Kwa hatua hii ya JK tayari tumewekwa kwenye target ya Al Shabaab

Katika woooote wachangiaji, wewe ndiyo umesema cha maana. Hakuna conventional war hapo -- humuoni adui yako yuko wapi -- yuko nyuma, mbele au kati kati yenu.

Sawa tulipigana na majeshi Idi Amin kwa ujasiri na kuyashinda. Lakini laiti wakati ule Waganda wangeamua kufanya mambo ya ugaidi humu mwetu sijui ingekuwaje.

Hofu ya kujiingiza Somalia hasa kwa kauli ya wazi ya kiserikali itakuwa imetuweka tayari kwenye mapambano na maharamia hao. Swali ni je, tunao uwezo humu ndani kukabiliana nao endapo wataanza vitu vyao kama jinsi tayari wamefanya huko ndani ya Kenya? Hilo ndilo swali la msingi la kujiuliza -- na siyo maneneno maneno tu ya kishabiki.

Umenena.Hivi watu hawajiulizi kwa nini Wazungu wasiingie Somalia kwa kupeleka askari wa ardhini ili kupambana na hao maharamia? Wanachokifanya ni kuwatumia Wakenya (bila shaka serikali zao zinagharamia kampeni hiyo) kufanya vita kwa niaba yao, yaani proxy war.

Tusisahau kwamba hatua ya serikali ya Kenya kuingiza askari kule ilitokana na kutekwa kwa watalii wa Kizungu kutoka ardhi ya Kenya.

Sawa, ni wajibu wa serikali ya kila nchi kulinda raia wa kigeni walio ndani ya nchi zao, lakini lazima ulinzi huo uwe ndani ya mipaka. Wazungu wanaogopa kupeleka majeshi kwa sababu hiyo hiyo -- kwamba guerrila war ni ngumu kuimudu, kama vile Marekani ilivyojikuta Afghanistan, na sasa inatafuta njia ya kutokea kwa heshima.
 
ya



Kikwete: Tanzania backs Kenya's operation in Somalia

He said his country backed Kenya's decision to invoke Article 51 of the United Nations Charter to defend its economic and security interests under threat by the terror group.
Chanzo: Daily Nation

Mkuu sina shaka hapo nilipo weka nyekundu kunajieleza wazi wazi, sasa hapo Kiwete kakosea nini? Sasa kama jirani yako anatumia article 51 iliyowekwa na Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kulinda usalama wake, Jk amekiuka sheria gani ya kuanza kumsema sema - we anafikili yaliyo tokea Kenya hayawezi kutokea hapa simply by JK keeping mum - you are dead wrong.

Yeye kama RAISI wa nchi na jasiri hawezi kukaa kimya eti anawaogopa misguided Somalis, lazima nchi hizi za Africa mashariki zishirikiane kutokomeza kikundi hiki, hatuwezi ku-burry vichwa vyetu kwenye mchanga kama mbuni kwa kuamini eti kwa kuwa huyaoni yanayo endelea nchini za jirani zetu, basi kwa hilo tu sisi kama TANZANIA hayo hayawezi kutukuta!!!

Wakati mwingine huwa nashindwa kuelewa madhumuni ya threads nyingine humu ndani ya JF, nimeona kuna muelekeo fulani wa kujaribu ku-dramatise kila kitu akisemacho Kikwete, yaani watu wanajaribu kimaksudi kupotosha kauri zake, je hii inatusadia nini? Tuwe tunamkosoa pale inapobidi, hata yeye akitafakali anajiona kweli kateleza kweli na anajirekebisha - lakini haya mambo ya blanket critism yasiyo kuwa na kichwa wala miguu HAYATUFAHI.
 
Nyie nao bwana. kikwete akikiongelea kitu mjue hayuko serious. hapo tayari kaishamueleza Rage kwamba ni utani tu,
alilazimika kuongea hivyo sababu ndio lugha ya heads of state. Kwani waliompa elkopta mbili wakati wa kampeni ni kina nani?
 
Na halafu mbona pia hamzungumzii suala moja muhimu, kwamba kiongozi wa serikali ya mpito ya Somalia, Sheikh Shariff Ahmed naye alipinga kuingiliwa kijeshi kwa nchi yake?
 
Juzi BBC ilikuwa na mahojiano na mwakilishi mmoja wa kikundi kimoja cha waandishi wa habari nchini Kenya ambacho kilipinga hatua ya serikali yao kuipeleka majeshi Somalia. Kilisema kwamba serikali ya ya Kenya tangu 2007 iliufunga mpaka wake na Somalia na kusema inaweka ulinzi mkali dhidi ya maharamia wanaotoka Somalia.

Waandishi hao walihoji jee, serikali ilikuwa imeshindwa katika hilo? Pia walihoji na hayo majeshi yaliyopelekwa Somalia yanapata mafanikio gani katika kuwaangamiza maharamia wa AlShabab? Wasiwasi ni kwamba majeshi hayo yanaweza kuwa yanauwa Wasomali hovyo tu, hata wale wasiohusika na kuripoti kwamba wamewaua AlShabab, ili tu kuridhisha Wamarekani.

Hata huko Afghanistan, Wamarekani huuwa raia hovyo na kusema ni Taliban ili tu kuwatangazia ulimwengu kwamba wanawakabili adui vilivyo.
 
Angeweza kuwaunga mkono bila hata kuitangazia dunia, kwa hili tutegemee kichapo!
 
Angefika mbali zaidi na kutoa amri kuwa yeyote anaejiona ana pua ya kisomali aondoke nchini in 48 hours. Pia kenya wangefanya hivo.
 
Tanzania ilipashwa kulinda mipaka yake na siyo kuongelea swala la vita vya kenya. Kama tunataka kuunga mkono kenya ni lazima tuunge kupitia jumuia za kimataifa kama AU au UN. Hata approach ya Kenya is wrong in the very first placce. Kenya walipashwe walinde mipaka yao na watu wao pamoja na watalii kwa kuhakikisha maharamia hwavamii. Kitendo cha kweenda ndani ya somalia maanake wameenda kuungana na serikali ya mpito ya somalia kuwapiga Al shababu kitu ambacho kingefanywa kupitia jumuia za kimataifa kwa kutoa majeshi.
 
Huyo anataka tu ku-waplease Wamarekani, si kingine. Hivi angekaa kimya ingekuwa nini?

Hivi wenzetu huwa mnatumia kiungo gani kufikiri? Yaani wewe unaona jirani yako anashambuliwa halafu ukae kimya, kisa utakosolewa na wahuni kama nyie.
 
Wakuu, habari hii mnaionaje? Kwa hatua hiyo ya serikali yetu si kwamba sasa tumewekwa kwenye target, wenyewe wanaita 'crosshairs' za hao Al Shabab?

Tujadili implications ya hatua hii.

Nawasilisha.

_____________________

Kikwete: Tanzania backs Kenya's operation in Somalia



Tanzanian President Jakaya Kikwete has supported Kenya’s military offensive against Somalia militia Al-Shabaab.

He said his country backed Kenya's decision to invoke Article 51 of the United Nations Charter to defend its economic and security interests under threat by the terror group.

President Kikwete said Kenya is justified in taking action against the Islamic militants who have blatantly violated her territorial integrity through escalated cross-border raids.

He pledged his country’s commitment to support efforts by Kenya, IGAD, EAC, AU and the international community to stabilize Somalia and the Horn of Africa region.

The Tanzanian leader, who is in Perth, Western Australia for the Commonwealth Heads of Government Meeting (CHOGM) 2011, was speaking when he paid a courtesy call on President Kibaki Friday.

The meeting followed an earlier brief by President Kibaki to an executive session on Kenya’s military operation against Al-Shabaab to secure national security and economic interests.

During the session, President Kibaki maintained that Kenya was not at war with Somalia but is carrying out military action against the Islamic militia which is a non-state actor.

The Tanzanian leader, at the same time, joined other world leaders in calling for tougher action against piracy in the Indian Ocean, which continued to increase the costs of international trade and cause enormous harm to regional countries' fishing and tourist industries.

Chanzo: Daily Nation

Kiongozi ambaye hana uwezo wa kutoa tamko la kulaani kwa hofu ya kuwachukiza wahuni na magaidi huyo hafai kuwa kiongozi hata wa serikali ya mtaa. JK kaongea na hao washenzi waje tuwateketeze
 
We have started involving our nation in the so called Al shabaab staff...Soon TZ ll experience the spark disasters that we have never had b4. Our enemies re looking for the way 2get-in,this might be one of their target, the planned one, look what is happening in Northern Africa....watch-out guys.
JK mara nyingi ameonesha udhaifu katika uongozi wake LAKINI KATIKA HILI YUPO SAHIHI KABISA. Yaani mnataka Tanzania isiseme ukweli kwa sababu ya kuogopa kushambuliwa na magaidi wa Al Shabaab? Unaogopa kusema ukweli kwa sababu ya kuogopa? Huo ndiyo unafiki. JK iunge mkono Kenya ili kikundi hiki kipotee, kikiachwa kitakua na kustawi, na kuwa tishio kwa amani ya Afrika nzima. Hongera Kenya.
 
Kuna habari nyingi sana kwamba viongozi kadhaa kwene serikali yetu wamekuwa wakitaka kuwatumia hawa jamaa (Al-Shabaab) kuwanyonga wapigania haki wa nchii na taarifa zilishapelekwa kwa wana-usalama ambao hawakuchukua hatua tulizoziona, labda walichukua hatua za siri kama ambavyo walitaka kuwatumia kwa siri. Nahisi anachoongea JK ni kuidhihirishia jumuiya ya Kimataifa kwamba anapinga ubazazi wa Al-Shabaab, lakini huku nyuma ya pazia kama kawaida yake atakuwa anawasiliana nao na kuwaambia "msijali mimi napiga mdomo tu kuridhisha wapiga kelele"

