Kwa hiki walichofanya CCM Iringa siku ya jana ni udhalilishaji,na ni aibu kwa chama kikubwa kama CCM

Elice Elly

JF-Expert Member
Dec 9, 2018
1,235
2,000
Jana Jumapili Chama cha Mapinduzi walikuwa na mkutano katika eneo la Stand ya Mlandege.

Katika mkutano ule alikuwepo pia Humphrey Polepole,Mbunge wa viti Maalum wa CCM ambaye jina lake sikulisikia vizuri,madiwani wa CCM, na baadhi ya VIONGOZI wa CCM.

Mimi pamoja na Baadhi ya vijana Tulikuwa eneo la Shule ya Msingi Mlandege tukiwa tunawasubiri wenzetu ili tukafanye mazoezi katika uwanja wa mpira wa Shule ya msingi Mlandege, ghafla walitokea vijana wawili wakatuuliza nyinyi hamuendi kusikiliza mkutano?

Tukawaambia sisi tunawasubiri wenzetu tunaenda kufanya mazoezi, wakatuambia kama hamuendi mkutanoni basi ondokeni katika eneo hili.

Tuliwajibu kwa ustaarabu kuwa sisi tupo katika eneo hili la Shule tunaenda kufanya mazoezi. Ghafla tukasikia mawe yameanza kurushwa kuelekea tuliko,mengine yalitupata na mengine yalitua kwenye paa la Shule.

Kumbe wale vijana walikuwa ni kundi Kubwa na wengine walikuwa ndani ya Noah.Hata tulipoamua kuondoka waliendelea kuwazonga baadhi yetu na binti mmoja walimvua mpaka mtandio wake,na Baadaye waliendelea kumnyanyasa mpaka alipopata msaada toka kwa wananchi wema.

Tukio lile limenifanya nikose usingizi,natafakari na kujiuliza ina Mikutano yetu ya siasa tumefikia hatua ya kulazimisha watu wahudhurie?

Je, watu wanaofanya shughuli zao jirani na eneo la mikutano ya vyama wanalazimika kuacha shughuli zao kwenda kwenye mikutano?

Kama Leo wanatumia nguvu kulazimisha watu waende mikutanoni mwakani itakuwaje?

Lakini swali jingine ni kwamba nani aliwatuma wale vijana wadogo kuja kutufanyia vurugu watu ambao tulikuwa kwenye majukumu yetu? Wale vijana wamefundishwa na Nani kuyatenda Yale waliyotenda?

Kama Leo katika umri ule wanatumika kuwafanyia watu vurugu,wakisha kuwa watu wazima watatumia tena mawe au watafanya makubwa zaidi?

Kwa kweli tunahitaji Neema ya Mungu vinginevyo tunatengeneza makundi hatari sana katika nchi yetu.
 

omutimbasafi

JF-Expert Member
Oct 17, 2017
578
1,000
Na bado 2020 mje mzungushe mikono kama 2015,si mliona juzi mbeya yule aliyepandikizwa kuzungusha mikono kule mbeya.
 

Kifaurongo

JF-Expert Member
Jan 18, 2010
3,638
2,000
Visingizio vingine ni vya kuwaambia watoto wadogo. Ati mnawasubiri wenzenu kwenda mazoezini, yaani hao wanaosubiriwa hawaujui uwanja wa shule ya msingi uliopo mita chache toka ilipo stand?

Ningekuelewa ungalidai ni haki yako kikatiba kuwapo sehemu yoyote na kukutana na mtu yeyote mradi huvunji sheria za nchi.

Inaelekea mlikuwapo eneo hilo kimkakati, mmzomee polepole wenzenu wakatumia ulinzi shirikishi kuwatimua
 

tozi25

JF-Expert Member
Aug 29, 2015
5,840
2,000
Kawaulize walimu wa shule wanavyo zalimishwa kwenda mikutanoni na kuchangia mwenge. Ndio utajua ccm nuksi


Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 

Elice Elly

JF-Expert Member
Dec 9, 2018
1,235
2,000
Visingizio vingine ni vya kuwaambia watoto wadogo. Ati mnawasubiri wenzenu kwenda mazoezini, yaani hao wanaosubiriwa hawaujui uwanja wa shule ya msingi uliopo mita chache toka ilipo stand? Ningekuelewa ungalidai ni haki yako kikatiba kuwapo sehemu yoyote na kukutana na mtu yeyote mradi huvunji sheria za nchi. Inaelekea mlikuwapo eneo hilo kimkakati, mmzomee polepole wenzenu wakatumia ulinzi shirikishi kuwatimua
Una haki ya kuandika uliyoandika.Ila ushauri Wangu kwa mtindo waliofanya Jana wataingiza nchi kwenye machafuko bila sababu za msingi.Nilichoandika ndicho namaanisha,Mimi siyo mwanasiasa,ila kwa mtinso ule hakuna atakayeipenda CCM kwa kutumia mabavu
 

Capt Tamar

JF-Expert Member
Dec 15, 2011
9,957
2,000
cha utoto ,hapo chama unakihusishaje na uhuni wa wahuni wenzio
Hapa kwenye hoja yako ndiyo kuna utoto mwingi zaidi! Yaani hujui kuwa ccm ina makundi ya vijana ambao wanalipwa kwa kufanya vurugu kama hizo kwa maslahi ya chama?hebu msikilize huyu halafu utuambie kama chama hakihusiki!
 

Ngushi

JF-Expert Member
Jul 8, 2016
9,097
2,000
Atakuwa Rita kabati huyo! Huyu mama huwa anahangaika kweli kutaka kulichukua jimbo la iringa mjini ila anashindwa
 

Emmanuel Robinson

Verified Member
May 29, 2013
1,164
2,000
Hapa kwenye hoja yako ndiyo kuna utoto mwingi zaidi! Yaani hujui kuwa ccm ina makundi ya vijana ambao wanalipwa kwa kufanya vurugu kama hizo kwa maslahi ya chama?hebu msikilize huyu halafu utuambie kama chama hakihusiki!
View attachment 1123480
Hapa kiongozi ambaye ni mwenyekiti wa ulinzi na usalama amekosea. Huwezi kuwaruhusu watu kuvunja sheria.
 

Elice Elly

JF-Expert Member
Dec 9, 2018
1,235
2,000
Ulishindwa kuchukua hata Picha
Kwa kweli nilijaribu kupiga picha Lakini mawe yalizidi nikaona jambo la muhimu ni kujiokoa kwanza. Hata pale walipoona jitihada za zangu za kutaka kupiga picha kundi likaongezeka nikakimbilia kwenye ya MTU mmoja ndo aliye saidia kuniokoa
 

Timiza

JF-Expert Member
Nov 29, 2017
5,145
2,000
Kwa kweli nilijaribu kupiga picha Lakini mawe yalizidi nikaona jambo la muhimu ni kujiokoa kwanza. Hata pale walipoona jitihada za zangu za kutaka kupiga picha kundi likaongezeka nikakimbilia kwenye ya MTU mmoja ndo aliye saidia kuniokoa
Due wamefikia hapo INA maana Siasa za ushawishi awaziwezi tena?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom