Kwa hiki analichokifanya Freeman Mbowe ameshindwa tu kuwa muwazi kama TLP

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,720
21,778
Habari wanaJamiiForums,

Siasa nzuri pale mmoja wao akiwahi kusoma akama za nyakati halisi. Na hili nimesisitiza sana huko nyuma Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe kama atasoma nyakati vyema apumzike kugombea uraisi

Else atakutana na aibu kubwa kilichofanyika ni sawa na kusema CHADEMA mmeifuata TLP kuruhusu Mgombea wetu Dr. John Pombe Magufuli ndie chaguo la Wananchi

Nakutakia kila la kheri mzee wangu huko Jimbo la Hai
 
Yaani ukiandika kwa herufi kubwa hivyo unaondoa hamasa ya watu kuchangia uzi wako maana unaoneka unapayuka siku nyingine jitahidi kufuata utaratibu umenieelewa.
 
Vyama Pinzani kujitanzua kutoka kwenye mitego na mapandikizi ya CCM itachukua miaka mingi ijayo

Muda ni Mwl
 
Usiwe na wasiwasi alishamuachia Lissu, sasa tunatafuta muungano na vyama vingine vya siasa ili mambo yanyooke zaidi.
Lissu au Nyalandu au Membe - nani atamwachia nini nani!? Ni akina nani wanaweza kumwachia NANI hicho kiti cha kugombea urais kutoka kambi ya upinzani!? Tusubiri tuone au wewe unasemaje juu ya hili!?
 
Nachojua Mbowe ni mtia nia kati ya watia nia wengine wengi kama Mchungaji Msigwa na Lissu.
Kura ndio mwamuzi,hakuna haja ya kujidanganya kwa hilo.Uchaguzi wa October ni wa kujenga Chadema sio wakutegemea kupata ushindi wa kishindo.
Quick fix politics bila kuangalia undani wa makubaliano na vyama vingine sio solution.
Jenga msingi wa chama kwenye mwamba sio mchangani.Labda ndio sababu Mbowe yupo kimya ana plan B.
 
Lissu au Nyalandu au Membe - nani atamwachia nini nani!? Ni akina nani wanaweza kumwachia NANI hicho kiti cha kugombea urais kutoka kambi ya upinzani!? Tusubiri tuone au wewe unasemaje juu ya hili!?
Mimi naona isipokuwa serikali imkamata Lissu au kumzuia kugombea, Lissu ndiye atakayepeperusha bendera ya CDM kwani hadi sasa anaonekana mwenye mvuto zaidi ya Nyalandu na Membe. Umeona hata Mbowe sijamtaja kwani inaonekana wazi atajitoa mapema au pengine alishafanya hivyo kwani nasikia anagombea jimbo la Hai.

Nyalandu anafaa na anaweza kuchukua nafasi endapo Lissu hatagombea. Membe kugombea kwa ticket ya CDM inaonekana itakuwa vigumu mwaka huu ila akiweza kuacha kwa Lissu na kumuunga mkono Lissu katika "UKAWA",basi upinzani utakuwa na nguvu zaidi. Watu wengi wamechoka na wanataka mabadiliko, kama serikali haitacheza rafu, watu wategemee mchuano mkubwa sana mwaka huu pengine kuliko mwaka 2015.
 
Hiyo ni tathimini yako fazili na mimi nina tabia ya kuheshimu mawazo ya kila mwana JF ingawa SIYO LAZIMA nikubaliane nayo; hivyo tusubiri tuone ingawa sidhani kama Membe atakuwa tayari kumwachia yeyote kati ya Lissu au Nyalandu nafasi ya kugombea urais mwaka huu kupitia muungano wowote. Membe angekuwa na subira ya namna hiyo, angesubiri 2025 kwa tiketi ya CCM, lakini kwa uchu wake alioonesha mwaka huu na hasa hasa akiamini bado ana visenti vya kumwaga kwa wapiga kura. Visenti alivyo vifisadi vya chenji ya RADAR na vile vya Libya. Anyway tuwe na subira wakati pia tukichangamsha akili zetu kwa HOJA mwanana, au siyo fazili?!
 
Back
Top Bottom