Kwa haya yanayoendelea South Africa, yamenifikirisha kuhusu kazi za mabalozi wetu nje ya nchi

Witmak255

JF-Expert Member
Feb 5, 2019
3,281
2,000
Kuna mambo mengi yanatokea huko nchi za nje lakini hili la South Africa limenitafakarisha kidogo, Kama utamaduni tuna embassies katika nchi nyingi hapa duniani, Tumepeleka mabalozi katika hizo nchi na nje ya Balozi kunakuwa na Balozi mdogo Councillor na office staff. Binafsi sijui hasa hawa mabalozi huwa wanafanyaga nini? Hivi huwa wanafanyiwa performance review?.

Pamoja na mambo mengine moja ya kazi za balozi duniani kote ni pamoja na Kusaidia Raia wake wakiwa nje incase kuna matatizo yanayoashiria ukosefu wa amani kwa raia husika huko nje, angalia nchi za ulaya, Ona USA na chi zingine zilizoendelea wanatoa alert kwa raia wao wakiwa nje ya nchi incase kuna viashiria vya uvunjifu wa amani na watatuma ndege inapobidi kwa usafiri na ulinzi kama kutakuwa na machafuko kuwarudisha raia wao kwao. Hawako tayari hata raia wao mmoja tu apoteze Maisha.

Ina maana hizi balozi zetu huko nje ya nchi kazi zao ni Kutoa Visa tu kwa wageni wanaotaka kuja nchini kutalii, maana hata Kutangaza nchi hasa kiutalii na uwekezaji sioni kama wanaweza…Hizi balozi zetu kwa ambao hawajawahi kusafiri nje ya nchi Mtanzania ukienda Ubalozini wanakuona kama umeenda kuwasumbua na mara nyingi wanakupuuza,, shida yako haisikilizwi, unless uwe na tabia ya kujichekesha chekesha na kujipendekeza kwao.

Angalia kinachoendelea South Africa, karibia nchi zote zinawarudisha raia wao nyumbani lakini ubalozi wetu huko kwa Madiba umetulia kama hakuna kinachoendelea, ina maana hatuna raia wetu walioko huko? Au kwao raia sio kipaumbele?

Hawa mabalozi ni wawakilishi wetu huko nchi za nje na wanatumia kodi zetu kuwa huko shida ni kama tunaona hawakituwakilishi ipasavyo, Binafsi mimi mwenyewe miaka ya nyuma nilikuwa Kenya nikawa nasumbuliwa na nilipokwenda ubalozi wetu NAIROBI Kutaka msaada wakaniambia kama watu hawawataki nchini kwao mnafuata nini? Haya yalikuwa ni majibu ya maafisa wa ubalozi wetu ikiwa nilikuwepo Kenya kihalali nikiwa na document zote
Kwa jibu hili unajiuliza hivi huyu anajua anachotakiwa kufanya akiwa kama ofisa wa ubalozi kweli?
 
Witmak255

JF-Expert Member
Feb 5, 2019
3,281
2,000
Mkuu sio balozi tu wote unaowaona katika nyazifa mbalimbali za serikali wapo kwa ajili ya matumbo yao sio wewe au yule, narudia tena wote yaani wote unaowajua wewe.
mkuu wapo wenye kujua kazi zao na hao kamwe hawapewi nafasi ya kusikika
 
Witmak255

JF-Expert Member
Feb 5, 2019
3,281
2,000
Mabalozi wengi wa kiafrika kazi zao kubwa ni kunywa na Mademu na Starehe mbali mbali.ukifanikiwa kukutana nae akiongea utasema Breweries imecheua unawakuta macho mekundu halafu wanakuwa wakali kweli kweli.
kama ni hivi, hizi balozi zitakuwa ni matumizi mabaya ya pesa za umma
 
Bradha

JF-Expert Member
Dec 18, 2017
8,613
2,000
Labda kuna mambo yemefanyika na sisi hatujui.Ingependeza kama kuna anayejua azitetee hizi balozi.Zimechukua hatua gani?
 
Witmak255

JF-Expert Member
Feb 5, 2019
3,281
2,000
Labda kuna mambo yemefanyika na sisi hatujui.Ingependeza kama kuna anayejua azitetee hizi balozi.Zimechukua hatua gani?
haya mambo sio confidential mkuu, lazma tungekujua mpaka ninavoongea na wewe kuna watanzania huko South Africa wanahitaji msaada ila wamekosa
 
kakamkubwa

JF-Expert Member
Jun 20, 2013
1,182
2,000
Sometimes watanzania tuna hali fulani hivi ya kujihisi inferior mno. Hata umuoni kiongozi mkubwa kiasi gani ana kitu hicho ndani yake ndo hasa hasa hii kitu imetufikisha hapa tulipo,watanzania wote tuna nidhamu ya woga iwe upo ndani au nje ya nchi. Zaidi tunabaki kuminyana na kuoneana wenyewe kwa wenyewe.
 
