Kada wa CHADEMA
JF-Expert Member
- Feb 27, 2016
- 289
- 615
Kwa sasa imekuwa ni aibu kubwa kujitambulisha hadharani kuwa mimi ni mwana CHADEMA kutokana na aibu kubwa ambayo wabunge wetu wa UKAWA wanatuletea kule Dodoma. Ndio maana hata zile sare za CHADEMA ambazo ilikuwa ni kawaida kuziona mitaani kwa sasa zimepotea kabisa. Imekuwa ni kawaida katika maisha yetu ya kila siku kuwa mtu anayesusa mara nyingi ndiye anayepata hasara. Ndio maana kuna msemo wa Kiswahili unaosema kuwa UKISUSA SISI TWALA.
Ndivyo inavyotokea Bungeni, maamuzi yetu ya kususa vikao vya bunge eti kwa vile tu hatumpendi Naibu Spika, Daktari Tulia Akson yamekuwa na mafanikio Hasi kwa Kambi ya Upinzani. Hii ni kutokana na ukweli kwamba, kususa kwetu hakujakwamisha mijadala ya bunge la Bajeti Bungeni. Sana sana imeongeza speed ya wabunge wa CCM kupitisha bajeti hiyo bila kuwa na michango yetu.
Nakumbuka wakati wa Uteuzi wa Wabunge wa Viti Maalum CHADEMA, Baraza la Wanawake CHADEMA walitenga nafasi moja kwa mama yetu Regina Lowasa kutokana na mchango alioutoa kwa umoja huo na chama kwa ujumla wakati wa kampeni za Urais. Hata hivyo, mama yetu alitumia busara kukataa nafasi hiyo. Alikataa si kwa sababu hakupenda kujenga historia kuwa aliwahi kuwa mbunge bali aliona mbali kutokana na hulka za viongozi wa kambi ya Upinzani na hasa mwenyekiti wetu Freeman Mbowe.
Bunge lililopita, CHADEMA tulideka sana Bungeni na mara nyingi tuliweka mpira kwapani. Mama Regina Lowasa aliona hilo kuwa hata Bunge hili, hali na tabia ya viongozi wa upinzani itakuwa ile ile ndo maana akaamua kukataa nafasi hiyo.
Najaribu kutengeneza taswira. Hivi na yeye kama angekuwa Mbunge, angefuata mkumbo wa kususa? Kama angefanya hivyo, hakika tusingemtendea haki mama yetu kwa kumuingiza bungeni then baada ya dakika tano tunamtoa. Hii inga toka inga toka inga toka hakika ingekuwa ni kumtusi mama yetu na Mzee Lowasa.
Hakika CHADEMA tusipobadilika, tutaendelea kuwa na wabunge fuata mkumbo na si wenye maono kama Mama Regina Lowasa