Kwa hii CHADEMA/UKAWA ya sasa Prof. Lipumba, Dr. Slaa naomba mtusamehe, 2015 Tuliwakosea sana

Deo Shy

Member
Oct 18, 2016
98
300
2015 baada ya Dr. Slaa na Prof. Lipumba kutoka katika muungano wa UKAWA na vyeo walivyokuwa navyo ndani ya CHADEMA na CUF wananchi wengi waliwananga (mimi nikiwa moja wao), na kuona ya kwamba hawataki kuleta mabadiliko, kwamba wao ndio kizingiti katika kuleta mabadiliko..

Baada ya miaka miwili hasa nikitafakari yanayoendelea ndani ya CHADEMA na UKAWA nadiriki kuwaomba msamaha Dr. Slaa na Prof. Lipumba. Kwa hakika nyie mlipewa maono na mkaona mbali. Wananchi wengi tuliopumbazwa na lile wimbi la mabadiliko, tunaomba mtusamehe. Hatukujua kama mna upeo na maono kiasi hicho...

Leo tazama kinachoendelea CHADEMA. Chama hakijui kinaelekea wapi, viongozi wanapigana wenyewe kwa wenyewe. Wanachama hawajui direction ya chama. Wabunge hawajielewi wamebaki kutukana Rais. Wabunge wao wanafikiri kuongea kwa sauti au kwa kutukana ndio kujenga hoja ya kukubalika kwa wananchi. Chama kinapinga kila kitu hata liwe jambo lenye maslahi pana kwa umma. Chama kimekuwa watetezi wa mafisadi na wala rushwa. Chama kimekuwa cha kichochezi kila siku.

Baada ya kushindwa katika ulingo wa ushindani na CCM, sasa wameamua kupigana wenyewe kwa wenyewe. Kila siku wanatukanana, wanashutumiana na kujenga matabaka mawili. Washika dau wa chama hao ni wafuasi kinda kinda wa Mbowe na Lowassa na wale wanaoonekana wakuja hawa wamewekwa chini ya uangalizi na hawatakiwa kuchangia chochote na pia hawatakiwi hata kushiriki misiba ya CCM.

Kwa hakika Dr. Slaa na Prf. Lipumba mliona mbali. Na kweli mzidi kubarikiwa. Mmeliokoa Taifa hili chini ya wezi, wala rushwa, wajivuni, wanaojifanya wanajua kila kitu. Watu wenye roho mbaya n.k..

Sent from my SM-N9005 using JamiiForums mobile app
 
Sio Bure, umenunulia na ccm
Ndio lugha wanazotumia kwa sasa pale wanapoambiwa ukweli.... Hawa watu hawataki kuambiwa ukweli, ukweli kwao ni sumu.... Kwa hakika tumshuku sana Mungu kwa uchaguzi wa 2015... Hawa majamaa wangeshinda nchi ingekuwa ya ajabu sana sana

Sent from my SM-N9005 using JamiiForums mobile app
 
Walioshinda nchi 2015 ndio wa ajabu ajabu kabxaa, huoni mambo yanavyoenda??? Ndugu yangu amka ww usiwe masikini wa kufikiri
 
2015 baada ya Dr. Slaa na Prof. Lipumba kutoka katika muungano wa UKAWA na vyeo walivyokuwa navyo ndani ya CHADEMA na CUF wananchi wengi waliwananga (mimi nikiwa moja wao), na kuona ya kwamba hawataki kuleta mabadiliko, kwamba wao ndio kizingiti katika kuleta mabadiliko..

Baada ya miaka miwili hasa nikitafakari yanayoendelea ndani ya CHADEMA na UKAWA nadiriki kuwaomba msamaha Dr. Slaa na Prof. Lipumba. Kwa hakika nyie mlipewa maono na mkaona mbali. Wananchi wengi tuliopumbazwa na lile wimbi la mabadiliko, tunaomba mtusamehe. Hatukujua kama mna upeo na maono kiasi hicho...

Leo tazama kinachoendelea CHADEMA. Chama hakijui kinaelekea wapi, viongozi wanapigana wenyewe kwa wenyewe. Wanachama hawajui direction ya chama. Wabunge hawajielewi wamebaki kutukana Rais. Wabunge wao wanafikiri kuongea kwa sauti au kwa kutukana ndio kujenga hoja ya kukubalika kwa wananchi. Chama kinapinga kila kitu hata liwe jambo lenye maslahi pana kwa umma. Chama kimekuwa watetezi wa mafisadi na wala rushwa. Chama kimekuwa cha kichochezi kila siku.

Baada ya kushindwa katika ulingo wa ushindani na CCM, sasa wameamua kupigana wenyewe kwa wenyewe. Kila siku wanatukanana, wanashutumiana na kujenga matabaka mawili. Washika dau wa chama hao ni wafuasi kinda kinda wa Mbowe na Lowassa na wale wanaoonekana wakuja hawa wamewekwa chini ya uangalizi na hawatakiwa kuchangia chochote na pia hawatakiwi hata kushiriki misiba ya CCM.

Kwa hakika Dr. Slaa na Prf. Lipumba mliona mbali. Na kweli mzidi kubarikiwa. Mmeliokoa Taifa hili chini ya wezi, wala rushwa, wajivuni, wanaojifanya wanajua kila kitu. Watu wenye roho mbaya n.k..

Sent from my SM-N9005 using JamiiForums mobile app
Lipumba naye ni wakuomba msamaha? Du! Dunia simama niteremke. Bora ungesema Dr slaa, siyo huyo siyejitambua

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Jina lako linaonesha we ni mkanda ya ziwa, hongera kwa kutema pumba hiz mchana kweupe

Sent from koromije using bashite
 
Back
Top Bottom