Kwa haya bando za internet za mitandao ni kama kisa cha mashirika ya posta kupinga barua pepe kuwepo

chizcom

JF-Expert Member
Jul 31, 2016
7,581
15,718
Kampuni za simu zilikuwa zinaingiza mapato mazuri kipindi cha kizazi cha mawasiliano ya 1g,2g na ilipofika 3g baazi ya vifaa vingi na mifumo mingi ilikuwa hupokeo finyu.

Watu wengi tuliamini internet cafe kuliko simu janja ambazo sasa zimekuwa mwimba na kampuni za simu.

Kutokana na mapinduzi makubwa ya teknolojia ya mawasiliano ya internet na program nyingi kuboresha inafanya kampuni zinazo shikilia mawasiliano kutopendezwa na huduma ya internet kwa sababu watumiaji wengi umaliza matumizi yao sana kwenye app zinyingi za internet kama whatsapp,mitandao ya kijamii na mambo mengi.

Fikra hii sasa hipo dunia nzima kwenye mitandao ya simu sana.

Ili kuondoa jambo hili watu wengi wanatakiwa kujikita na huduma za ISP ambazo kazi zake zinatoa huduma za internet majumbani,makazini na sehemu nyengine kwa sababu huduma hizi ni unlimited,zinauza spidi na free ya bando.

Uzuri wa ISP wanajiusisha na internet na si swala la mawasiliano ya mitandao.

Hiki ndiko kitendawili ambacho mkifanya hivi lazima watarudi kwenu kuwa bembeleza na vifurushi au kubadilika kwa sababu mpinzani hawana kwa ajili ya simu janja zetu.
 
Back
Top Bottom