Kwa heri Desmond Tutu. Alama dhidi ya ubaguzi wa rangi na udhalimu duniani

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,339
45,659
Alipata kusema, “If you are neutral in situations of injustice, you have chosen the side of the oppressor. If an elephant has its foot on the tail of a mouse, and you say that you are neutral, the mouse will not appreciate your neutrality.”

Kwa tafsiri isiyo rasmi;
"Ukiwa nyutro kwenye hali udhalimu umechagua upande wa mdhulumaji, kama unaona Tembo ameukanyaga mkia wa panya na wewe unasema uko nyutro panya hatafurahia unyutro wako"- Desmond Tutu

Mwana mwema wa bara la Africa. Unastihili kupumzika kwa amani, Africa itakukosa sana na utakumbukwa daima kwa kutumia mimbara yako ya dini kama jukwaa madhubiti dhidi ya uovu wa ubaguzi wa rangi na dhuluma ya binadamu mmoja mwenye mamlaka kwa mwingine.

Miaka yako 90 hapa chini ya jua haikuwa ya bure bali ya uongozi ulioutukuka katika uwanja wa mapambano ya haki na usawa wa binadamu. Sifa yako kuu ya tofauti na viongozi wengine wengi wa dini ni kutokubli kukaa kimya au kumung'unya maneno uliopoona dhuluma.
 
Bila shaka Dunia bado ilikuwa inamuhitaji, hasa kipindi hichi ambacho baadhi ya watawala wanafanya mambo kama ya Makaburu kwa wananchi wao, UKAPUMZIKE PARADISO DES,TUTU.
 
Hamba Kahle, Lala Ngoxolo Tata Omukhulu DUSMOD MPILO TUTU.
Ulale ngokuthula Archbishop Desmond Tutu, uyibekile induku ebandla. Umhlaba wonke nomndeni wakhe ngathi ungathola ukududuzeka ngalesis'khathi esinzima #RIPDesmondTutu
 
Apumzike kwa amani Desmond Tutu.

Katika jumbe zote za maombolezo zote ni masikitiko kwa kwenda mbele.

Funzo: jamii inavyo chukizwa nasi katika uhai au vifo vyetu, busara kujihoji tutakuwa hatuko katika njia iliyo sahihi.
 
Kizazi cha dhahabu kinaondoka jukwaani, na jukwaa linatawaliwa na kizazi cha chuma kilichojipaka rangi ya dhahabu...
 
Ndiyo askofu wa kwanza mwafrica muangalikana kuwa na akili nyingi.
 
Back
Top Bottom