ukiachana na raia, so viongozi wenye mamlaka wanaancha raia wao waangamie sababu ya uoga? na wanaoga nini wakati wao huko wana kinga ya kidiplomasia
 
kakamkubwa

JF-Expert Member
Jun 20, 2013
1,182
2,000
ukiachana na raia, so viongozi wenye mamlaka wanaancha raia wao waangamie sababu ya uoga? na wanaoga nini wakati wao huko wana kinga ya kidiplomasia
Sasa wewe unafikiri nini kinawafanya washindwe kuwasafirisha watanzania waishio kwa madiba? Mtanzania yupo tayari kumkera mtanzania mwenzake kwa kumtetea raia wa kigeni. Usikute kiongozi hapo anatoa mrejesho kuwa watanzania wote wako mahali salama wakati jana kuna member humu ndani ameandika wapo katika hali hatarishi kiusalama na wamejificha mafichmi huko kuogopa kuuliwa.
 
Witmak255

JF-Expert Member
Feb 5, 2019
3,281
2,000
Sasa wewe unafikiri nini kinawafanya washindwe kuwasafirisha watanzania waishio kwa madiba? Mtanzania yupo tayari kumkera mtanzania mwenzake kwa kumtetea raia wa kigeni. Usikute kiongozi hapo anatoa mrejesho kuwa watanzania wote wako mahali salama wakati jana kuna member humu ndani ameandika wapo katika hali hatarishi kiusalama na wamejificha mafichmi huko kuogopa kuuliwa.
daaaah aiseee
 
rodrick alexander

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
6,405
2,000
waziri wa mambo ya nje kakaa kimya mpaka sasa pia ni mwenyekiti wa mawaziri SADc, naibu wake alikuwa afrika kusini badala ya kujua juu ya vurugu na kiasi gani zimewaathiri watanzania wanaoishi huku anajitapa juu ya kuwa na phd kuhusu mabalozi wengi wanapewa kama zawadi lakini hawajui wajibu wao
 
Aisee
 
elvischirwa

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
6,945
2,000
Kuna mambo mengi yanatokea huko nchi za nje lakini hili la South Africa limenitafakarisha kidogo, Kama utamaduni tuna embassies katika nchi nyingi hapa duniani, Tumepeleka mabalozi katika hizo nchi na nje ya Balozi kunakuwa na Balozi mdogo Councillor na office staff. Binafsi sijui hasa hawa mabalozi huwa wanafanyaga nini? Hivi huwa wanafanyiwa performance review?.
Pamoja na mambo mengine moja ya kazi za balozi duniani kote ni pamoja na Kusaidia Raia wake wakiwa nje incase kuna matatizo yanayoashiria ukosefu wa amani kwa raia husika huko nje, anagalia nchi za ulaya, Ona USA na chi zingine zilizoendelea wanatoa alert kwa raia wao wakiwa nje ya nchi incase kuna viashiria vya uvunjifu wa amani na watatuma ndege inapobidi kwa usafiri na ulinzi kama kutakuwa na machafuko kuwarudisha raia wao kwao. Hawako tayari hata raia wao mmoja tu apoteze Maisha.
Ina maana hizi balozi zetu huko nje ya nchi kazi zao ni Kutoa Visa tu kwa wageni wanaotaka kuja nchini kutalii, maana hata Kutangaza nchi hasa kiutalii na uwekezaji sioni kama wanaweza…Hizi balozi zetu kwa ambao hawajawahi kusafiri nje ya nchi Mtanzania ukienda Ubalozini wanakuona kama umeenda kuwasumbua na mara nyingi wanakupuuza,, shida yako haisikilizwi, unless uwe na tabia ya kujichekesha chekesha na kujipendekeza kwao.
Angalia kinachoendelea South Africa, karibia nchi zote zinawarudisha raia wao nyumbani lakini ubalozi wetu huko kwa Madiba umetulia kama hakuna kinachoendelea, ina maana hatuna raia wetu walioko huko? Au kwao raia sio kipaumbele?
Hawa mabalozi ni wawakilishi wetu huko nchi za nje na wanatumia kodi zetu kuwa huko shida ni kama tunaona hawakituwakilishi ipasavyo, Binafsi mimi mwenyewe miaka ya nyuma nilikuwa Kenya nikawa nasumbuliwa na nilipokwenda ubalozi wetu NAIROBI
Kutaka msaada wakaniambia kama watu hwawataki nchini kwao mnafuata nini? Haya yalikuwa ni majibu ya maafisa wa ubalozi wetu ikiwa nilikuwepo Kenya kihalali nikiwa na document zoteKwa jibu hili unajiuliza hivi huyu anajua anachotakiwa kufanya akiwa kama ofisa wa ubalozi kweli?
Kaa nyumbani mbona yeye ametulia tuli Magogoni. Mjerumani kaita mara mbili tumeuchuna.
 
