Kwa haya madudu anayovumbua Waziri Silinde huko TAMISEMI ni kama vile Jafo hakuwepo Mitano iliyokwisha!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
41,773
2,000
Nimefuatilia ziara ya Naibu waziri Silinde wa Tamisemi na hasa mkoani Mtwara, kwa kweli madudu ni mengi sana.

Najiuliza tu mbona waziri Jafo alikuwa anatamba sana kwa kujenga madarasa na zahanati kwa kutumia fedha za ndani, kumbe zilikuwa mbwembwe tu.

Huyu Silinde akiendelea hivi na huu ujasiri bila shaka atakuwa waziri kamili soon.

Maendeleo hayana vyama!
 

Pilitoni

JF-Expert Member
Jul 11, 2011
1,167
1,500
Jafo ana hekima fulani hivi anajua kuna maisha baada ya uwaziri,sasa huyu wa kutumbua wakuu wa shule tu watu wenyewe wanyooonge, sijasikia ametumbua maafisa Elimu, maafisa Elimu ndio mafisadi wakuu kwenye miradi mingi ya shule hao wakuu wa shule ni mbuzi wa kafara tu.

Afisa Elimu ndio mtu wa mwisho kupitisha pesa,mkuu wa shule akivimba anaundiwa zengwe ananyang'anywa ukuu wa shule.Silinde anza na watu wa halmashauri hasa ma Deo acha kunyanyasa wakuu wa shule.
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
39,401
2,000
Ukitaka kucheka sasa subiri Magufuli atoke madarakani usikie rais ajaye atakavyokuta Madudu kwenye manunuzi ya ndege, SGR, SG nk. Usishangae na yeye kutekeleza miradi ya SG na SGR maana imejaa upigaji. Chain ya wezi haiwezi kuleta matokeo tofauti zaidi ya kujibadilisha rangi kama vinyonga.
 

ki2c

JF-Expert Member
Jan 17, 2016
2,949
2,000
Ngoja JPM atoke,mtaona kua nchi hii inaliwa hadi basi,ukienda kwenye suala la ujenzi,watu wanakula kinoma,utalii nako,ni shida.
Ngoja atoke akina Nape,January na wengine wateme nyongo.
 

Ng'wale

JF-Expert Member
Nov 24, 2011
3,134
2,000
Hiyo ni ndogo. Ngoja utakuja kuyasikia madudu ya jiwe siku akitoka.
Usishangae katiba ikaja kurekebishwa ili ashiuakiwe
Katiba inaundwa kwa misingi ya sheria. Sheria hairudi nyuma. Inaanzia pale ilipotungwa na katiba vivyo hivyo.
 

UmkhontoweSizwe

JF-Expert Member
Dec 19, 2008
4,510
2,000
Bwashee, hiyo itoshe kukuambia kwamba bongo tulikuwa tumejichimbia kwenye kufanya madudu. Kama rais, p/m, waziri, na naibu waziri wote wanaibua madudu, lakini bado kuna mengine yanabaki, ujue kuwa madudu yalikuwa yameota mizizi. Mwili wote ulikuwa umejaa majipu.
 

Ivan said

Member
Feb 14, 2021
28
75
Silinde Anza na maafisa elimu wanaojifanya miungu watu wa kunyanyasa walimu; unakuta mwl. anapeleka kwa mkurugenzi barua ya kuomba kuhama kutokana na matatizo ya kiafya yaliyothibitishwa na wataakam wa afya lkn afisa elimu anagoma kupitisha barua na badala yake anamwambia mwl. atafute mwl. wa kubadilishana nae! Ninyi maafisa elimu (miungu watu) hivi n sheria namba ngapi inayomtaka mwl. akitaka kuhama anatakiwa kutafuta mwl. wa kubadilishana nae? Ninyi maafisa elimu hasa wa mkoa wa Dar Es Salaam mnafahamu kuwa cheo ni dhamana na mnafahamu kuwa na ninyi ni walimu kama hao walimu mnaowanyanyasa? Ninyi maafisa elimu mnafikiri ninyi ndo wenye mamlaka ya mwisho ya kupitisha barua za walimu wanapotaka kuhama? Kama hamtaki kupitisha barua za walimu fahamu kuwa kuna ngazi inayofata na mnachotarajia kukipata hamtakipata.

Silinde anza na maafisa elimu acha kuwasumbua wakuu wa shule. Acha kuhangaika na dagaa wakati papa wapo!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom