Leo nimerudi nyumbani mapema. Nikakaa siting room, mm mpenzi wa music bila kujali music wa aina gani mm napenda tu, ijapokuwa singeli tu ndio sipendi. Akaja mwanangu analia ananiambia toa huo, toa hua, toa huo, nikamuuliza unataka nini anasema nimeoooooona!!!!!! Nikauliza tena eti !!!!!! nimeuooooooooona kama mara saba hivi sikuelewa kitu ikabidi nimuite mdada wa kazi amsikilize mwanangu. Yeye akamuelewa kumbe anataka wimbo wa nimeuona mkono wa bwana wa jamaa mmoja anaitwa goodluck. Baada ya kuwekwa huo wimbo amani ikapatikana nyumbani. Nimejifunza kitu kwakweli