Kwa haya yanayotendeka Zanzibar BAKWATA na BARAZA LA MAULAMAA mko wapi?

mzee wa njaa

JF-Expert Member
Jun 16, 2011
1,366
223
Baada ya kujiuzuru Ubunge Rostan Aziz ambaye alikuwa Mbunge wa Igunga, tume ya Uchaguzi iliitisha Uchaguzi mpya katika jimbo hilo lililoko Mkoa wa Tabora na nia hasa ni kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Mbunge huyo.

Na ikumbukwe baada ya kurudiwa uchaguzi huo Mbunge wa CCM aliibuka kidedea kwa ushindi wa zaidi ya tofauti ya kura 3000 dhidi ya mpinzani wake Bw. Kashindye kutoka chama cha chadema.

YALIYOJIRI KATIKA UCHAGUZI HUO:

Mkuu wa Wilaya hiyo yasemekana alivuliwa HIJAB wengine wanaita mtandio na inavyosemekana ni wafuasi wa Chadema. Cha kushangaza BARAZA LA MAULAMAA TANZANIA lilitoa tamko kali eti Mkuu huyo wa Wilaya alidhalilishwa sana na pia Uislam ulidhalilishwa pia. Na kikubwa zaidi walikuwa wakiita Press Conference kwania ya kuelezea uislam ulivyochafuliwa kwa Mkuu huyo wa Wilaya kuvuliwa HIJJAB.

Cha kujiuliza hivi yanayotendeka Zanzibar kwa baadhi ya MAKANISA KUCHOMWA MOTO Je, Baraza la Maulamaa na BAKWATA hawalioni hili tatizo????

Mbona wamekaa kimya pasipo sababu za msingi? Kukaa kwao kimya kunapelekea watu waamini kwa tamko walilolitoa kuhusu kuvuliwa Hijjab kwa Mkuu waWilaya kule Igunga kulikuwa kunaashiria KUNUNULIWA NA MAGAMBA KAMA KAWAIDA YAO.

Kama kweli wao ni wapenda haki basi watoke hadharani kama walivyoita waandishi wa Habari kwenye tukio la Igunga, ndio tutaamini wao wana uchungu na Uislam.

Au kuchomwa moto MAKANISA wao haiwaumi ila la Hijjab ndio waliloliona la maana sana!!!!

Tunaomba majibu ya kueleweka.....
 
Wanakubaliana na hayo yaliyofanywa na wenzao. Kamwe mungu hawezi kuchanganywa na shetani. Ishimail kamwe hawezi kuwa na mamlaka juu ya Isaka! Waache wa chome laana hiyo haitawaacha salama!
 
Back
Top Bottom