Lugumgya
JF-Expert Member
- Dec 10, 2019
- 629
- 1,997
Mwaka fulani nikiwa Chuo, Dr. ....alituambia twende kwenye Kijiji fulani kwa ajili kujifunza mbinu za Ushirikishwaji Jamii katika kutatua changamoto zinazowazunguka na kubaini vipaumbele vya mahitaji yao. Moja ya mbinu hiyo ilikuwa Participatory Rural Appraisal (PRA), n.k.
Logistics zote zikawekwa sawa. Siku ya tukio tulitangulia na yule Dr.....alibaki ili atujoin baadae. Siye tulivofika kijijini pale kwa gari la kukodi, tukatulia na kuanza kuchati ili tumsubiri mwalimu wetu huyo.
Baada ya saa kama mbili hivi akaja, alivofika tulikuwa hatujafanya chochote. Akachukia Sana. Alituuliza maswali mawili?
1. Inawezekanaj Wanafunzi wa Chuo Kikuu, mnatatoa fedha kukodi gari kuja kuchati wakati mngeweza kuchati mkiwa mmelala vitandani kwenu?
2. Je, kweli nyie ni Wanafunzi wa Chuo Kikuu, na mnatambua wajibu wenu kwa Taifa lenu?
Nimeamua kumrejea mwalimu wangu, baada ya kuona kinachoendelea bungeni, nikiwa nafuatilia mjadala wa mapendekezo ya bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi leo.
HALI ILIKUWA HIVI.
1. Mbunge wa Kwanza.
Mh. Spika nakushukuru kwa kuongoza Bunge vizuri. Nampongeza pia Mh Lukuvi kwa kuchapa kazi. Alikuja jimboni kwangu akachezewa ngoma za jadi, nafikiri zimemhamasisha kuchapa kazi. Ameshakuja jimboni kwangu Mara 2 na blah blah nyingine. Then, naunga mkono hoja kwa asilimia ! Kwaa! Kwaaa! Kwaaa! Kwaaa! Kwaaa!
2. Mbunge wa Pili.
Mh spika nakushukuru kwa nafasi. Nafahamu vizuri mh Lukuvi tangu alipoteuliwa Mara ya kwanza kuwa DC, Bukoba. Mimi nilikuwa afisa utumishi na utawala wa Mji. Nilimzungusha Mjini, na kumtoa ushamba wa mji. Tangia hapo anapaa tu. Na blah blah nyingine. Then, kwaaa!kwaaa! Kwaaa! Kwaaa! Kwaaa!
3. Mbunge wa Tatu.
Ahsante Mh Spika kwa kunipatia nafasi. Waziri hongera Sana, unachapa kazi isiyokuwa na mfano. Wengine nafikir wanapaswa kujifunza kutoka kwako. Umetusogezea huduma pale wilayani, badala ya mkoani Kama ilivyokuwa awali. Tunashukuru Sana. Naunga mkono hoja asilimia mia moja. Then, kwaa! Kwaaa! Kwaaa! Kwaaaa!
Nimejaribu kurejea kwenye maswali ya mwalimu wangu, miaka hiyo. Labda kwa sababu hakuwa mtanzania ndo maana alituona wajinga kutumia raslimali kwa Mambo yasiyo kuwa na tija. Unawezaje kuchangia mapendekezo ya bajeti kwa stori!? Unawezaj kuchangia mapendekezo ya bajeti kwa kusema ulivyomtembeza mtu mjini. Ina ongeza nn kwenye mapendekezo husika? Au jinsi alivyochezewa ngoma za jadi alivokuja kwenye Jimbo lako? Inaongeza nini na inatija gani kwenye hicho unachokichangia?
Fikra zangu zilikuwa zinaniambia kuwa kazi yao itakuwa ni kuibua Mambo muhimu kwa ajili ya kuboreha hayo mapendekezo na kushauri kwa kina ili kutatua changamoto zilizopo katika Wizara husika. Kumbe kwa Waheshimiwa wetu ni tofauti.
Binafsi natambua mchango wa Bunge katika Maendeleo ya Taifa letu, lkn natambua namna baadhi wabunge walivyogeuka kuwa mwiba mkali dhidi ya raslimali za Taifa letu. Wanazitumia bila huruma.
Unawezaj kulipwa pesa za kujikimu na pesa za kikao kwa ajili ya kupiga stori. Kwa ajili ya kuwaambia watu namna ulivyotembelewa Mara 2 na Waziri. Namna ulivyo mtembeza DC kujua mji? Nimesikitika na ukweli mmetuangusha.
Sasa kama michango ndo hiyo, Kuna tofauti gani na hao CHADEMA ambao hawashiriki. Kama michango ndo hiyo ni sawa na kwamba mmechukua fedha kwa kazi ambayo siyo yenyewe. Kusifia na stori badala ya kujielekeza kwenye hoja. Kama CHADEMA wnapaswa kurejesha posho za kujikimu, nyie mlioshiriki pia mnapaswa kurejesha hizo fedha, mbaki na za kikao kwa sababu mmehudhuria. Lakini kama mnajikimu ili kutekeleza wajibu wenu, tekelezeni kwa weledi. Maaana nafikiri uwezo mnao, tena Mkubwa tu.
Nahitimisha kwa kurejea maswali ya mwalimu wangu kwenu;
1. Inawezekanaj Wawakilishi wa Wananchi mkapokea fedha za kodi ya Wananchi kwa ajili ya kwenda kusifia na kupiga stori, wakati mngeweza kusifiana na kupiga stori mkiwa mmelala vitandani kwenu? Huo muda mnaopata, nashauri muutumie vizuri kuibana Serikali ili itusaidie Wananchi kutoka kwenye umaskini tuliyo nao.
2. Je, kweli nyie ni Wawakikishi wa Wananchi, na mnatambua wajibu wenu kwa Taifa lenu?
Nawasilisha kwa masikitiko.