Elections 2010 Kwa hili chadema hamtaeleweka

Kahema

JF-Expert Member
May 21, 2010
202
43
Kufuatia kauli aliyoitoa dr slaa kua hawatakubaliana na matokeo ya uraisi na ubunge kwa kile anachokidai kua kuna wizi wa waziwazi umefanyika. nategemea yafuatayo yafanyike kama kweli anataka sisi tuliompigia kura tujue kweli chadema ipo kwa ajiri ya watu na sio mtu binafsi.1; wabunge waliochaguliwa kupititia chama hicho wasikubali kuingia bungeni kwa kua zoezi zima halikua huru na haki. la sivyo tutajua kua kila mtu alikua anatafuta kula na sio kura,
2.kama alivyojibu jaji makame kua hajapata malalamiko yoyote toka kwa chadema tafadhali wafanye haraka kulifisha hilo wakiwa na vielelezo vya kutosha.
3. jammii za kimataifa zijulishwe upesi kilichotokea kwa vielelezo maana tayari wameshasema uchaguzi ulikua huru na haki.
4. wajitoe kwa hari na mali kupigania haki yao hiyo mpaka tone la mwisho la damu.
 
Heli mimi sijasema, ila mambo yako wazi wazi hayahitaji PHD kujua kama kura zimechakachuliwa au vipi, Mfano Segerea. ilifahamika toka mwanzo Chadema imeshinda. wameiba iba ndiyo wakatangaza. ama kweli hii ni Tanzania
 
hawana data umewauliza au unaandika kuonekana na wewe kuwa umetoa wazo lako.....kaa kimya!
 
Kufuatia kauli aliyoitoa dr slaa kua hawatakubaliana na matokeo ya uraisi na ubunge kwa kile anachokidai kua kuna wizi wa waziwazi umefanyika. nategemea yafuatayo yafanyike kama kweli anataka sisi tuliompigia kura tujue kweli chadema ipo kwa ajiri ya watu na sio mtu binafsi.1; wabunge waliochaguliwa kupititia chama hicho wasikubali kuingia bungeni kwa kua zoezi zima halikua huru na haki. la sivyo tutajua kua kila mtu alikua anatafuta kula na sio kura,
2.kama alivyojibu jaji makame kua hajapata malalamiko yoyote toka kwa chadema tafadhali wafanye haraka kulifisha hilo wakiwa na vielelezo vya kutosha.
3. jammii za kimataifa zijulishwe upesi kilichotokea kwa vielelezo maana tayari wameshasema uchaguzi ulikua huru na haki.
4. wajitoe kwa hari na mali kupigania haki yao hiyo mpaka tone la mwisho la damu.

Data zote feki hazija hakikiwa aiseeee na wanao hakiki kwa mujibu wa sheria ni NEC, hapo sasa !
 
Dr amesema uchaguzi wa uraisi urudiwe upya, na data za kutosha wanazo za jinsi gani waliiba kura
 
Na tume holela ijiuzuru. Hatutaki hawa wazee watuingize kwenye matatizo sababu ya madaraka. Wamepewa madaraka miaka mitano hawakujuwa kuwatumikia wananchi mwishowe wizi. Noma sanaaaa. Unatawala watu ambao hawakukuchagua. Hatari. No mafanikio.
 