Thebroker

JF-Expert Member
Aug 26, 2016
850
1,000
Tishio jipya

As taxi drivers , we are announcing that on the 9th of September 2019 from 08:00 am. We are going to kill all foreign nationals. We are declaring a strike from all the cities in KZN, Cape Town, Eastern Cape and all provinces. We are marching to the parliament. There shall be Blood-shed and fire smelling the whole South Africa. The President of the country has failed as well as police Minister has failed to deal with crime committed by foreign nationals. Minister of Home affairs Motsoaledi has also failed to prevent them from entering our boarders. Our children are addicts of drugs, high rate of crimes committed, child kidnapping and prostitution, fake certificates /qualifications, fake bank cards and teenage pregnancy. Our youth is unemployed; they are driving luxury cars, having churches, owning businesses on all the streets of South Africa. They do all fake goods and South Africa smells of churches owned by them. They own everything that we don’t have as South Africans. When and how did they enter in our country, we need an answer. Because our leaders were using the slogan “Thuma Mina (send me)”; now we are speeding up the process and fix everything. This is our land; their children are not addicted to nyaope / wunga as our children have and died. All these churches owned by them should be closed and if anyone will go to work on the 9th; we are going to kill whoever especially at the airports, home affairs and we are going to bomb the whole South Africa there will be shedding of blood. Smoke of guns and fire will smell the whole country. In KZN, everything will be closed we don’t want these people they must go back to their own country. We offer them Lesotho as Zulus, we are not scared. As the transport organisation we are saying the gates you used to come in are now open to leave. We are giving you until the weekend to leave, if you’ll still be here on Monday, we are taking the law into our hands as Zulus. In Mpumalanga we are going to destroy everything and anything. In JHB, Pretoria and Cape we are going to kill Nigerians, Ghanaians, Congolese, Tanzanians, Malawians, Zimbabweans, Mozambique’s, Chinese, Ethiopians, and Pakistanis. There is no business that will continue run by these people; we are going to burn the malls, we don’t want them. We will burn the trucks, all foreign nationals’ shops, internet café, sewing areas, we don’t want them all. Let them relocate and we will deal with the police by killing them because they are shooting at South Africans, protecting the foreign nationals. Let the country be destroyed even in 1976 we died for it, sleeping in the forests to be insulted by these dogs. . If local churches are not supporting us on fighting this, we will kill them; there is no train, bus, flight that is going to work. Whoever we will find going to work will be we will kill even those walking on the streets if they are not in support of chasing the foreign nationals. As police are arming, we are also arming ourselves with weapons, those who will die, let it be. Let there be a smell of blood in the streets, perishing and the land of our forefathers being claimed back.

C&P
 
Chrismoris

JF-Expert Member
Oct 27, 2017
13,205
2,000
Wanachofanya mabalozi huko nje ni kutafuta wanachama wapya wa ccm watakakipa chama msaada wa pesa nyakati za uchaguzi.
 
imhotep

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
22,566
2,000
kama ni hivi, hizi balozi zitakuwa ni matumizi mabaya ya pesa za umma
Kuna kipindi tulizuiliwa Kigali tulikuwa kama Wabongo 40 hivi ilikuwa wakati wa Serikali ya Zamani ya Habyarimana tukaenda ubalozini hakuna msaada tuliopewa zaidi ya kusoma Magazeti ya Daily News na Uhuru tukaondoka mpaka Ubalozi wa Kenya.

Kilichonishangaza tulipokelewa na kusaidiwa na Maafsaa wa ubalozi walikuja mpaka Magerwaa kuja kushinikiza.

Mimi nilijiuliza maswali mengi sana kama ubalozi wetu unazubaa hivyo basi kuna haja Seminaa kwa hawa ma clueless wetu wenye suti nyeusi.
 
Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
5,669
2,000
Sasa wewe unafikiri nini kinawafanya washindwe kuwasafirisha watanzania waishio kwa madiba? Mtanzania yupo tayari kumkera mtanzania mwenzake kwa kumtetea raia wa kigeni. Usikute kiongozi hapo anatoa mrejesho kuwa watanzania wote wako mahali salama wakati jana kuna member humu ndani ameandika wapo katika hali hatarishi kiusalama na wamejificha mafichmi huko kuogopa kuuliwa.
Kwanza ufahamu kuwa balozi zetu huko nje zinapata fedha kiduchu sana! Ni mateso sana kuwa mtumishi wa balozi zetu kwani ukata ni mtindo mmoja. Hivyo ukipata matatizo usijisumbue kwenda ubalozini kwani kwenda kwako ni kuzidi kutonesha kidonda!

Serikali yetu inaona ufahari kufungua ofisi za kibalozi nje lakini huduma ni zero! Usitegemee waathirika wa fujo huko kwa Madiba kupata msaada wo wote wa kurudishwa nyumbani!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom