kama wenzangu wengi ambao walifundishwa na wazaz wao na jamii yao kwa ujumla? .................

Hapo kwenye RED mkuu napata shida kuamini. Hivi ni mzazi yupi anaweza kumfundisha mwanaye MATUSI?
 
Mm hata neno K nalitamkaga kwa kupunuza sauti inapobidi ila sijui matusi na mdomo wangu mzito sana
 
Kila Siku Huwa Nasema Hakuna Anayezaliwa Na Tabia Mbaya Ila Mazingira Utakayoishi Ndiyo Yatakufanya Uchague Namna Ya Kuishi Na Chanzo Cha Yote Ni Jamii Yetu Ndugu Marafiki
 
Hivi Gudume una matatzo gani ww ndg yangu? Kila cku unakuja na jpya...punguza hzo sarakasi kjana
 
Mama yangu kiukweli toka nikiwa mdogo alikuwa anaonesha mapenzi makubwa sana kwangu na dada na wadogo zangu. Ingawa ilikuwa ngumu kubaini nani anapendwa sana ktk familia ya watu 5 wa kike 3 wa kiume wawili. Kila mtu aliamini anapendwa sana.

Tulipoanza kukua niligundua mama alikuwa akinipenda zaidi ingawa mwanzoni sikugundua hilo. Mara nyingi alipenda kunituma na kunipa kazi mbalimbali.

Mwanzoni nlihisi ananichukia. Kazi nyingi alipenda nifanye pamoja na kuwa na dada wa kazi yeye alitaka tufue nguo zetu wenyewe na vyombo alituwekea zamu wote kuosha wa kike na wakiume.

Mama alinifundisha kufanya kazi, kujiamini na kuamini nachoamini, kupenda shule, kuwa mtu mwema n.k

LINALONIFANYA NIMLAMU leo mama yangu ni kuwa katika mahusiano yetu kama mama na mwanaye hakunifundisha MATUSI. HILI KILA SIKU NIKIKAA NAWAZA SANA. Kwanini hakunifundisha matusi kama wenzangu wengi ambao walifundishwa na wazazi wao na jamii yao kwa ujumla?

Mpaka leo huwa nikitukanwa sijui kukasirika, sijui kutukana back...nacheka tu. Wakati wenzangu wanamwaga matusi kama maporomoko ya mafuriko kuelekea bondeni.

Namlaumu mama namlaumu pia baba. Baba simlaumu sana maana yeye alikuwa mtu wa safari za kikazi nje ya nchi. Tulibaki sana na mama.

Yeye kwanini hakuona umuhimu wa kunifundisha matusi?

Nimekutukana kimoyo moyo aisee....cheka kidogo basi....
 
Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom