Kwa hili Fransis Kiwangwa, hatuwezi tena kupinga malipo ya DOWANS

MBUFYA

JF-Expert Member
Aug 15, 2011
445
68
Kituo cha haki za binadam kupitia kiongozi wake mwanaharakati ndg fransis kiwango amekubali kusitisha maandamano ya kupinga malipo ya dowans kwa sababu moja tu miongoni mwa sababu kadhaa zilizo tolewa Kova.

Sababu hiyo ni kuwa na tetesi za tishio la kuwepo kwa kundi la kigaidi la alshabab. hivyo akawaomba wote waliojiandaa kuandamana leo, atawatangazia maandamano pale hali ya usalama itakapo rejea nchini. Hoja ni kwamva, ni lini kova atatangaza kuwa hal ya nchi ni salama?

Je malipo ya DOWANS yatasitishwa?
 
yaani leo nilijiandaa kabisaaa!
Duu haya bwana na mbona mpira wa yanga na simba unachezwa alshababu hawafiki huko!
 
Hapa ndipo ninaposhindwa kuelewa mambo yanavyokwenda hapa nchini kwetu,pilisi wanafanya kazi gani kuzuia hali hiyo ya wasiwasi wa tishio la ugaidi ili watu waandamane?

Hii hoja inachukuliwa tu kama ndio kigezo cha kutotaka watu waandamane maana shughuli nyingine zinaendelea kama kawaida iweje iwe kwenye maandamano tu?
 
mi nadhani kova angetuambia ni jitihada gani wanazo zichukuwa kuwaangamiza hao magaidi kwani ukisema unaimarisha ulinzi ni vigumu na huo usalama hautarejea nchini na itachukuliwa kama kigezo cha kuzuia maandamano yoyote yenye maslahi kwa taifa.
watanzania, hizo pesa ni nyingi mmno mi nidhani hata kova anamgao wake hapo kama hao dowans watalipwa.
 
Hawa DOWANS wanauhusiano gani na al-shabab.
Nina hofu tunafanya biashara na magaidi ndio maana wakitutapeli tunanywea.
 
Heri al shabaab waje maana hata vyombo vya usalama vimeingia kwenye siasa....waje tu watuchape mchana kweupe maana hata pesa zao zinapitishwa hapa hapa na hao hao wanasiasa kwa hiyo wanatujua udhaifu wetu wote!hakuna cha kova wala inteligensia waje watufunze utawala na ulinzi!!
 
mchumia-tumbo utamjua tu. nchi hii hata kuwa na elimu ni aina ya ujinga kama si upumbaf.
 
Deni la Dowans lazima lilipwe. Pia tuheshimu ushauri wa kiusalama unaotolewa na vyombo vya dola.
 
Mimi nilijua kama alikuwa hajafikia thamani alioahidiwa kupewa na magamba, lakini alipozitia mkononi tu kasingizia Al-shabaab.

Wananchi mnakiwa kuandamana wenyewe, maana wasomi wengi wanaogopa kipigo na rumande.
 
Kwa jinsi Polisi ya nchi hii ilivyo, wako tayari kama wangeng'ang'aniza hayo maandamano kulipua hata bomu moja wao wenyewe kisha waseme si tuliwaambia Al shabab watalipua?
Binafsi nimekosa kabisa imani na jeshi letu kwa vile limekubali kutumiwa dhidi ya wanaowalinda(wananchi)
 
Hao Al shabaab wameibuka baada ya kutangazwa maandamano? Hiyo inteligencia imeanza lini? Mbona ishu kibao zinatokea na hakuna cha taarifa za kiintelijensia wala nini,watu wanachota mahela bank'madin na udongo pembe za ndovu,wanyamapori tena wakiwa hai wanatoroshwa kwa ndege za jeshi tena la nje bila taarifa' magogo yanapelekwa china kwenye makontena kinyemela na intelijensia ipo,hii nahisi ni trick ya kuzimisha maandamano,sidhani kama kuna kitu kama hicho.
 
Damn kwa stili hii Dowans watachukua chao 111billions
Hawawezi.........zitafika mpaka 200Billion........kitakachofanyika ni kwamba watalipwa kwa style ya wizi.....wtaruhusiwa kuiba EPA style.

Watch this space.
 
Na hao Dowans kuna sababu zipi za kutowalipa?
drunk-people-3-400x282.jpg
 
Back
Top Bottom