Kwa hili CHADEMA kina tofauti gani na CCM? Bora kuwa ''non partisan'' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa hili CHADEMA kina tofauti gani na CCM? Bora kuwa ''non partisan''

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ntaramuka, Jul 25, 2012.

 1. Ntaramuka

  Ntaramuka Senior Member

  #1
  Jul 25, 2012
  Joined: May 2, 2008
  Messages: 169
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Chadema kinatazamiwa na wengi kama chama mbadala wa CCM, ambacho kinapoteza imani yake kwa wananchi wengi sasa, (kwa wanaoamini hivi).

  Kama chama mbadala, binafsi, nilitaraji CHADEMA kitakuwa na utofauti na mtangulizi wake, CCM. Wangejifunza kwanini ccm kimeshindwa kuwa chama cha wanyonge, wakulima na wafanyakazi, badala yake kimekuwa chama cha matajiri mabepari. Lakini sasa CHADEMA wanaomba ridhaa ya watanzania kuwa mbadala wa CCM wakati wanafanya mambo yale yale yaliyokifikisha CCM hapa:

  1. Kukumbatia matajiri wahindi na waarabu; hawa wamekuwa wafadhili wakubwa wa CCM kwa muda mrefu huku wakitumia nafasi hiyo kuifisadi nchi hii, mfano Jitu Patel, Manji, R. Aziz nk. Na sasa Chadema wanapita mle mle, mfano M. Sabodo
  2. Makundi ndani ya chama; makundi yamekifikisha CCM hapa hadi kuwasahau wananchi na kupeana vyeo kimakundi, leo CHADEMA wanapita mle mle-kundi la Zitto na la Mbowe, kwa mfano, chama kitapasuka
  3. Kutopenda ushauri; kama ilivyokuwa kwa CCM, ukitaka vita na Chadema basi kosoa chama au kiongozi wa chama. Hivi chama hakifiki popote.

  Wito wangu kwa chadema, onyesheni tofauti yenu na CCM otherwise watanzania tutapoteza imani na vyama vya siasa!
   
 2. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #2
  Jul 25, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,629
  Likes Received: 9,842
  Trophy Points: 280
  huwezi ona tofauti kama umefumba macho,,,fumbua macho nyanyua kichwa utaona mbali zaidi ya urefu wa pua yako.......................
   
 3. Scofied

  Scofied JF-Expert Member

  #3
  Jul 25, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,025
  Likes Received: 199
  Trophy Points: 160
  Nna wasiwasi na uwezo wako wa kufikiri mkuu
   
 4. B

  Bubona JF-Expert Member

  #4
  Jul 25, 2012
  Joined: Aug 31, 2011
  Messages: 449
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Huwezi ona tofauti kwa sababu hutaki kuona; umefumba macho kwa nguvu ili usione.
  Tukusaidieje?!!
   
 5. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #5
  Jul 25, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Chadema hakuna makundi ila Zitto ndiye ambae anajaribu kutengeneza makundi ila bado hajafanikiwa na hatafanikiwa milele ! Chadema na CCM ni mbingu na ardhi haviwezi kulingana kamwe !
   
 6. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #6
  Jul 25, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Kama huoni tofauti wewe utakuwa kipofu na siyo kazi yetu kuponyesha vipofu
   
 7. proisra

  proisra JF-Expert Member

  #7
  Jul 25, 2012
  Joined: Jun 14, 2012
  Messages: 213
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  CCM wamekutuma, waambie wakamuulize wasira!!!!!!!!!
   
 8. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #8
  Jul 25, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145

  Kwani WAHINDI na WAARABU sio Wananchi wa Tanzania? Kwani wote wenye fedha ni MAFISADI?

  Mzee SABADO alianza biashara yake Tangu enzi ya Nyerere na Msafi CCM ingesha kata CHIA ZAKE ZA KIFISADI

  SIJUI KWAnini unaweka hoja kama hii haina miguu wala kichwa;

  CHADEMA ni bora kiwe chama cha watanzania wote kuliko kuchagua kuwa cha kipande fulani; Sasa Unawaita

  WAHINDI na WAARABU Mafisadi baadaye ni NANI? Acha UFINYU wa MAARIFA; HATUTAKI kwenda huko
   
 9. m

  majebere JF-Expert Member

  #9
  Jul 25, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,521
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  Umesema wanakumbatia wahindi na warabu halafu unataja majina ya wahindi na bulushi. Sasa hapo mwarabu ni nani? Kajipange wewe
   
 10. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #10
  Jul 25, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Baba v kapitaaa!!! pole kaka/dada
   
 11. m

  majebere JF-Expert Member

  #11
  Jul 25, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,521
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  Wanasiasa wote wanapigania matumbo yao, tofauti yao ni jina la chama tu.wote wanatafuta njia za kukuza vitambi.
   
