Kwa hili bora waniue tu. Sio Makamba wala Rais nina imani nao kuhusu mradi wa Rufiji. Tumepigwa

Bei ya Gas na mafuta mpaka dhahabu haipangwi na mtu ni soko la dunia demand and supply hata mazao yetu tunalima wenyewe lakini soko linaamuwa bei sio serikali wala mtu mmoja. Gas inauzwa nje ndio kwenye dollar sasa wauze Tsh kwani ulisikia nyanya zile.
Kwa hiyo bei ya mafuta wanayo nunua wa Saudi Arabia na sisi huku ni sawa?
 
Price is determined when Demand = Supply ila kuna gvt measures za kureduce inflation kama wewe umesoma vzr uchumi. Haiwezekani Gas inachimbwa kwako lazma uangalia fair kwa wananchi wako na sio unakwenda kutoza viwandani tena kwenye bidhaa muhimu una expect nn?. Tunafaham bei zinapanda kwasabu serikali inachukua tozo viwandani pia tushajua tayri mchawi ni nani ni serikali.

Mkuu kama wewe una maisha mazuri una afford basic needs mshukuru sana Mungu, kuna watanzania wana maisha magumu sana natembea kona zote za Tz hali ni mbaya sana kama wewe mjin unanunua mafuta ya kura kwa 8,000 wa kule ndani kabisa bush atanunua kwa sh ngapi?

Hapa tunajadili maslah ya Taifa kwa ujumla tuweke utim pembeni.
Inflation ni somo kubwa sana na sio kila infalation ni mbaya inflation ina maana mbili labda bidhaa zimekuwa chache wanunuzi wengi dawa kuongeza uzalishaji kuna inflation kodi za zimeongezwa bei juu ila vipato viko palepale hili ni somo kubwa sana na hapa unaweza kujaza page ila sio kila inflation ni negative inahitaji kuwa control. nirudi kwenye Gas, gharama za uchimbaji ni kubwa sana haijalishi unachimba kwako au kwa jirani gharama za usafirishaji ni ndogo sana katika cost za product, nchi chache sana duniani ukiona bei ya mafuta au gas iko chini ni kuna ruzuku inatolewa lakini sio bei halisi ila huko sisi hatuwezi kurudi wala hatuna uwezo. Kusema kuwa sababu Gas ya kwetu ndio iwe bei rahisi ni kama kutaka kuniambia kuwa kwa sababu dhahabu ya kwetu basi ni bei rahisi. kumbuka anayechimba haya sio serikali ni mwekezaji gharama hazibadiliki ni soko linaamua ikitokea siku Gas ikawa subsidized basi nakuhakikishia utaona watu wanavusha nchi jirani kwa kununua rahisi iliyopewa ruzuku kupiga pesa. Mafuta ya kula yamepanda duniani kote na ziko sababu sio Tanzania tu mbadala si kuna mafuta ya alizeti ya nchini yanauzwa vipi huko? nyama zimepanda bei kwanini? sababu mahitaji makubwa kuliko supply mbona huko hatuongelei na kusema ng'ombe zetu vipi bei zipande? vitunguu bei juu kwanini? demand and supply kama ni inflation positive kwa maana watu wanapesa siku hizi walaji nyama ni wengi basi ni wajibu muuza nyama kuongeza nyama kama ni issue hakuna mifugo michache wanunuzi wengi ng'mbe wachache hii ni issue tofauti. Serikali inachoweza kupunguza kodi zake tu ila hili nalo lina madhara yake mapato kupungua na uwezo wa serikali kupungua. Mambo ya ruzuku hakuna tena huko tumeshapita.
 
Wewe nishakuona fala, ukitoka hapo kwa shemej yako utajua tunaongela suala gani. Hayo yote unayoongea yanajulikana. Hivi unajua kwenye gas hatuna chetu pale? Mtu anapewa fungu anasain mikataba ya hovyo, fu***
Ukiona mtu anaanza matusi ujuwe hoja hana mimi nakupa hoja kama shemeji yangu hajalalamika tatizo lako nini? si shemeji yangu. weka hayo mambo tuliyopigwa sio kukariri tu nenda kuna kitu kinaitwa PSA somo kubwa mikataba ya hovyo weka hapa walichotia sign cha hovyo na kipi kingefanyika sio kukariri tu bila kuwa na ushahidi. mikataba inaandaliwa na wana sheria sio waziri inapitia process kama mikataba mibovu then una watumishi wabovu ziko njia za kuwajibisha kubwa acha kuchagua viongozi wabovu sio kulalama kesho ndio wa kwanza kuvaa kofia za kijani au red.
 
