Kwa heshima tuliyopewa Watumishi wa Umma ndani ya hii miaka 5, hakika nitachapa kazi kwa uadilifu

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,480
35,371
Huu Uzi nauandika nikiwa na machungu sana.
Miaka mitano
- Sijapandishiwa mshahara
- Sijapanda daraja
-I ncrement ya mbinde.
- Kazi yetu kama Watumishi wa Umma haithaminiwi. Wanaoshukuriwa kwenye mikutano ni watumishi wa Vyombo vya dola tu.
- Kila siku kiongozi mkuu anasema fedha ziko za kutosha ila ustawi wa watumishi sio kipaumbele.

Haki na wajibu ni vitu ambavyo vinakwenda sambamba. Sasa kinachofanyika ni kuhimizwa tutimize wajibu lakini haki zetu hazizungumzwi.
Serikali inajifanya inanijali nami nitajifanya natimiza wajibu wangu.
 
United we stand. Devided we perish!

Wapi kachero mbobezi na crew nzima ya ACT wazalendo?
 
- Mkuu kama wameshindwa kuwapandisha mishahara kapandeni mabasi wenyewe mwende muendako!

- Hamjapanda madaraja kivipi mkuu?,mbona madaraja yapo kibao,anzeni na hilo la hapo Tazara kisha la ubungo likikamika mtaenda pia kulipanda bure kabisa!

tukiacha unafiki japo madaraja hayajapanda lakini utawala huu uhakika wa mshahara upo tena kwa wakati si kama utawala uliopita, watu walikua na malimbikizo ya mishahara awamu ilopita lakini yameshughulikiwa vizuri

hakuna utawala usio na changamoto kwa hiyo kutopanda madaraja ndo changamoto ya utawala huu
 
Kati ya watu 500 wanalipwa watu 3 halafu unasema malimbikizo yameshughulikiwa. Kama wewe umelipwa shukuru Mungu. Watu bado wanadai malimbikizo ya nyuma hadi malimbikizo mapya yanakuja yanakutana inakuwa malimbikizo juu ya malimbikizo.
 
tukiacha unafiki japo madaraja hayajapanda lakini utawala huu uhakika wa mshahara upo tena kwa wakati si kama utawala uliopita, watu walikua na malimbikizo ya mishahara awamu ilopita lakini yameshughulikiwa vizuri

hakuna utawala usio na changamoto kwa hiyo kutopanda madaraja ndo changamoto ya utawala huu
 
tukiacha unafiki japo madaraja hayajapanda lakini utawala huu uhakika wa mshahara upo tena kwa wakati si kama utawala uliopita, watu walikua na malimbikizo ya mishahara awamu ilopita lakini yameshughulikiwa vizuri

hakuna utawala usio na changamoto kwa hiyo kutopanda madaraja ndo changamoto ya utawala huu
Nilioahiriwa nao June 30 ,2015 kuna baadhi mpaka leo hawajalipwa mshahara wao wa July 2015. Mimi nililipwa
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom