Kwa hili Gazeti la Mwanahalisi liwaombe radhi Watanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa hili Gazeti la Mwanahalisi liwaombe radhi Watanzania

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by mpigauzi, Jul 28, 2012.

 1. m

  mpigauzi JF-Expert Member

  #1
  Jul 28, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Taarifa iliyoandikwa na gazeti la Mwanahalisi kumponda Katibu wa nishati na madini imeonesha Gazeti hili liliandika bila kufanya utafiti. Ukweli halisi tumeupata siku bajeti ilipowasilishwa na Prof Mhongo. Ni vema gazeti hili liwaombe radhi watanzania. Soma habari yenyewe:

  Richmond mpya wizara ya nishati

  [HR][/HR]
  [​IMG]
  Na Jacob Daffi - Imechapwa 25 July 2012

  [​IMG]


  KATIBU Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi anakabiliwa na lundo la tuhuma ikiwa ni pamoja na kilichoitwa kujipa mamlaka ya kuendesha Shirika la Umeme la Taifa (Tanesco), imefahamika. Aidha, Maswi anatuhumiwa kushinikiza kusimamishwa kazi Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, William Mhando bila kufuata taratibu na kanuni za ajira yake.

  Katibu mkuu huyo anatuhumiwa pia kukiuka baadhi ya taratibu, ikiwamo kufanya manunuzi kinyume cha sheria na kuingiza shirika katika mikataba tata. Taarifa zinasema Maswi ndiye aliyeshinikiza Mhando kusimamishwa kazi kwa maslahi binafsi. Uchunguzi wa MwanaHALISI unaonyesha kuwa bodi ya wakurugenzi ya Tanesco haikutaka kumfukuza Mhando hadi ipate kwanza baraka za mamlaka ya uteuzi (rais); lakini shinikizo lilitoka kwa Maswi.

  Mwenyekiti wa bodi ya shirika hilo, Jenerali Robert Mboma amethibitisha kufanyika maamuzi hayo bila kufuata taratibu.
  "Ni kweli, kulikuwa na hoja ya kumsimamisha kazi Mhando, lakini nilisema uamuzi usitangazwe mpaka nimpe taarifa Mhe. Rais Jakaya Kikwete; naye anipe kibali kwa sababu yule ni mteuliwa wake…lakini ndiyo hivyo tena. Ikatangazwa kabla ya Jumatatu ya 16 Julai," ameeleza.

  Lakini kiongozi mmoja ndani ya bodi ya Tanesco ameeleza, "Huyu bwana ndiye amekuwa mtendaji wa Tanesco. Jambo hili na mengine ambayo bado hayajafumuka, yamemuudhi sana mwenyekiti." Akitaka kuthibitisha madai hayo, mtoa taarifa amesema Maswi ndiye anahusika na kuipa kazi kampuni ya BP (T) Ltd., ya kusambaza mafuta ya kuzalishia umeme wa IPTL, yenye thamani ya zaidi ya Sh. 28 bilioni.

  Taarifa zinasema ni Maswi aliyeagiza BP kuuza mafuta yake kwa Tanesco wakati kampuni hiyo ilienguliwa kwenye zabuni; jambo ambalo ni kinyume cha sheria ya manunuzi ya umma (PPRA) ya mwaka 2004. Sakata la Richmond ambalo linaendelea kuitesa serikali, lilitokana na kampuni hiyo kupewa mkataba wa kufua umeme kwa upendeleo baada ya kushindwa kwenye zabuni.

  Inadaiwa Maswi alifanya maamuzi kama hayo kwa BP, tena bila kushirikisha Mhando. Taarifa zinasema pia ni kwa "vitendo vya hatari vya aina hiyo, vya kuingiza shirika katika mgogoro wa kisheria," Jenerali Mboma ameamua kuripoti kwa Rais Kikwete.
  Bali Maswi aliwaambia waandishi wa habari juzi Jumatatu, ofisini kwake, Dar es Salaam kuwa hahusiki na tuhuma hizo kwa vile alipoingia wizarani hapo mchakato huo ulikuwa tayari umeanza.

  Lakini alipoulizwa na MwanaHALISI, aligoma kuzungumzia suala hilo, badala yake alitaka mwandishi kwenda ofisini kwake kuchukua taarifa aliyosambaza kwenye vyombo vya habari. Hata hivyo, nyaraka zilizopo zinathibitisha jinsi Maswi alivyokuwa wakala wa BP, mratibu, msimamizi, mlipaji na mnunuzi wa mafuta hayo yaliyonunuliwa kwa fedha za umma.

  "Ndugu yangu, katika mazingira haya, ni nani anayepaswa kuchunguzwa kati ya katibu mkuu wizara ya nishati na madini, Eliakim Maswi na Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, William Mhando," amehoji mjumbe mmoja wa bodi ya Tanesco. Taarifa zinamuonyesha Maswi akipokea hati ya kabla ya malipo – Profoma Invoice – iliyoambata na ujumbe wa barua pepe kutoka meneja masoko ya BP (sasa Puma Ltd), Machumani Shebe uliosema, "…itakuwa ni vema zaidi kama utaweza kutupatia nyaraka rasmi za jambo hili kiofisi."
  Anasema,

  "Naomba tupate barua ya uthibitisho wa malipo kutoka wizarani kwako ili kuwa na uhakika wa malipo. Tunataka pia utupatie LPO (ankara ya malipo) ya kiwango cha mafuta kitakachosambazwa." Akiandika kwa njia ya kushukuru, Shebe anasema, "Tunakushukuru kwa kutupatia biashara hii na tunatarajia kusikia kinachoendelea kutoka kwako hivi mapema iwezekanavyo."

  Mara baada ya kupata ujumbe huo kutoka BP, Maswi alimwandikia ujumbe naibu mkurugenzi mtendaji wa Tanesco anayeshughulikia uzalishaji, Boniface Njombe, tarehe 12 Julai 2012 kumwamuru kuandaa malipo hayo haraka iwezekanavyo. Barua ya Maswi kwenda kwa Njombe, ilinakiliwa kwa Mhando na Decklan Mhaiki, ambaye ni naibu mkurugenzi wa shirika anayeshughulikia usambazaji umeme.
  Kwa kasi ya aina yake, siku hiyohiyo ya 12 Julai, Njombe alimwagiza Anetha Chengula wa idara ya uhasibu, kuandaa malipo kwa kile alichoita, "Utekelezaji wa maelekezo ya Maswi."

  "Bila shaka unakumbuka juu ya jambo hili. Tupo wizarani hapa na tumepokea hati malipo kutoka kwa katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini iliyotoka Puma (BP) watakaosambaza HFO kwa ajili ya mitambo ya IPTL," ameeleza Njombe katika barua yake kwa Chengula. Amesema, "Malipo hayo yatafanywa na wizara ya nishati na madini kama ambavyo tulikubaliana. Hivyo unatakiwa kuandaa malipo ya mafuta hayo haraka kwa msambazaji na unijulishe."

  MwanaHALISI lilipomuuza Mboma kuhusu madai hayo, alikiri kuwa shirika lake halijawahi kuipa kazi kampuni ya BP. Alisema, "Mimi ninachofahamu ni kwamba TANESCO ina-deal (inashughulika) na makampuni yale matatu yaliyokuwa na sifa. Sifahamu jingine nje ya hapo."

  Mbali na kulazimisha kulipwa fedha hizo, Maswi amedaiwa kuzuia Sh. 36 milioni kutoka Wizara ya Fedha (Hazina) ambazo ni sehemu ya fedha zilizoombwa na Tanesco serikalini. Tanesco iliomba, tarehe 22 Septemba 2011, Sh. 136 bilioni kwa ajili ya gharama za kuendesha mitambo ya dharura ya umeme. Ilitarajia kuzirejesha baada ya kupata mkopo wake mkubwa wa Sh. 408 bilioni ambazo shirika hilo liliahidiwa.

  Akiwa kaimu katibu mkuu wa wizara hiyo, Maswi anadaiwa kukata Sh. 36 bilioni na kuipa Tanesco Sh. 100 bilioni. Inadaiwa alitoa maelezo kuwa kiasi kilichokatwa kitafuta mkopo wa Sh. 20 bilioni katika benki ya CRDB. Katika barua yake ya 28 Septemba 2011 yenye kumb. Na. AB.88/286/01/15 kwenda kwa mkurugenzi mtendaji wa Tanesco, Maswi anaeleza kuwa kiasi kilichobaki cha Sh. 16 bilioni kingetumika kununulia mafuta mazito kwa mitambo ya IPTL kwa mwezi Oktoba 2011 kutoka Puma/BP.

  Mhandisi Mhando alisimamishwa kazi 13 Julai 2012 pamoja na maofisa watatu waandamizi – Naibu Mkurugenzi, Huduma za Shirika, Robert Shemhilu, Ofisa Mkuu wa Fedha, Lusekelo Kassanga na Meneja Mwandamizi Manunuzi, Harun Mattambo kwa kilichoitwa "madai ya matumizi mabaya ya madaraka na ubadhilifu."


  Gazeti toleo lenye makala hii
   
 2. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #2
  Jul 28, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Hili gazeti ni bingwa la kuandika udaku na majungu siku zote uwa naliweka kundi moja na KIU, UWAZI. leo baada ya bajeti kusomwa limeabika kwa majungu.
   
 3. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #3
  Jul 28, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Ritz,
  Kwa mtu kama wewe ambaye una mahaba na Uhuru,Mzalendo, Tazama, na Habari leo, kamwe huwezi kuona thamani ya Mwanahalisi. Kwa Tanzania yetu hii, usipokuwa na mahaba na Mwanahalisi na Raia Mwema, basi kamwe hutoweza kufikiri nje ya box, na siku zote utaona contents za magazeti haya ni upuuzi kwako. Hili linasababishwa na uwezo wako, mazoea uliyonayo, akili yako ulivyoitune, na hasa pale yanapofunua yale maovu unayoyasapoti katika jamii, ni hakika utaichukia.
   
 4. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #4
  Jul 28, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Sasa nani wa kuomba radhi kati ya Mwanahalisi na Muhongo?
  Au Muhongo ni Mungu wako mazee?
   
 5. Msalagambwe

  Msalagambwe JF-Expert Member

  #5
  Jul 28, 2012
  Joined: Jul 11, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Hivi katibu mkuu akiongea basi anachosema ni ukweli?

  Naona bado umedwell kwenye enzi za kila kisemwacho na viongozi wa serikali ni kweli.

  Umeandika bila kufanya uchunguzi,
  Uchunguzi wako ni maneno ya mtu mmoja ambaye yuko huru kusema lolote ukiwamo uongo,
  ili mradi unga wake na wa wale waliomuweka hautiwi mchanga.
   
 6. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #6
  Jul 28, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kinachoniuma ni kwamba i thot ccm were the corrupt thugs.. I stand corrected... Ccm chadema wote ni wala rushwa na wote hawaaminiki...cant trust neither of them
   
 7. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #7
  Jul 28, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Mkuu mie sio bendera fuata upepo ebu niambie wewe mwenye uchungu na nchi hizo tuhuma na makosa ya Eliakim Maswi yako wapi mie nachofahamu huyu Katibu Wizara Nishati na Madini Eliakim Maswi uamuzi wake umeokoa bilioni 3 kwa kila juma pesa ambayo ilikuwa inakwenda mifukoni kwa wajanja.
   
 8. m

  mpigauzi JF-Expert Member

  #8
  Jul 28, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu hapa haitakiwi ushabiki, angalia content ya habari yenyewe. Hatukatai Gazeti ni zuri, na kwa uzuri wake ni rahisi kuamininiwa na wananchi. Ingekuwa UHURU NA MZALENDO tusingehangaika. Ila kwa hili ni vema watumie busara kuomba radhi kwani wamejichafua kutetea ufisadi
   
 9. m

  mpigauzi JF-Expert Member

  #9
  Jul 28, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu pitia hotuba ya msemaji wa kambi ya upinzani. Imewekwa humu. Mnyika kaeleza ufisadi wote. Ukisema hata CDM tusiwaamini, mie sitakubaliana na wewe
   
 10. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #10
  Jul 29, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  lakini wizara hii ina nini?je wabunge kama wanaingia kwenye rushwa kuna nini tena?
   
 11. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #11
  Jul 29, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  sijaisoma bana
   
 12. Mingoi

  Mingoi JF-Expert Member

  #12
  Jul 29, 2012
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 10,634
  Likes Received: 2,344
  Trophy Points: 280
  Mwanahalisi lilikuwa ni miongoni mwa mkakati wa kukwamisha bajeti ya wizara, pesa bana?
   
 13. y

  yaya JF-Expert Member

  #13
  Jul 29, 2012
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 694
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu pole sana.
  Kwa mawazo yako wabunge ni watakatifu?
  Wabunge hao ambao baadhi yao wanateuliwa kugombea ubunge kwa rushwa? Wanachaguliwa kwa rushwa, halafu unashangaa kwamba wanapokea rushwa?
  Nasema tena pole mkuu.
   
 14. kbosho

  kbosho JF-Expert Member

  #14
  Jul 29, 2012
  Joined: Jun 4, 2012
  Messages: 12,505
  Likes Received: 3,314
  Trophy Points: 280
  duh ya kwel hayo?
   
 15. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #15
  Jul 29, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Umelisahau Tanzania Daima katika hilo kundi.
   
 16. b

  beyanga Senior Member

  #16
  Jul 29, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 184
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ​waziri na katibu hawana jipya tayari chadema ilishayasema kwenye bajeti yake
   
 17. b

  beyanga Senior Member

  #17
  Jul 29, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 184
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  matatizo sio wizara ni kikwete kawekeza kwenye hiyo wizara kupitia mtoto wake ridhiwani hakuna jipya pale ni mbwa mzee aliyepigwa poda ilimradi waziri antoka ccm hawezi kufanya lolote yote ni majizi yanaiba kwa wakati tofauti ngeleja kafanywa nini si bado yuko mitaani?QUOTE=zomba;4332489]Umelisahau Tanzania Daima katika hilo kundi.[/QUOTE]
   
 18. b

  beyanga Senior Member

  #18
  Jul 29, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 184
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ​lakini sio kama uhuru na mzalendo mawakala wa tiss na nyie akina ritz hamna jipya pesa ya lumumba inawazuzua mkawadanganye watu wa bagamoyo labda elimu tunawapa watz mpaka kieleweke
   
 19. b

  beyanga Senior Member

  #19
  Jul 29, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 184
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ritz kashomeshwa ccm kivukoni haoni wala hasikii ni kansa ya ubongo ukishaipenda ccm maana ni sawa na dini ya mashetani hawajui kama kuna mungu wala ubinadamu
   
 20. Kingcobra

  Kingcobra JF-Expert Member

  #20
  Jul 29, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,008
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Baadhi ya wabunge walitumia pesa kuteuliwa kuwa wagombea ubunge, walitumia pesa kuhonga wapiga kura ili wawachague sasa watashindwaje kupokea rushwa ili warejeshe gharama hii. Nachofurahi ni kwamba hotuba ya kambi rasmi ya upinzani iliyosomwa na mhe. Mnyika ipo very clear kuhusu mazingira yaliyo dhahiri ya rushwa katika sakata zina la ununuzi wa mafuta unaotetewa na baadhi ya wabunge wakiwemo akina ole sendeka. Kilichonifurahisha kingine ni namna mbunge wa Rombo alivyoeleza jinsi rushwa isivyo na mipaka ya chama, kabila, rangi, itikadi, n.k. Kwa kusema hivyo, alimaanisha kwamba hata wabunge wa cdm wanaweza kuwa involved katika rushwa.
   
Loading...