Mohamed Ismail
JF-Expert Member
- Mar 16, 2014
- 214
- 229
Baniani Mbaya, Kiatu chake Dawa
_______________________
Watu wengi wamekuwa wakimzungumzia Pierre Nkurunzinza kwa namna moja pekee ya uwi (ubaya) ambao kila mmoja anao tunapishana viwango tu. Lakini ukimtumpia jicho la tija hususani kwa Burundi na Tanzania; Pierre alikuwa ana tija.
Mosi, aliifanya Burundi kuwa nchi inayoweza kutawalika kutoka kwenye tawala za kibabe na kivita na walau kuwa taifa ustaarabu wa kiwango chake. Ndani ya uongozi wa Nkurunzinza, Burundi kwa mara ya kwanza ilikuwa na uwezo wa kutoa kikosi cha askari (wanajeshi) kwenda kulinda amani. Kwa nchi iliyokuwa ina uchovu wa vita vya wenyewe kwa wenyewe kuweza kutoa kikosi cha kulinda amani kwenda nchi nyingine si jambo dogo (watu wa ulinzi wanaelewa zaidi). Nkurunzinza aliirudisha Burundi katika hali ya kuwa taifa na alikuwa mzalendo kindakindaki wa nchi yake. Nchi iliyokuwa haina Ikulu ikawa nayo (kwa usaidizi wa waChina), kukawa na ujenzi wa miundombinu na kupungua kwa wakimbizi wanaoikimbia nchi yao.
Pili, kwa Tanzania, kutengemaa kwa Burundi kulikuwa ni afua kwa mikoa ya mipakani. Mikoa ya Kigoma na Kagera ilikuwa maskani ya wakimbizi wa kiRundi waliokuwa sehemu ya chanzo cha uharibifu wa mazingira, gharama za kuwatunza na ujangili uliokuwa unahatarisha usalama wa mikoa hiyo.
Ndani ya Burundi ya Nkurunzinza, malaki ya raia wa Burundi waliokuwa wakimbizi nchini Tanzania waliweza kurudi nchini mwao tangu kipindi cha Rais Kikwete hadi wakati huu wa Rais Magufuli. Tuliona Rais Kikwete alivyotumia "busara" kuhakikisha Nkurunzinza anarudi Burundi baada ya mapinduzi dhidi yake yaliyofanyika wakati wa Mkutano wa EAC wa mwaka 2015 nchini Tanzania. Vilevile, tumeona namna Rais Magufuli na Nkurunzinza walivyokutana Ngara mwaka 2017 na kufanya mikataba yenye lengo la kuhimiza waRundi warudi kwao kuijenga nchi yao.
Miaka kama miwili iliyopita tuliona Rais Museveni na Rais Magufuli wakiiambia Rwanda iache kuingilia mambo ya ndani ya Burundi. Kauli hiyo ilikuwa inaonesha namna Afrika Mashariki ilivyokuwa inauona umuhimu wa utulivu wa Burundi kwa eneo zima la Maziwa Makuu.
Leo hii si ajabu kuona Tanzania na Kenya kurusha bendera nusu mlingoti kwa ajili ya Rais Pierre Nkurunzinza. Chambilecho wahenga: baniani mbaya kiatu chake dawa.
Tangulia kamanda.
Gervas A. Kasiga (Rutakirwa)
Idodomiya
13-06-2020