Kwa hili CCM inataka kuficha ukweli kwa wanachi!! Kabisaaaa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa hili CCM inataka kuficha ukweli kwa wanachi!! Kabisaaaa!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by analysti, Sep 3, 2010.

 1. analysti

  analysti JF-Expert Member

  #1
  Sep 3, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 704
  Likes Received: 354
  Trophy Points: 80
  Nasikitishwa sana na kauli za viongozi wa CCM za kutaka vyama vya upinzani visizungumzie habari za ufisadi na matumizi mabaya ya uongozi vilivyokuwa vimetamalaki katika serikali iliyopita.

  Nashindwa kuelewa maana ya vyama vingi ni nini?, ninavyojua chama kinatakiwa kieleze wananchi bayana,ni kwa nini kichaguliwe chenyewe na si kingine, Pia kieleze ni kwanini wasikichague chama kilichokuwa madarakani na wakipe chenyewe madaraka. Katika kuelezea haya lazima kiseme ni wapi serikali iliyopita ilishindwa ambapo yenyewe itaparekebisha kwa maslahi ya wapiga kura. Hapa huwezi kuacha kuwaeleza wananchi kuwa serikali iliyopo madarakani ilishindwa kusimamia kodi zao na kwa makusudi iliziacha zichukuliwe na mafisadi, na mambo kama hayo.

  Nijambo la ajabu sana viongozi hawa kukataza wapinzani wasizungumzie haya na waongelee sera tu. Tatizo siyo Sera peke yake tatizo ni uadilifu ndani ya serikali. Hatutaki kuchagua mtu kwa misingi ya sera peke yake, lazima uadilifu wa huyu mtu uzingatiwe pia.Si kweli kuwa sera zote za CCM ni mbovu, tatizo kubwa la CCM ni kiwango cha uadilifu wa viongozi kimeporomoka mpaka sifuri. Hata ukishusha sera kutoka mbinguni, kwa uadilifu uliomo ndani ya CCM hakuna chochote cha maana kitakachofanyika, CCM imekuwa chama cha wafanya biashara na wenye pesa kwa maslahi ya wenye pesa!! Hilo linafahamika na watanzania wote wakiwamo wana CCM wenyewe pamoja na Mzindakaya(rejea speech yake ya kuliaga Bunge 2010). Mambo haya yote ndo yanayofanya vyama shindani viombe kuchaguliwa badala ya CCM, sasa kuwaambia wasiongelee haya, ni sawa na kusema hivyo vyama havina kitu mbadala cha kujitofautisha na CCM.

  kama CCM hawataki kukosolewa basi watangaze kuondolewa kwa mfumo wa vyama vingi na kubadili katiba. Hivi Hawa CCM wanafikiri watanzania sisi ni wajinga kiasi gani?
   
 2. M

  Msharika JF-Expert Member

  #2
  Sep 3, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  mzee madaraka matamu, lazima wafiche uozo wao waonekane wema, ila 2010 hatudanganyiki
   
Loading...