Kwa Heshima ya Haika na Hygeia: Bei ya Kupandisha Dume..

Mtoboasiri

JF-Expert Member
Aug 6, 2009
5,101
1,946
Mfugaji mmoja alikwenda kwa mfugaji mwenzake (ambae pia ni bwana mifugo wa eneo lao) asubuhi moja. Alipobisha hodi mtoto wa kiume wa umri upatao miaka 12 akamfungulia mlango. Mazungumzo yafuatayo yakafuatia:

Mkulima: Baba yako yupo?

Mtoto: Hapana Mzee, amekwenda mjini.

Mkulima: Mama yako?

Mtoto: Nae kaenda mjini na baba.

Mkulima: Kaka yako Howard yupo?

Mtoto: Nae hayupo, wote yeye, baba na mama wamekwenda mjini. Kwani una shida gani? Kama kuna kitu unahitaji niambie maana nimeachiwa funguo na najua vifaa vinapowekwa.
Mzee akawaza kidogo halafu akasema: Kwa kweli nilitaka kuongea na baba, mama au kaka yako kwa kuwa kaka yako amempa mimba binti yangu.

Mtoto akafikiria kidogo halafu akasema: Kusema ukweli itabidi umsubirie baba, ila kwa kukusaidia ni kuwa baba hulipisha shilingi laki moja kwa kupandisha dume la ng'ombe na elfu hamsini kwa beberu. Ila sijui baba hutoza shilingi ngapi kwa Howard akifanikiwa kutia mimba.
 
Kwa Heshima ya Haika na Hygeia:
Background: Joke hii ilitoka mara ya kwanza kwa lugha ya kiingereza ikiwa na mandhari ya kimarekani.Ilianza hivi: A Idaho farmer............. Nikaisoma nikamwambia mleta joke hivi: Kwa nini hukuchakachua hii joke iwe na maudhui ya Kitanzania?
Ndo naona Mtoboasiri kaitafsiri joke kwa kiswahili na imenoga kuliko ile ya kiingereza iliyojaa umarekani. Nashukuru Mtoboasiri kwa kuguswa na malalamiko yangu. Nakuona uko tofauti na baadhi ya WanaJF ambao hawapendi ukosoe post zao. Nakumbuka nililalamikia post moja ya joke hapahapa, na mleta post akajibu:: 'Wewe ni boya'. Nashukuru Mtoboasiri, kwako mimi si 'boya'
 
Asante sana mkuu! Nimefarijika (and humbled - Kiswahili chake kimenitoka) sana kwa bandiko lako. Kusema ukweli nimejifunza na kuona thamani ya kukosolewa na kukubali kukosolewa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom