KWA HILI BENCHI LA UFUNDI TAIFA STARS MMEWAKOSEA WATANZANIA.

Jj football

New Member
Mar 8, 2018
4
8
Imekuwa Kasumba kwa makocha wa taifa stars kuchagua wachezaji wa timu ya Taifa kwa mazoea, hali hii inapunguza uzalendo wa kushabikia timu yetu ya taifa. Kila siku wadau wanajitokeza kuwapa ushauri ni jinsi gani tunaweza kuifikisha Taifa stars sehemu nzuri lakini ushauri wao haufanyiwi kazi.

Hivi unawezaje kumwacha mchezaji kama Rashid Mandawa kwenye timu ya taifa? Juzi tu kawafunga Township Rollers wapinzani wa Yanga magoli matatu pekee yake sio hivyo tu bado ameendelea kufanya vizuri ligi kuu ya Botswana hadi sasa amefunga zaidi ya magoli kumi na moja na anazidi kuipeperusha Bendera ya Tanzania vizuri nchini Botswana.

Wachezaji wengi wa Tanzania wanapotoka njee ya Tanzania wanakosa nafasi tena ya kuitwa timu ya taifa mfano Deogratius Munish na bado ana kipaji kikubwa na uzoefu wa mechi za kimataifa.

Ni vyema sasa benchi la ufundi la timu ya Taifa lifanyiwe maboresho kwa kuongeza watu wa kuscout wachezaji wetu wanaocheza njee ya nchi na kutafuta takwimu zao ili soka letu lipige hatua.

Naijeria kila mwaka wanaandaa mechi za ushindani kwa vijana wao waliopo njee ya nchi na cream wanayoipata wanaishindanisha na wachezaji wao wa ndani ndio maana kila siku wanafanya vizuri kuanzia timu za vijana hadi timu ya taifa.

Tuna wachezaji zaidi ya ishirini ambao umri wao ni chini ya miaka 21 ambao wapo njee ya nchi kwenye academies kubwa kama Aspire, Reading , lassenCcSoccer,Vancouver whitecaps, Sc Heerenveen na Roda Jc,Fc chiasso etc.

Narudia hii cream ya hawa wachezaji ingechanganywa na Serengeti boyz wa Gabon hakika tanzania baada ya miaka kadhaa tungefika mbali sana.
IMG_20180308_122102_800.jpg
 
Waliostahili kuitwa ni wengi mfano,Uhuru Suleiman mambugu,Ibrahim ahmada,habibu kiyombo,ditram nchimbi n.k ,lakini kaitwa kichuya mkimbia uwanjan
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom