Kwa hili dada zetu mnatudanganya.. au mmetuzidi maujanja!

Tunaamini kuwa mwanamke anahitaji kuwa na 'hisia' na mtu kumbe wapo wanawake ambao nao tendo hilo ni kama mazoezi ya viungo tu au kama kashata! wanakula wakiwa na hamu na wakimaliza hata hawakumbuki!

....mmmmh....NSA and one night stand...just saying!

tena hizo NSAs na one ONS za wenzetu mbaya kweli!!!
 
mwanakjj natumaini wewe umeshaishi ulaya...ulaya mwanamke wa kizungu anaweza kuamka siku akasema leo nina hamu na nikitoka hapa naenda kutafuta mwanaume wa kunipunguzia hamu yangu.anatoka anakutana na mtu wanaenda kulala kesho asubuhi kila mtu na zake..tena bora wa ulaya hawataki hela...mwanamke anaweza yeye ndio akanunua pombe usiku kucha mwanaume asitoe hata senti tano na bado mwanaume akaenda kufanya mambo...afrika or bongo ni kua ukipata mwanamke wa namna hiyo lazima atakula hela yako kwanza sana tu ndio utaenda na wewe kumfaidi.. bt siwalaumu wanawake..kuna wakati jamani hata wanawake pia wanakua na hamu ya mwanaume lakini ni yule wa siku moja tu sio baadae kuanza kusumbuana..ile hamu ikiisha basi wanataka waendelee na shuhuli zao...
 
Kaazi kweli kweli! Yaani hata soga tu nazo ziwe zinajadiliwa kwa kutumia sijui ma sample space na ma nini nini? Mweh!

Unachofikiri ni soga si soga, unafikiri tu kwamba ni soga. Au una sample space ya kutosha kuonyesha kwamba unachofikiri ni soga ni soga na si shoga yake soga toka Msoga?
 
Mambo ya usawa siku hizi, kama nyie mnacheat kwa nini sie tuendelee kufa kwa pressure? Uzuri wetu tunafanya mambo kwa akili sio kama nyie mkishaogeshewa maji ya karafuu basi yale ya hiriki hamkumbuki tena. Chezeya wanawake weye!

Mhhh! I didn't know about that. Kumbe akili mu kichwa....Kuna jamaa alinikumbusha muda mrefu kidogo kwamba aligomea kwenda sherehe ambayo mama alikuwa kila akiamuka anaikumbusha maana ilikuwa imekaa kama kumuunga mkono mama kwa mme mwenza. Well, wanaume wengi huwa hawapendi kelele siku hizi, so ni rahisi kumezea. Ila hakuna siri kwenye mambo hayo.
 
msinyong'onyee....huo ndio ukweli.....

Kwamba na wanawake nao wana nyumba ndogo? Ukifa leo tu, mtu huku nyuma hawezi kusubiri hata mwezi upite ashabadilika kuwa uncle kwa watoto zako! Duuh, kufa kufaana.
 
Kutokana na uzoefu wangu wa kuona, huko mitaani na maofisini, (si kwa utafiti rasmi), kwenye ligi ya cheating Wanawake wanawafunga wanaume tatu bila;
  • Wanawake hawatambi wakifanya, na hawapendi ijulikane hata kwa kukisia - hasara ya kujulikana ni kubwa
  • Kwa wanawake kufanya hakuna gharama, kuna incentive kibao kutoka kwa wanao watongoza - Mwanaume ukitaka kufanya hivyo hadi ukague urefu wa wallet yako
  • Wanawake si initiators - hakuna ugumu, ni kukubali tu
  • Wanawake wengi hawawaamini waume/wachumba zao - ni popular belief kuwa wanaume ni wahuni, hii hutoa incentive kwa wanawake kufanya nje wakijua kuwa hata wapenzi/waume zao wanafanya tu
  • Wanaume - hata kama hafanyi; akisingiziwa wako tayari kubeba lawama kwa sababu wao huona kama sifa. Hii huwafanya wanawake waende zaidi kwa lengo la kukomoa.
Tukubali tu, hata statistics za ukimwi zina reveal hii kitu. Yaani kuna wanawake kibao wana ngoma waume zao hawana! Ingawa kuna cases unakuta mwanamke hana ila mwanaume anao, hizo huwa ni rare cases sana ukilinganisha za wanawake wenye ngoma huku mwanaume akiwa mzima.
 