data hizi hapa chache

Kwa mujibu wa Dk Slaa, ambaye pia ni katibu mkuu wa Chadema, chama chake kimekuwa kikifuatilia kwa makini matokeo hayo na kugundua wizi mkubwa wa kura kwenye nafasi za urais na ubunge.
Mgombea huyo wa urais, ambaye mara nyingi hujenga hoja kwa kutumia ushahidi, alisema moja ya maeneo waliyogundua kuwepo kwa wizi wa kura ni matokeo ya Jimbo la Geita lililo mkoani Mwanza ambako alidai Nec ilitangaza kuwa kwenye uchaguzi wa rais, CCM imepata kura 17,792 na Chadema kura 3,789.
Lakini akasema kwa mujibu wa fomu walizonazo ambazo zilisainiwa na mawakala wao kwenye kata 20 za jimbo hilo, CCM ilipata kura 30,960 na Chadema 15,736.
"Nashangaa Nec wanatangaza matokeo haya kutoka wapi? Hayo ya Geita ni moja tu. Kule Hai, fomu zinaonyesha kwenye urais CCM ina kura 20,120 na Chadema 26,724, lakini Nec imetangaza kuwa CCM ina kura 35,910 na Chadema kura 18,513," alisema Dk Slaa huku akionyesha baadhi ya fomu kwa waandishi wa habari.
Dk Slaa pia alitoa mfano aliodai kuwa wizi wa kura katika kituo namba 00070103 cha Ubungo jijini Dar es Salaam na kueleza kuwa fomu 24A inaonyesha CCM wamepata kura 68,727 na Chadema 65,450, lakini matokeo ya kata za Ubungo yanaonyesha CCM ina kura 70,472 na Chadema 72,252.
Dk Slaa alisema mbali na Ubungo, tatizo hilo pia alidai liko Kigoma Mjini ambako Chadema imeshinda kwa zaidi ya kura 500, lakini "matokeo yalichakachuliwa na kusababisha vurugu hadi askari wakawapiga mabomu wafuasi wa Chadema".
Pia alisema kwenye Jimbo la Segerea, ambako matokeo yalicheleweshwa kwa siku mbili na kutangazwa usiku wa manane juzi, mambo ni mabaya zaidi kwa kuwa fomu 21 A na B hazikuwepo na wasimamizi walikwenda nazo majumbani kulala.
"Kiwalani fomu hazikuwepo na matokeo hayakuonekana. Kipawa vituo vinne matokeo hayakuonekana na Vingunguti kuna vituo saba na Tabata vituo viwili ambako matokeo hayakuonekana," alisema Dk Slaa.
Aliongeza kusema: "Hali kama hiyo pia imetokea Morogoro Mjini. Matokeo hayajaonekana na yametangazwa tu. Kibakwe na Kiteto mgombea hakushirikishwa katika kutangaza matokeo.
"Hayo ni majimbo ya mifano tu. Yapo majimbo mengi na kutokana na hali hiyo, Chadema imetoa tahadhari kwa Tume na vyombo vya ulinzi na usalama kuwa taratibu hazijafuatwa na nyingi zimevunjwa."
Dk Slaa alisema kuwa ni muhimu waangalizi wote wa uchaguzi wakatoa taarifa zao hadharani ili kusaidia nchi na kumtaka mkuu wa Jeshi la Polisi kuendesha chombo hicho cha dola kwa haki na maadili waliyosaini.
Baadaye mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema kuwa kauli hiyo ya Dk Slaa ni tamko rasmi la Chadema.

Kutoka Mwananchi la leo
 
CCM na makuhadi wao very pointless ivi unadhani Slaa huwa anaraise hoja bila ushaidi
 
Kufuatia kauli aliyoitoa dr slaa kua hawatakubaliana na matokeo ya uraisi na ubunge kwa kile anachokidai kua kuna wizi wa waziwazi umefanyika. nategemea yafuatayo yafanyike kama kweli anataka sisi tuliompigia kura tujue kweli chadema ipo kwa ajiri ya watu na sio mtu binafsi.1; wabunge waliochaguliwa kupititia chama hicho wasikubali kuingia bungeni kwa kua zoezi zima halikua huru na haki. la sivyo tutajua kua kila mtu alikua anatafuta kula na sio kura,
2.kama alivyojibu jaji makame kua hajapata malalamiko yoyote toka kwa chadema tafadhali wafanye haraka kulifisha hilo wakiwa na vielelezo vya kutosha.
3. jammii za kimataifa zijulishwe upesi kilichotokea kwa vielelezo maana tayari wameshasema uchaguzi ulikua huru na haki.
4. wajitoe kwa hari na mali kupigania haki yao hiyo mpaka tone la mwisho la damu.

Kama umetumwa vile! ila una point kidogo.
Mbona unamsikiliza Makame zaidi kuliko kujua nini wandishi wa habari walionyeshwa? walionyeshwa barua mbili,moja inatoka kwa msimamizi wa uchaguzi jiji la MWANZA kwenda kwa wasimamizi wasaidizi ikiwa na mlengo wa kuchakachua...chadema wakamuandikia barua hajajibu mpaka jana,wewe unasema wapeleke malalamiko!!!yepi tena wakati wanayo bado kujibu tu!!!!
 
