Kwa hiki nilichokishuhudia leo, wenye magari hawatokuja kuwapenda waendesha pikipiki maarufu kama “bodaboda”

fizo talent

JF-Expert Member
Oct 17, 2017
2,257
3,882
Habari za weekend wakuu,

Nielekee kwenye mada moja kwa moja, leo nikiwa katika usafiri wa umma maarufu kama daladala inayofanya safari zake Chanika to Machinga Complex nilishuhudia tukio ambalo gari aina Harrier ikiwa barabarani katika eneo ambalo barabara ni mbovu, hivyo alilazimika kusubiri gari inayotoka mjini ipite ili na yeye aweze kupita.

Kilichotokea akiwa hana hili wala lile dereva bodaboda akiwa amepakia vijana wenzie wawili maarufu kama mshkaki walikuja wakaigonga ile gari kwa nyuma na taa ya nyuma ya gari kupasuka pale pale na hapo ilikuwa ni eneo la stendi kuna boda boda nyingine zimepaki pembeni japo kwa haraka haraka inaonekana yule aliyegonga ile gari hapaki katika kituo kile.

Baada ya tukio, maana dereva na abiria wake wote walianguka na kosa alilofanya dereva wa ile gari ajali ilivyotokea hakutoka pale pale katika gari yake, basi dereva wa ile pikipiki aliamka na kunyanyua pikipiki yake na kufanikiwa kuiwasha na kukimbia kwa mwendo mkali kabisa, madereva wa pikipiki wengine wa hapo kijiweni wakawa wanamuangalia tu.

Dereva wa gari kuja kutoka dereva wa pikipiki kashatokomea na hapo madereva wa pikipiki hata kusogea eneo la tukio hawakusogea.

Abiria tuliokuwa kwenye usafiri wote tulipigwa na butwaa, ingetokea dereva boda boda ndio amegongwa na mwenye gari kukimbia hapo angefukuziwa na akishikwa lazima achezee na kipigo kwanza.

Haki yako ipiganie wewe mwenyewe kwanza na sio kutegemea msaada wa wasamaria wema, unaweza ukapoteza haki yako kwa kuwategemea walimwengu.

Weekend njema!
 
Yaani hawa jmaa wanakuwaga na haraka za kijinga sana.
Kuna siku tupo kwenye daladala. Ikafika kuna sehemu daladala ikasimama kwa sababu kuna gari ilikuwa ilikuwa inakunja kuingia barabara ndogo.
Jinga moja kwa kuona gari imesimama lenyewe hata kujiuliza hakuna limefika na kupitiliza tu. Likabutuliwa huko.
Na hii ndio ajali inatokea na raia walioshuhudia wanasema sawa sawa
 
Dereva wala gari anabusara sana mambo mengi nikuacha tu hawa madereva bodaboda angetoka wengeweza kuleta fujo kumpiga hata kuchoma gari au kuiba bodaboda akili zao haziko fresh kabisa


Sent using Jamii Forums mobile app
Duu....yani kosa afanyiwe yeye na bado apingwe yeye...ila nakubaliana na ww wengi wao akili hazipo sawa zimeathirika na upepo
 
Kuna dereva bodaboda jana nimemkosa kosa kumwaga kinyesi. Nilishika brakes za ghafla sana hadi brake zikanuka kuungua.

Kisa kiko hivi, kuna sehemu ni 4 ways ambapo ni connection ya barabara ya mtaa inayokatiza main road.

Sasa kwa kawaida mtu anayetoka barabara ya mtaa anatakiwa asubirie gari za mainroad zipite ndipo avuke, kilichotokea yeye ametoka alikotoka akaunga na 100 asijue kuwa main road kuna gari linakuja kuhamaki nilikuwa nambamiza ubavuni maana nilikuwa na kama 60 kph ubaoni.

Nilibana brake nikamkemea na kunyoosha.
 
Hawa jamaa wa bodaboda ni bomu linalosubiri kulipuka. Tabia zao ni aina moja Tanzania nzima.

Wakiwa barabarani hawafuati kabisa sheria za barabara. Hawajali taa za kuongoza magari, wengi wao ni wagomvi na kujifanya wababe. Mbaya zaidi wanakuwa na umoja wa kijinga haswa linapotokea jambo linalomhusu mmoja wao.
Huwa hawana busara ya kuangalia tukio kwa uhalisia wake.

Jambo la Ajabu na la kushangaza; serikali (polisi) imewafumbia macho hawa watu kiasi kwamba wanajiona wako juu na sheria za nchi haziwahusu kabisa. Wamefikia hatua ya kuunda umoja haramu wa kujihami,kupiga watu na kuharibu mali za watu bila kuchukuliwa hatua yoyote.

Huko Arusha miaka ya nyuma walimuandama jamaa mmoja aliyemgonga mmoja wao mpaka jamaa akajiua.
Hatari sana!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom