Kwa haya yanayoendelea katika siasa za Tanzania ilikuwa ni suala la muda tu

msomi kutoka znz

JF-Expert Member
Sep 18, 2017
599
2,677
Habari wana jamvi,

Haya ni maoni yangu, kwa yale yote yanaondelea ndani ya siasa za Bongo, niweke wazi mie sio mlengwa wa chama chochote bali mwananchi mwenye maoneleo fulani juu ya siasa.

Kwa yale yanayo zungumzwa na yanayoonekana, hata kama ingekua mwendazake tunae leo na pengine kwa miaka kadhaa mbeleni sidhani kama mambo kadha wa kadha yangeenda vile alivyotarajia. (N.B Mipango yote anapanga Mwenyezi).

sababu za maoni yangu zinafall kwenye uhalisia ufuatao.

1. Kushuka kwa Mapato ya ndani, pengine sisi ni watu wasahaulifu kidogo, unakumbuka makusanyo ya kwanza ya TRA ya mwendzake? yale yaliotokana na misamaha ya riba kwenye madeni? unakumbuka swala la Dodoma kuongoza kwa mapato? Je, trend iliendeleaje? kupungua kwa misaada kutoka kwa nchi wahisani, mashirika haya yote yangefanya mambo mengi ya mwendazake yakwame sababu kuu ikiwa alikua anategemea mapato ya ndani kama kimbilio la kupungua misaada. Je, tungeminywa ndani kwa ndani mpaka lini?

2. Fedha kwa ajili ya kuendeleza miradi, vipande vya SGR vilivyobaki, muendelezo wa flyovers, mwendokasi hili lilikua linaumiza vichwa ukizangatia mwendazake alitaka atuachie Watanzania legacy ya kuwa baba wa miundombinu, Tanzania aliyoiota aliitaka kwa namna yoyote of which it was a good thing, lakini shida ilikua angepata wapi pesa za muendelezo?

3. Manipulation of Numbers, ndege zetu ndo kama ivo tunaambiwa kuna manegative yamefunikwa, magawio hayo yaliokua yanatolewa achana na taasisi hio tu hizi zote na zile uchumi wa kati angeendelea kuzifanya/ kuzimaintain mpaka lini?

4. Msukumo kutoka kwa kundi la vijana wasio na ajira na wale walalamikaji wa kutokupandishwa madaraja..ilikua ni suala la muda na pengine ajenda ya mwendazake kuwepo kwenye kiti cha enzi kwa muda mrefu ingeleta changamoto kubwa kutoka kwa vijana wengi ambao ndio wangekuwa wapiga kura wake ambao pengine walikua na matumaini ya kupata ajira kwenye awamu yake ya pili ama nyingine kama angeongezewa muda.

5. Msukumo kutoka mataifa/diplomasia
Hali ya kidiplomasia ilishuka na pengine hii ilikua sabbu kwanini bakuli la misaada lilikua empty pia kwa kiasi flani (najua fika hakuna msaada wa bure *masharti), mwendazake alijiweka kama muweza wa yote mbele ya mataifa mengine na kutuma picha kuwa hahitaji external support, je angeweza kuhold for long?

6. Uwepo wa wateule walamba viatu, haikua ajabu kila mteule wa mwendazake nyimbo ilikua moja, sgr, barabara, ndege, soko etc.. over 6 years the same song, inachosha eh? tena yote ya mwendazake? je wao hawana mawazo mapya au mbadala? maboresho? Je, ingefaa sasa watoke wote tu wamuache mwendazake sababu yaonekana kila kitu ni yeye anafanya?

7. matukio ya chini kwa chini ya kutumia mabavu ie. task force, ama wateule wa mwendazake kuingia front kwa minajili ya kuamua kurekibisha mambo bila kufuata mifumo ya kawaida, pengine mwendazake alikua na muoneleo mzuri lakini hakujua wateule pia walikua wanatumia nafasi hii kunufaisha mifuko, wateule walimshajulia mzee tunamfanyaje ili nasi tupate yetu, matokeo ya muda mfupi yana akisi kufungwa kwa biashara kadha wa kadha.

8. Swala la Msiba wa KMK, na MW2 ZNz.
Walifariki wengi ila skuwahi kuona mwendazake akiwa mnyonge kama baada msiba wa KMK, unajua unaweza kua jemedari sana lakini kuna msiba unaweza kukutingisha mpaka ukomandoo wote ukakutoka, refer kwenye issue ya kibonde vs ruge, namanisha hata kama mwendazake angekuwepo sidhani kama mambo yangeenda sawa baada ya kumpoteza KMk wake

9. Kuporomoka kwa umoja na mshikamano wa Watz
kwa maana ya haya yanaoendlea sasa, chuki hutokea pale ambapo upande mmoja unakua treated unfarely na upande huo ukakosa muhimili wa kupata msaada, taratibu kaa cha chuki lilikua linawaka kadri siku za mwendazake za uhai. huyu kuwekwa ndani raha kwa wengine, huyu kufukzwa kazi raha kwa wengine. Tajiri akishushwa furaha kw wengine..taifa la kupenda hali mbaya, vitu vibaya, taifa la kutambiana sisi wa mavi-eite (v8) nyie wa mabonde maporomoko.

Hitimisho
Lala salama mwendazake, Mwenyezi Mungu akupunguzie adhabu kama vile tunavyoomba tupunguziwe sisi kwani sote si watimilifu lakini sote pia ni wa kurudi mavumbini, tunashukuru kwa yale mema uliotufanyia, umetupa uthubutu wa kuyaendea yale tunayoamini kama taifa.
 
Back
Top Bottom