Ona unavyojichanganya .... ohhh nimempigia kura slaaa .... ohhh chadema siwajua na siwaelewi....ohhh chadema hamkubaliki....ohhh nina shida ya kuandika vizuri.

If you happy and you know it CRAP your hands ...... CRAP CRAP CRAP pwa pwa pwa
 
dotto njowepo big up..
wengine wote nmliochangia naona ni memba wapya hamjui mnachosema
 
data hizi hapa chache

Kwa mujibu wa Dk Slaa, ambaye pia ni katibu mkuu wa Chadema, chama chake kimekuwa kikifuatilia kwa makini matokeo hayo na kugundua wizi mkubwa wa kura kwenye nafasi za urais na ubunge.
Mgombea huyo wa urais, ambaye mara nyingi hujenga hoja kwa kutumia ushahidi, alisema moja ya maeneo waliyogundua kuwepo kwa wizi wa kura ni matokeo ya Jimbo la Geita lililo mkoani Mwanza ambako alidai Nec ilitangaza kuwa kwenye uchaguzi wa rais, CCM imepata kura 17,792 na Chadema kura 3,789.
Lakini akasema kwa mujibu wa fomu walizonazo ambazo zilisainiwa na mawakala wao kwenye kata 20 za jimbo hilo, CCM ilipata kura 30,960 na Chadema 15,736.
"Nashangaa Nec wanatangaza matokeo haya kutoka wapi? Hayo ya Geita ni moja tu. Kule Hai, fomu zinaonyesha kwenye urais CCM ina kura 20,120 na Chadema 26,724, lakini Nec imetangaza kuwa CCM ina kura 35,910 na Chadema kura 18,513," alisema Dk Slaa huku akionyesha baadhi ya fomu kwa waandishi wa habari.
Dk Slaa pia alitoa mfano aliodai kuwa wizi wa kura katika kituo namba 00070103 cha Ubungo jijini Dar es Salaam na kueleza kuwa fomu 24A inaonyesha CCM wamepata kura 68,727 na Chadema 65,450, lakini matokeo ya kata za Ubungo yanaonyesha CCM ina kura 70,472 na Chadema 72,252.
Dk Slaa alisema mbali na Ubungo, tatizo hilo pia alidai liko Kigoma Mjini ambako Chadema imeshinda kwa zaidi ya kura 500, lakini "matokeo yalichakachuliwa na kusababisha vurugu hadi askari wakawapiga mabomu wafuasi wa Chadema".
Pia alisema kwenye Jimbo la Segerea, ambako matokeo yalicheleweshwa kwa siku mbili na kutangazwa usiku wa manane juzi, mambo ni mabaya zaidi kwa kuwa fomu 21 A na B hazikuwepo na wasimamizi walikwenda nazo majumbani kulala.
"Kiwalani fomu hazikuwepo na matokeo hayakuonekana. Kipawa vituo vinne matokeo hayakuonekana na Vingunguti kuna vituo saba na Tabata vituo viwili ambako matokeo hayakuonekana," alisema Dk Slaa.
Aliongeza kusema: "Hali kama hiyo pia imetokea Morogoro Mjini. Matokeo hayajaonekana na yametangazwa tu. Kibakwe na Kiteto mgombea hakushirikishwa katika kutangaza matokeo.
"Hayo ni majimbo ya mifano tu. Yapo majimbo mengi na kutokana na hali hiyo, Chadema imetoa tahadhari kwa Tume na vyombo vya ulinzi na usalama kuwa taratibu hazijafuatwa na nyingi zimevunjwa."
Dk Slaa alisema kuwa ni muhimu waangalizi wote wa uchaguzi wakatoa taarifa zao hadharani ili kusaidia nchi na kumtaka mkuu wa Jeshi la Polisi kuendesha chombo hicho cha dola kwa haki na maadili waliyosaini.
Baadaye mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema kuwa kauli hiyo ya Dk Slaa ni tamko rasmi la Chadema.

Kutoka Mwananchi la leo

Azipeleke mahakamani zikathibitishwe, hatutaki RAW DATA hapa , please !
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom