Kwa hili, CUF walikuwa wanahitaji madaraka sio kuibadilisha nchi hii...!!

Eiyer

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
28,258
20,709
Wakati wa uchaguzi wa mwaka 2000, vurugu zilizokuwepo Z'bar na baadhi ya maeneo T'bara mpaka zikapelekea maandamano kule Z'bar yaliyopoteza maisha ya watu zilionesha chama cha CUF kitaleta ukombozi!

Lakini baada ya muafaka na CCM pamoja na kupewa nafasi katika uongozi,viongozi wa CUF hawaikosoi tena serikali,kwanini?Hakuna maendeleo yoyote yaliyofanywa,maisha yamekuwa hovyo zaidi,uko wapi uchungu wa CUF?

Au wamepata walichokuwa wanahitaji?
 
Seif alijipima akaona uzee umefika na hajapata madaraka yoyote kwenye serikali akabidi akubali kuolewa na CCM!
 
Saa hizi huwezi tena kuwasikia kama wapinzani,wameshatulizwa na wanatekeleza ilani ya magamba.
 
Wale ni ma opportunist HR type toka lini Mpemba akapigania maisha bora ya Mtanganyika.
 
Mtetezi wa kweli ni yule Bishop anayekwapua 7.2M za walipakodi kila mwezi ili kuwatetea Watanzania!
 
Seif alijipima akaona uzee umefika na hajapata madaraka yoyote kwenye serikali akabidi akubali kuolewa na CCM!
<br />
<br />
wachakuropoka kwa mambo usiyoyajua,unasema maalim seif hajapata madaraka yoyote serikalini,KALAGABAHO seif alikuwa waziri wa elimu ktk smz miaka 6 pia alikua waziri kiongozi sawa nawazirimkuu kwamiaka kadhaa,usikurupuke kama hujui uliza wanaojua wakujuze.
 
ndugu siasa za dunia zimebadilika leo haziendeshwi kwa vurugu hata kama ni mapigano mtapigana mwisho mtarudi kwenye meza ya mazungumzo, kumbuka leo kuna mahakama y kimataifa ukichochea vurugu na watu wa kafa ujue utasimamishwa the hague kujibu mashtaka japo hiki chama cha magwanda wao wanataka wachukue nchi kwa njia ya vurugu japo wanainchi hawawaelewi!!
 
ndugu siasa za dunia zimebadilika leo haziendeshwi kwa vurugu hata kama ni mapigano mtapigana mwisho mtarudi kwenye meza ya mazungumzo, kumbuka leo kuna mahakama y kimataifa ukichochea vurugu na watu wa kafa ujue utasimamishwa the hague kujibu mashtaka japo hiki chama cha magwanda wao wanataka wachukue nchi kwa njia ya vurugu japo wanainchi hawawaelewi!!
<br />
<br />
Watafute wasiojua uwadanganye,hiyo mahakama ya kijeshi ni kwa wale walio kinyume na Wamarekani tu,nani alikuambia amani ya kweli na maendeleo yanapatikana kirahisi hivyo?
 
Ni kiongozi asiye na mamlaka ya maamuzi,kazi yake ni kuhutubia mikutano na kushiriki kwenye dhifa za kitaifa tu,kuhusu maendeleo hilo halimuhusu wapo wengine so matokeo yake upinzani na cuf kwesha kabisa.
 
....Hakuna maendeleo yoyote yaliyofanywa,maisha yamekuwa hovyo zaidi,uko wapi uchungu wa CUF?

Au wamepata walichokuwa wanahitaji?

Kitanda usichokilalia unajuwaje kunguni wake...????

CUF wameunda serikali kule Zanzibar, kwa mfumo waliochaguwa Wazanzibari wenyewe, na hivyo ndiyo ilivyo hata kama hampendi, wa nyinyi wenye uchungu mmeshindwa kuuunda hata halmashauri kule Arusha matokeo yake watu wamekufa na kuumia, mtaweza kuongoza nchi?
Sharti utambuwe kuwa serilkali za pamoja ni style ya ulimwengu siku hizi, vyama chungu nzima vimefanya serikali ya namna kama hiyo, mbali na Afrika hata ulaya na Amerika, upinzani siyo lazima uwe backbencher, siasa za siku hizi za vyama vingi zinabadilika (not static) uzalendo unaonyeshwa mnamna mnavyoendesha serikali na kuweka kando misimamo yenu ya kisiasa kuelekea kwenye siasa za maslahi ya nchi, hivyo ndivyo wanavyofanya conservativi na Lib dem kule Uingereza.

Waulizeni Wazanzibari wenyewe faida wanayoipata na serikali ya Umoja wa kitaifa, halafu ndiyo mpige makelele yenu yasiyo kuwa na mpango!!!!
 
Back
Top Bottom