Witmak255
JF-Expert Member
- Feb 5, 2019
- 3,264
- 5,403
Kuna mambo mengi yanatokea huko nchi za nje lakini hili la South Africa limenitafakarisha kidogo, Kama utamaduni tuna embassies katika nchi nyingi hapa duniani, Tumepeleka mabalozi katika hizo nchi na nje ya Balozi kunakuwa na Balozi mdogo Councillor na office staff. Binafsi sijui hasa hawa mabalozi huwa wanafanyaga nini? Hivi huwa wanafanyiwa performance review?.
Pamoja na mambo mengine moja ya kazi za balozi duniani kote ni pamoja na Kusaidia Raia wake wakiwa nje incase kuna matatizo yanayoashiria ukosefu wa amani kwa raia husika huko nje, angalia nchi za ulaya, Ona USA na chi zingine zilizoendelea wanatoa alert kwa raia wao wakiwa nje ya nchi incase kuna viashiria vya uvunjifu wa amani na watatuma ndege inapobidi kwa usafiri na ulinzi kama kutakuwa na machafuko kuwarudisha raia wao kwao. Hawako tayari hata raia wao mmoja tu apoteze Maisha.
Ina maana hizi balozi zetu huko nje ya nchi kazi zao ni Kutoa Visa tu kwa wageni wanaotaka kuja nchini kutalii, maana hata Kutangaza nchi hasa kiutalii na uwekezaji sioni kama wanaweza…Hizi balozi zetu kwa ambao hawajawahi kusafiri nje ya nchi Mtanzania ukienda Ubalozini wanakuona kama umeenda kuwasumbua na mara nyingi wanakupuuza,, shida yako haisikilizwi, unless uwe na tabia ya kujichekesha chekesha na kujipendekeza kwao.
Angalia kinachoendelea South Africa, karibia nchi zote zinawarudisha raia wao nyumbani lakini ubalozi wetu huko kwa Madiba umetulia kama hakuna kinachoendelea, ina maana hatuna raia wetu walioko huko? Au kwao raia sio kipaumbele?
Hawa mabalozi ni wawakilishi wetu huko nchi za nje na wanatumia kodi zetu kuwa huko shida ni kama tunaona hawakituwakilishi ipasavyo, Binafsi mimi mwenyewe miaka ya nyuma nilikuwa Kenya nikawa nasumbuliwa na nilipokwenda ubalozi wetu NAIROBI Kutaka msaada wakaniambia kama watu hawawataki nchini kwao mnafuata nini? Haya yalikuwa ni majibu ya maafisa wa ubalozi wetu ikiwa nilikuwepo Kenya kihalali nikiwa na document zote
Kwa jibu hili unajiuliza hivi huyu anajua anachotakiwa kufanya akiwa kama ofisa wa ubalozi kweli?