Ukweli uko hivi, wale waliotufisadi gesi yetu kwa mikataba ya kijinga ya enzi za fisadi Kikwete ndio wanafanya kila linalowezekana ili mradi usikamilike kwa kuwa hiyo ni heri kwao kwa kuendelea kutuuzia gesi yao ya bei ya juu tuzalishie umeme.

Mradi wa JNHPP ukikamilika maana yake ni kwamba tutajitosheleza kwa mahitaji ya umeme na kupata ziada ya kuuza nje, bila kuwategemea hao wanyonyaji wanaotuuzia gesi.

Kwa hiyo ni lazima wafanye juu chini ili mradi usikamilike ili waendelee kutupiga. Sina uhakika sana kama Kikwete hana share kwenye hayo makampuni ya gesi.

Inabidi tufike mahali tuchague aidha kuendelea kuwa na Kikwete/ makamba & co, au tuwafyeke watuachie mradi wetu!
Kuwafyeka msoga gang anza na chief.
 
Kwa hiyo bei ya mafuta wanayo nunua wa Saudi Arabia na sisi huku ni sawa?
Saudi arabia wanatoa ruzuku kwenye refine product kwa maana wanalipia tofauti ya bei halisi ila nchi kama UAE wanaondoa ruzuku bei zimepanda hata Saudia wameondoa kiasi fulani cha ruzuku mafuta yamepanda kidogo japo bado bei ya chini sana sababu wanatoa ruzuku kwa maana serikali inalipia difference, sasa kwanini wao wanafanya hivyo? sababu kwanza uwezo wanao wa pesa wala hawaendi kukopa IMF huko kwa sisi huwezi kwenda kuomba mikopo hawakupi wakijuwa unatumia pesa kutoa ruzuku hupewi utaambiwa ondoa ruzuku kusanya kodi sawasawa ndio uje kuomba mikopo. Umewahi kusikia wanaenda IMF au banki ya dunia kuomba pesa? Leo serikali ikiamua kuondoa pesa wanazotoa katika kugharamikia elimu unadhani shule gharama zitakuwaje? kuna mtu atachangia tu gharama awe mzazi au serikali au wote.
 
Sina imani na Makamba na Rais Samia kuhusu mradi wa bwawa la Nyerere, huenda Makamba anatumiwa na nchi za kigeni.

Hivi huu mgao wa umeme mnaounaje? Kiukweli maswali ni mengi mno, wanasema wanarekebisha ili tuhamie kwenye umeme wa gesi, ukiwauliza kwa gesi ipi wakati gesi ina mwenyewe?

Utaratibu uliopo ni kuwa serikali kupitia Tanesco itanunua gesi kutoka kwa mwekezaji pale mtwara wakishanunua ndo nao wazalishie umeme na watuuzie.

Zamani nilifikirigi ni serikali inachukua tu gesi yake inazalisha umeme kumbe sio kweli kumbe tunaenda kununua gesi kutoka kwa hao wawekezaji wenye vitalu then wanatuuzia na sisi ndo tunaipeleka Tanesco wanazalisha umeme nao wanauuza kwa wananchi.

JPM baada ya kuingia madarakani na kugundua gesi ilishachukuliwa na mikataba ishasainiwa huwezi kuivunja, ilibidi kinyonge akubali tu kuwa tushapigiwa.

Unaambiwa hakuna mkataba ulimuumaga Magufuli kama mkataba wa gesi wa Mtwara, mzee wa watu akaona isiwe kesi akaona wacha apambane ajenge mradi wa Steglaz wa bwawa la Nyerere tupate megawatt 2200 kwa wakati mmoja.

Umeme ambao ni mwingi kwani hata mamitambo yote ya gesi yaliyoko nchi hii uyaunganishe yote hayawezi toa megawat 300 lakini maporomoko ya Rufiji Nyerere Dam pekee yatatoa megawatt 2200 kwa wakati mmoja huu ni umeme mwingi tutauza nchi zaidi ya 5 nje!

Lakini cha ajabu sasahivi wameachana na huu mradi ghafla wamerukia kwenye umeme wa gesi.

Wamerukia kwenye umeme wa gesi ambao ni ghali na gharama kubwa kwa faida ya nani? Ni nani anafaidika na hiyo mikataba ya gesi? Ninani yupo nyuma ya hili?

Kwanini wameacha umeme nafuu wa bwawa la Nyerere na umeme wa uhakika na bei rahisi na kurukia umeme wa gesi ambao ni ghali na ni gesi ya kununua kwa mwekezaji?

Nani atafaidika tukianza kununua gesi kwa mwekezaji halafu wanatupangia bei halafu na tanesco watuuzie hawaoni ni biashara kichaa ya hasara watakaofaidika ni wawekezaji wanaotuuzia gesi yetu wenyewe?

Muulizeni Makamba iko wapi output ya mradi wa gesi wa Kinyerezi? maana nasikia megawatts zilizotarajiwa zingepatkana hazijafikia hata nusu?

Hivi mnajua mradi wa bomba la gesi Mtwara inasemekana serikali ya Jk ilikopa? Mradi wa gesi wa Kinyerezi wa gesi pia walikopa sasa chukua hyo mikopo yote jumlisha na bado hiyo gesi watauziwa na mwekezaji maana gesi siyo yetu tena bado watapangiwa bei ya kutuuzia umeme hao tanesco sasa kwa haya yote mnadhani tutafaidika nini kama nchi?

Hivi wanadhani mwendazake alikua hana akili alivyoachana na haya mauzauza ya gesi? Hivi hawa jamaa wanatuonaje?

Makamba aliingia mkataba na kampuni ya kihindi kutoka India kwa ajili ya kukodi app (application software) ya kutumika Tanesco eti hiyo software alikodi kwa bilioni 70 jamani hii nchi daaah, bilioni 70 ukodi software? Uwiiii hivi kuhama bongo unabonyeza ngapi?

Ilitakiwa ikifika November 2021 bwawa la Nyerere liwe limeshajazwa maji tayari kwa kuanza kazi, lakini cha ajabu Mama akamtoa Waziri Kalemani mchapakazi na akamuweka Makamba!

Hadi leo Kalemani katolewa bila kufanya kosa lolote lile. Halafu Makamba anaulizwa bungeni kwanini maji hayajajazwa hadi leo anatoa sababu ambazo hazieleweki, mara ooh et winchi ya kuchimbia moja haipo eti hadi iagizwe nje! Mara shimo lilikosewa kuchimbwa! Huu mradi nahisi unacheleweshwa tu, na nchi za magharibi wanaupiga vita huu mradi kwasababu.

Wanaupigavita huu mradi maana wanajua mkishakua na huu mradi tatizo la umeme litabaki historia nchini, na watapoteza soko la kuuza solar, majenereta, mafuta na maumeme yao ya ghali nchini.

Huu mradi unapigwa vita balaa kila rais alotaka kujenga huu mradi alizuiwa na kupigwa biti na wazungu na mabepari wa dunia hii kuanzia Nyerere, Mwinyi, Mkapa, JK

Wote walitaka jenga ila mabeberu wakawapiga biti wasijaribu JPM ndio mwanaume pekee alosema liwalo na liwe na siogopi, Uwiii sina imani na Makamba juu ya huu mradi. Sidhani kama ana nia ya huu mradi uishe hata maza simuamini ktka hili.

Jamani leo kwa mara ya 1 nasema simwamini mtu yeyote juu ya huu mradi sina imani kabisa na yoyote yule.

Bimkubwa kwanini alimtoa Kalemani? Unajua nyie watu mimi sielewi mjue! simwamini Makamba toka aingie ni migao tu ya umeme na umeme kukatika ovyo.

Sasa nitaamini vipi kwamba ana nia ya dhati ktk kukamilisha miradi ya mwendazake ambayo alijitoa sadaka liwalo na liwe ili huo mradi ujengwe?

Kwa hili na waniue kabisa lakini hivi vitu vinakera kabisa!!!
We endelea kufikirigi....😁😁
 
Saudi arabia wanatoa ruzuku kwenye refine product kwa maana wanalipia tofauti ya bei halisi ila nchi kama UAE wanaondoa ruzuku bei zimepanda hata Saudia wameondoa kiasi fulani cha ruzuku mafuta yamepanda kidogo japo bado bei ya chini sana sababu wanatoa ruzuku kwa maana serikali inalipia difference, sasa kwanini wao wanafanya hivyo? sababu kwanza uwezo wanao wa pesa wala hawaendi kukopa IMF huko kwa sisi huwezi kwenda kuomba mikopo hawakupi wakijuwa unatumia pesa kutoa ruzuku hupewi utaambiwa ondoa ruzuku kusanya kodi sawasawa ndio uje kuomba mikopo. Umewahi kusikia wanaenda IMF au banki ya dunia kuomba pesa? Leo serikali ikiamua kuondoa pesa wanazotoa katika kugharamikia elimu unadhani shule gharama zitakuwaje? kuna mtu atachangia tu gharama awe mzazi au serikali au wote.
Ngojera nyingi, ww unasema bei inapangwa na soko la dunia, nimekuuliza bei ya mafuta anayo nunua Msaudi kwa lita na sisi huku ni sawa?
 
Makimuda hujui kama hujui chochote kuhusu umeme na mikataba zaidi ya kwamba wewe ni mhanga wa uwongo wa Magufuli. Na nyinyi wajinga ndiyo mlikuwa mtaji wa Magufuli kwa miaka 5.

JNHPP was wastage of money. Hilo dude litabakia white elephant. Litajengwa ila halitakuja kuzalisha hizo megawati 2,100 za umeme.

Kwa maamuzi ya Dikteta mmoja mkemia asiyeamini sayansi, tumeharibu baioanuai ya selous na kukata miti yenye saizi ya ukubwa wa Mkoa wa Dar es Salaam. Hili litatugharimu milele.

Ni wakati wa kufanya maamuzi magumu kwa kusitisha kuendelea kujenga na kuendelea na umeme wa gesi. Kwa sasa Kinyerezi 1 & 2 zinachangia 60% ya umeme tunaotumia Tanzania. Na zinatumia hardly 10% ya gesi ya Mtwara

Miradi yote ya maji yaani Kidatu, Mtera, Kihansi, Nyumba ya Mungu, Hale, Pangani nk inachangia 40%. Numbers don't lie. Umeme wa kutegemea mvua siyo reliable na vile vile una athari kwa mazingira.

Kama Magufuli asingetokea mwaka 2015 tungepiga hatua kubwa sana kiuchumi kwa kuwa;
1. Kinyerezi 3 & 4 zingekamilika na kuwa chanzo kikuu cha nishati.

2. Tusingevuruga baioanuai ya Selous kwa kukata miti ili tujenge bwawa la umeme kwa ajili ya kupata Megawati 2,100 tu ambazo zinapatikana kwa kutumia 25% tu ya gesi ya Mtwara.
Your not serious
 
Ngojera nyingi, ww unasema bei inapangwa na soko la dunia, nimekuuliza bei ya mafuta anayo nunua Msaudi kwa lita na sisi huku ni sawa?
Hivi wewe unasoma nimekwambia Saudia wanalipia mafuta wao kama ruzuku kupunguza gharama za wananchi wao wewe una uwezo wa kulipia ruzuku? serikali yako inaweza? Saudia hawachukui kodi kwenye mafuta bure na bado tofauti wanalipia. Nchi ina reserve 700 billion $ hawakopi unataka kujifananisha na wewe unayekopa hata kujenga choo cha shule. acha ujinga kujifananisha na wale. Unajuwa UAE wananunua bei gani liter? ni kama 1700 Tsh no tax zero wewe unataka kununua kama wao wakati kuna tax unalipa. jifananishe na Kenya, Uganda na Zambia huko sio na Saudia
 
Ngojera nyingi, ww unasema bei inapangwa na soko la dunia, nimekuuliza bei ya mafuta anayo nunua Msaudi kwa lita na sisi huku ni sawa?
Nadhani ujuwe kuna crude hiyo inapangwa na soko la dunia refine product ni jambo lingine wewe huna hata refinery Tanzania unataka kununua Diesel bei rahisi. wale wana refinery wakipeleka ku refine crude yao ili wauze product hawachukui faida wanatoa barrel kwa barrel na proccesing cost serikali inabeba. ndio ruzuku yao hiyo wewe ulisikia Saudia anaagiza Gasoline au Diesel toka nje? wana refine wenyewe kwa crude yao wenyewe. unataka wewe uwe kama wao jenga refinery, chimba mafuta ya refine uza kwa bei ya bure. mahindi na mahindi ya kusagwa bei moja? kuna gharama za kusaga unalipia mtumiaji
 
Nadhani ujuwe kuna crude hiyo inapangwa na soko la dunia refine product ni jambo lingine wewe huna hata refinery Tanzania unataka kununua Diesel bei rahisi. wale wana refinery wakipeleka ku refine crude yao ili wauze product hawachukui faida wanatoa barrel kwa barrel na proccesing cost serikali inabeba. ndio ruzuku yao hiyo wewe ulisikia Saudia anaagiza Gasoline au Diesel toka nje? wana refine wenyewe kwa crude yao wenyewe. unataka wewe uwe kama wao jenga refinery, chimba mafuta ya refine uza kwa bei ya bure. mahindi na mahindi ya kusagwa bei moja? kuna gharama za kusaga unalipia mtumiaji
Screenshot_20220218-094109_Chrome.jpg


Tuachane na mafuta vipi kuhusu ndizi zetu, unataka kuniambia bei ya ndizi tuanazo nunua hapa ndani zinapangwa na soko la dunia?

Huwezi niambia eti kwa Saudi mafuta yao then,soko la dunia liwa amulie bei kwa matumizi yao ya ndani. Nijiavyo mimi kitu ukikizalisha ww na ukikiuza kwa watu wako wa ndani lazima kiwe cheap.
 
Hivi makabira ambayo yanaishi kweny msitu wa amazon hko brasil wanawezaje kuishi pasipo TV radio au ata hizo cm
 
View attachment 2122649

Tuachane na mafuta vipi kuhusu ndizi zetu, unataka kuniambia bei ya ndizi tuanazo nunua hapa ndani zinapangwa na soko la dunia?

Huwezi niambia eti kwa Saudi mafuta yao then,soko la dunia liwa amulie bei kwa matumizi yao ya ndani. Nijiavyo mimi kitu ukikizalisha ww na ukikiuza kwa watu wako wa ndani lazima kiwe cheap.
Nimefurahi unataka kujuwa hapo tutaenda vizuri. Mafuta wateja wako duniani kote na kumbuka mafuta ya Saudia ndio lakini wao soko lao kubwa ni nje sio ndani ndio maana wanatoa kiasi kidogo wanafanya refine wanauza bila faida ila mafuta yanaenda nje wanunuzi wako nje. Kuna brent na WTI hizi ni benchmark bei elekezi. mafuta yako yakiwa na kiwango cha brent unauza bei juu ila unaweza kuwa na mafuta lakini sio ubora wa brent ukauza bei chini. Sasa turudi mifano mepesi tu ndizi, ndizi zikiwa nyingi sokoni bei automatic zinashuka lakini ikitokea siku ndizi zimeadimika sokoni kwa sababu yoyote ile bei zitapanda na tuongelee mahindi kwa mfano wakivuna mengi yakijaa sokoni bei chini na tunalima wenyewe siku yakipungua tu bei taratibu zinapanda hapa hakuna bei elekezi ni wale madalali wa sokoni wanajuwa mahindi macheche mahitaji makubwa ndio wanapanga bei kutokana na hali ya sokoni. Tukija kwenye crude soko la dunia huko mfano New york wako pia madalali ndio kazi yao wanatizama manunuzi kwa siku na supply wakiona haviendani bei zinapanda au kushuka hii sio science. Ndio maana siku za sikukuuu ma bus yanapandisha nauli kwa sababu mahitaji makubwa wakati huo siku wateja wakipungua hata bei nusu wanakubeba japo gharama za uendeshashi ni zilezile. mifano mingi ndio tunarudi demand na supply. OPEC hawa wakiona bei inashuka sana wanachofanya kupunguza uzalishaji bei ipande na wakiona inapanda sana wanaongeza uzalishaji.
 
View attachment 2122649

Tuachane na mafuta vipi kuhusu ndizi zetu, unataka kuniambia bei ya ndizi tuanazo nunua hapa ndani zinapangwa na soko la dunia?

Huwezi niambia eti kwa Saudi mafuta yao then,soko la dunia liwa amulie bei kwa matumizi yao ya ndani. Nijiavyo mimi kitu ukikizalisha ww na ukikiuza kwa watu wako wa ndani lazima kiwe cheap.
Katika kujibu swali la ndizi hili linaamuliwa na soko la ndani sababu wewe unauza mfano Kariakoo mzigo unashushwa mahitaji yakiwa makubwa kuliko magari yanayoleta ndizi bei inapanda lakini kwa kuwa ndizi huwa supply iko steady utaona bei zake ziko steady lakini nenda kwenye mananasi yakijaa unauziwa kwa mafungu yakipungua na bei tofauti ila ikitokea leo kuna soko kubwa la mananasi Kenya utaona supply inapungua watauza Kenya wakiona kuwa bei ya Kenya iko juu sasa ili umvute mtu alete Kariakoo akijuwa tu atauza na kupata kama bei ya Kenya hapo sasa soko linaamuliwa na Kenya na Tanzania. Kuna wakati serikali ilizuia kuuza mahindi nje kwa sababu wakulima wanaona soko la ndani bei ndogo supply kubwa Kenya wanahitaji na bei juu wakazuiwa ile sasa kuwaumiza wakulima mwisho wa siku wameruhusu ili kuwe na ushindani wa supply and demand bei itajiamulia yenyewe.
 
Back
Top Bottom