Tulikuwa kwenye kikao kidogo cha wazee kijijini na tukawa tunazungumza mambo mengi. Kama kawaida mambo ya watu kucheat yakajitokeza mara moja kwanza ilikuwa hoja ya "kina nani wanacheat zaidi kati ya wanaume na wanawake". Jibu la kwanza ambalo lilionekana kwa urahisi - bila watu kufikiria sana na lilitoka kwa wanaume tena kwa fahari - ni kuwa wanaume ndio wanacheat sana. Hasa ni kwa sababu kubwa mbili mara nyingi (kama siyo zote) wanaume ndio hutongoza zaidi na pili wanaume wanaonekana wanakodolea macho ""kila chenye sketi kipitacho kikitingishikika". Wakati wanaume wanaendelea kujisifu kauli zetu zilijikuta zinakatishwa na moto wetu kupoozwa kama chuma cha moto kinapotumbukizwa kwenye maji!

"Mnajidanganya tu" alisema dada mmoja kwa sauti ya utulivu huku akiendelea kula kuku wake wa kuchoma. Macho yetu yalimgeukia kwa ghafla na mara moja tukapoteza kujiamini; wanawake wenzie pale kikaoni walimuangalia kwa macho yaliyojaa kila alama ya umbea (mshangao, dukuduku, shuku, kebehi... n.k).

"Tunajidanganya?" mmoja wa wazee pale kikaoni (I swear it wasn't MOI)

Well, dada yule alianza kutuelezea kwa sauti iliyochagua neno moja moja utadhani mashine ya kupigia chapa. Lakini kimsingi alisema mambo yafuatayo ambapo alipomaliza na kurudia kisusunilo kilichobakia mezani baadhi yetu tulitafuta gia za kutokea kikaoni! Alisema kwamba:

a. Wanaume wanadanganywa kirahisi kitandani! - mwanamke anaweza kupiga kelele na kusema maneno yote matamu kiasi cha kumfanya mwanamme afikiri kuwa ndiye aliyebuni na kukiunda kitendo hicho. Mwanamme anavyoitikiwa wakati wa shughuli inamjenga mno "confidence" yake kiasi kwamba hawezi kuamini kabis akuwa mwanamke wake anaweza hata kutoka nje - ambako nako anaweka mbwembwe zilizojaa iliki, mdalasini, limau, pilipili mbuzi, pilipili hoho, karafuu na thyme! Kelele za kitandani zinawapumbaza wanaume na mwanamke mjanda hujua kelele zipi za kuziingiza siku ya kwenda kucheat!

b. Wanaume wanafikiria wanawake wote wanahitaji hisia kufanya tendo: Kuna imani kuwa mwanamke hawezi kwenda na kufanya tendo hilo na mtu yeyote bila kuingiza hisia ndani yake. Yaani, wanaume wanafikiria (tunafikiria) kuwa ni sisi tu tunaoweza kwenda kulala na mwanamke na kesho yake kumfikiria mwingine. Matokeo yake wazo la kwamba mwanamke kwa vile anaonesha anakupenda sana na anakufanyia mambo mengi anapata pia pembeni na labda zaidi ya mtu mmoja haiingii akilini. Tunaamini kuwa mwanamke anahitaji kuwa na 'hisia' na mtu kumbe wapo wanawake ambao nao tendo hilo ni kama mazoezi ya viungo tu au kama kashata! wanakula wakiwa na hamu na wakimaliza hata hawakumbuki!

Yule dada alisema kitu cha kushangaza kuwa wapo wanawake hata hawakumbuki kabisa wanaume waliolala nao; na wengine ndio wale wanaoweza kwenda mahali - hasa kwenye visafari vya kikazi - akajipatia mwanamme wa usiku mmoja (one night stand) na wala asihangaike naye tena wala kutaka kujua alimradi alitumia kinga!

Baada ya kujaribu kubadilisha mazungumzo wazee wazima tuliondoka tukiwa na mawazo sana....

Kwa ufupi.. dada zetu nyie wajanja a.k.a mashapu!!! sijui ni vizuri au vibaya!!

Kaka ina maana uliukuwa hujui hilo? Pole sana. Bahati nzuri huyo dada amekufumbua macho! KODOA
 
Kwenye mambo haya kina data/wanawake huwa ni zaidi siku zote ingawa huwa hawadai credit, ila wao hufanya tu! Credit huenda kwa wanaume;
  • On average wasichana huanza mambo ya ngono mapema (hii ni official) - Yaani msichana mliyezaliwa mwaka mmoja, unapokuwa na girl friend (wa ku-do naye) wako wa kwanza yeye ana boyfriend (wa ku-do naye) wa nne au wa Tano.
  • Wanawake wako more-likely kubadilisha wapenzi wao zaidi kuliko wanaume. Yaani maisha ya kingono yakiisha anza wanawake wanabadirisha wapenzi zaidi kuliko wanaume wanavyobadirisha (kwa wale walio single)
  • Kwa wale wanaoingia kwenye ndoa; Na hii ni muhimu sana. Wanawake wanaoingia kwenye ndoa wameshakuwa na wapenzi wengi zaidi (ex-lovers) kuliko wanaume wanaoingia kwenye ndoa (hii ni official vile vile). Cheating nyingi za wanawake huwahusisha ex-lovers.
 