 12. majuto mperungu

  majuto mperungu JF-Expert Member

  #12
  Jul 25, 2012
  Joined: Jul 20, 2012
  Messages: 394
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  uharo wa jana
   
 13. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #13
  Jul 25, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Nikusahihishe jambo moja hapa...

  Sabodo ni mtanzania kama waTZ wengine, huyu mzee amejaliwa kuwa na pesa kama watu wengine na ameamua kuisaidi Chadema na wananchi kwa njia ya kuchangia operations zinazofanywa na CDM kuwaelimisha umma wa watanzania...

  Na inawezekana huyu mzee ameona namna nzuri ya kuwasaidia waTZ ni kutoa misaada kupitia CDM hayo ni maamuzi yake, you can't question about that maana ni hiari.

  Kuhusu makundi najua chanzo cha kiburi cha Zito ni CCM na si kitu kingine, kama anavyojitamba kuwa anautaka Urais na kusema Rais lazima atoke kigoma, huu kwanza ni ubaguzi na nimewaona watu wengi wa kigonma na wao wanadai lazima Rais atoke kigoma kwa sababu gani?????

  Je rais akitoka kigoma ndiyo watu wa kigoma watakuwa ikulu???? au wanabaki kigoma na huu utata wa zito unatokana na CCM hasa JK na si mtu mwingine. Na wanaomfahamu zito tangu chuo watatueleza.

  Na mimi nafikiri ni muda mwafaka wa kujiuliza hivi Dr Walid Kabour yuko wapi???? maana mbwembwe zilikuwa kama hizi...
   
 14. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #14
  Jul 25, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,841
  Trophy Points: 280
  Kama huoni hatuwezi kuku lazimisha, kuna watu kama zitto ,,mna watumia ili kuleta makundi.

  Lakini kamwe zitto wenu hata tugawa na wala cdm hakuna makundi na vizuri mnafiki amejitaja mwenyewe.

  Yan ccm unataka kuifananisha na cdm lazima huwe kipofu.
   
 15. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #15
  Jul 25, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Nna hakika cha kwako siku hizi kitakuwa hakitizamiki manake unavyowateteaga mafisadi wa ccm humu ndani mpaka unatia huruma kama basi wanakulipa vizuri !
   
 16. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #16
  Jul 25, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Du! Yaani umekubali kutumiwa na magamba kama ile mipira ya zinaa
   
 17. j

  jigoku JF-Expert Member

  #17
  Jul 25, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Makundi hakuna japo mh Zitto na mwenzie Shibuda wanajaribu kuyaleta kwa back up ya CCM,hilo tunalijua fika,na hata mafisadi wanamtumia Zitto kuleta makundi ili wakidhoofishe chama,maana kujenga hoja sio tatizo ni kweli Zitto anaweza kujenga hoja laikini cha msingi matokeo ya hoja iliyojengwa yanawanufaisha vipi watanzania wanyonge na wapenda mageuzi?tunajua jinsi watu wanavyojiandaa kugombea uraisi huko ccm lakini walioenda mbali zaidi wanajaribu kuhusisha mbinu zao kwa kukidhoofisha CDM,lakini nedeleeni ku-warm up maana mechi bado.
  Kuhusu wahindi na warabu na mfano wako wa Sabodo,nadhani huishi TZ na wala hujui siasa za CCM,mwambie leo mzee Abdalah wa camel oil achangie shughuli za cdm,au mwambie oil com,au mwambie Kishimba wa Mwanza na wengine kam kina patel halafu utanipa jibu kama ni mafisadi au sio,kama wanafanya biashara zao halali au la.mzee sabodo biashara zake ni halali na wala sio fisadi,angesafilisiwa,ccm wakuache uchangie CDM.unacheza wewe.
  Kama tu kukodi ofisi za matawi wanatishwa wenye nyumba iweje kutoa fedha nyingi kama sabodo?
  CDM NI TOFAUTI NA CCM
   
 18. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #18
  Jul 25, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,696
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  1. CDM haijamkumbatia Sabodo, ila Sabodo ndio anaipenda CDM.

  2. Makundi mnayaona nyie CCM, huku hakuna makundi.

  3. Ushauri unapokelewa as long as uwe na maslahi kwa chama. Mambo ya ndoa ya Dr Slaa ukileta tunakuchana live.
   
 19. Josephine03

  Josephine03 JF-Expert Member

  #19
  Jul 25, 2012
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 752
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ndo maana tunashauri CCM itoke iingie CDM ili uone tofauti ya Kulwa na Doto ingawa wametoka tumbo moja, siku moja na kunyonya ziwa moja wakati moja, lakini kuna mnene na mwembamba, mfupi na mrefu. Nafikiri umenielewa na hoja yako mdebwedo

  Sent from my BlackBerry 9910 using JamiiForums
   
Loading...