Ukijumulisha tu, unaua mtu. Hayo mambo ya cheating ni kuacha hivyo hivyo, punishment ni pale unafumaniwa. Na Mungu hawi radhi na mpumbavu. Mwanaume au mwanamke anaweza kucheat akafikiri ni mjanja kumbe siku yake inakuja.

Mwili wako unaufanya kuwa pango la uzinzi na uasherati, halafu unajifiia wewe ni mjanja. (sifa za kijianga)./
 
Tulikuwa kwenye kikao kidogo cha wazee kijijini na tukawa tunazungumza mambo mengi. Kama kawaida mambo ya watu kucheat yakajitokeza mara moja kwanza ilikuwa hoja ya "kina nani wanacheat zaidi kati ya wanaume na wanawake". Jibu la kwanza ambalo lilionekana kwa urahisi - bila watu kufikiria sana na lilitoka kwa wanaume tena kwa fahari - ni kuwa wanaume ndio wanacheat sana. Hasa ni kwa sababu kubwa mbili mara nyingi (kama siyo zote) wanaume ndio hutongoza zaidi na pili wanaume wanaonekana wanakodolea macho ""kila chenye sketi kipitacho kikitingishikika". Wakati wanaume wanaendelea kujisifu kauli zetu zilijikuta zinakatishwa na moto wetu kupoozwa kama chuma cha moto kinapotumbukizwa kwenye maji!

"Mnajidanganya tu" alisema dada mmoja kwa sauti ya utulivu huku akiendelea kula kuku wake wa kuchoma. Macho yetu yalimgeukia kwa ghafla na mara moja tukapoteza kujiamini; wanawake wenzie pale kikaoni walimuangalia kwa macho yaliyojaa kila alama ya umbea (mshangao, dukuduku, shuku, kebehi... n.k).

"Tunajidanganya?" mmoja wa wazee pale kikaoni (I swear it wasn't MOI)

Well, dada yule alianza kutuelezea kwa sauti iliyochagua neno moja moja utadhani mashine ya kupigia chapa. Lakini kimsingi alisema mambo yafuatayo ambapo alipomaliza na kurudia kisusunilo kilichobakia mezani baadhi yetu tulitafuta gia za kutokea kikaoni! Alisema kwamba:

a. Wanaume wanadanganywa kirahisi kitandani! - mwanamke anaweza kupiga kelele na kusema maneno yote matamu kiasi cha kumfanya mwanamme afikiri kuwa ndiye aliyebuni na kukiunda kitendo hicho. Mwanamme anavyoitikiwa wakati wa shughuli inamjenga mno "confidence" yake kiasi kwamba hawezi kuamini kabis akuwa mwanamke wake anaweza hata kutoka nje - ambako nako anaweka mbwembwe zilizojaa iliki, mdalasini, limau, pilipili mbuzi, pilipili hoho, karafuu na thyme! Kelele za kitandani zinawapumbaza wanaume na mwanamke mjanda hujua kelele zipi za kuziingiza siku ya kwenda kucheat!

b. Wanaume wanafikiria wanawake wote wanahitaji hisia kufanya tendo: Kuna imani kuwa mwanamke hawezi kwenda na kufanya tendo hilo na mtu yeyote bila kuingiza hisia ndani yake. Yaani, wanaume wanafikiria (tunafikiria) kuwa ni sisi tu tunaoweza kwenda kulala na mwanamke na kesho yake kumfikiria mwingine. Matokeo yake wazo la kwamba mwanamke kwa vile anaonesha anakupenda sana na anakufanyia mambo mengi anapata pia pembeni na labda zaidi ya mtu mmoja haiingii akilini. Tunaamini kuwa mwanamke anahitaji kuwa na 'hisia' na mtu kumbe wapo wanawake ambao nao tendo hilo ni kama mazoezi ya viungo tu au kama kashata! wanakula wakiwa na hamu na wakimaliza hata hawakumbuki!

Yule dada alisema kitu cha kushangaza kuwa wapo wanawake hata hawakumbuki kabisa wanaume waliolala nao; na wengine ndio wale wanaoweza kwenda mahali - hasa kwenye visafari vya kikazi - akajipatia mwanamme wa usiku mmoja (one night stand) na wala asihangaike naye tena wala kutaka kujua alimradi alitumia kinga!

Baada ya kujaribu kubadilisha mazungumzo wazee wazima tuliondoka tukiwa na mawazo sana....

Kwa ufupi.. dada zetu nyie wajanja a.k.a mashapu!!! sijui ni vizuri au vibaya!!

mie hata cha kuchangia hapo sikioni make mie bado hawajani DO!
 
Back
Top Bottom