Upande wa pili ni wa hatari sana, kama ni kweli JK anaongea tu kwa kuwa ndio dunia yote inavyosema... basi tuko kwenye hatari kubwa sana. Kwanza tukumbuke kwamba kabla haya hayajaja JK mwenyewe ameipamba sana dhana ya udini na imeshashika kasi vya kutosha, iwapo tu itatokea Al-Shabaab wakaamua kuja Tanzania basi tujue tutakuwa kwenye shida kubwa tena ya muda mrefu sana. Al-Shabaab wanafanya kazi kwa kutafuta wanachama wapya na kuwafunza kila inapowezekana, watapata wanachama wengi na kwa haraka sana hapa kwa sababu zifuatazo;
  • Udini ulioanzishwa na JK umeshashika kasi kiasi kwamba Waislamu wengi wanaweza kushawishika kirahisi sana kushambulia wakristo kwa sasa, hii ni kwasababu Al-Shabaab ni Waislam na hutumia ushawishi mkubwa wa dini kwenye vita yao siku zote.
  • Hali ya Watanzania Kifedha ni ngumu sana kwa sasa, ni rahisi kuwashawishi wote (Waislamu na Wakristo) kuingia Al-Shabaab kwa nguvu ya fedha na kujikuta tukilipuana wenyewe huenda hata Al-Shabaab wakiwa hawapo kwenye nchi hii.
  • Tayari kuna habari nyingi kwamba kuna viongozi walishakuwa na mawasiliano na hawa jamaa, kama ni kweli kuna uwezekano mkubwa hawa hawa viongozi wakatumia nafasi hiyo kuwafanyia kazi wabaya wao ama kuyashambulia makundi ambayo wangependa yaathirike zaidi na hali itakavyokuwa.
  • Al-Shabaab hawajikusanyi mahala ili muwashambulie, wao hujificha kisha hushambulia kwa kuvizia. Usalama wa Taifa wa wakati huo wa Mwl. ungefanya kazi, kwa sasa hakuna Usalama wa Taifa na kuwageuza wananchi watoe taarifa itachukua muda maana tayari polisi wameshawageuka wananchi kwa kuwa waonevu wakubwa kiasi kwamba wananchi wanaweza kufikia kuwaamini Al-Shabaab kuliko hata polisi wetu. Polisi jamii ni usanii usio na mashiko kwa sasa hivi, ni dhana nzuri isiyofanyiwa kazi kwa sasa. Ukitaka kujua katoe taarifa kwamba Mkubwa anaiba uone nini kitatokea, inaweza kutokea unaenda kutoa taarifa ya Al-Shabaab unashangaa unakuja kushikwa wewe. Siombei itokee hivyo ila najaribu kufikiria itakuwaje iwapo viongozi wetu wataingia kwene kutumia hali hiyo kufanya shughuli zao. Tukumbuke sasa hivi akina Uhuru Kenyata wanalaumiwa kwamba wakati huo waliwatumia Mungiki kufanya shughuli zao wakati wa hali iliyojitokeza Kenya baada ya uchaguzi ulioleta zahma kubwa hapo kwa majirani zetu. Sijasema ni kweli walitumia Mungiki lakini lisemwalo kama halipo basi lilikuwa linaelekea kutokea ama litatokea baadaye.
Hizi ni sababu chache ninazoziona zinaweza kuleta hatari kubwa, tujaribu kutafakari kwa upana wake. Nahisi ni bora vita kabisa kuliko kuwa na watu kama Al-Shabaab maana vita yao haiishi. Angalieni hapo Libya vita ya miezi kadhaa imeisha maana target zilikuwa zinaonekana, hapo Iraq ni miaka na vita haiishi imekuwa kama kidonda kisichopona maana jamaa si taifa fulani na hawana makao maalum, wanatumia popote penye nafasi kujijenga na hushambulia kwa mtindo huo huo. Kuendeleza vita ya Al-Shabaab ni kuendeleza vita isiyoisha, hawa Kenya wenyewe wameshasema kabisa kuwa wako tayari kukaa mezani na kuongea na Al-Shabaab. Kumbukeni Kenya wako uwanjani na wanakiona kinachotokea, sisi hatujui chochote tunaingia tu ushabiki wa kusema mara wapigwe.., wakija tutawapiga.., ooh Kenya songeni mbele.., mara JK sema tu hakuna tatizo na mambo mengine mengi. Hapa tulipo yawezekana tunao Al-Shabaab wengi tu wametulia kila mahali wanasubiri maelekezo, ninyi mnasema oooh uhamiaji watafunga mipaka...wapi??? Hakuna usalama hapa, tuwe makini na maneno yetu kabla hatujafikia kuongelea mambo kama haya.

Huyu jamaa aliyehukumiwa hapa Kenya juzi alifanya kwa shurti yake mwenyewe na ameikubali hukumu yake bila tatizo, mnajua tunao wangapi wa namna hii hapa Tanzania? Mnajua traffic ya watu wetu kwenda na kurudi Somalia, Pakistan, Afghanistan na kwingineko ikoje? Mnajua watanzania wanajifunza nini kwenye makanisa na misikiti yao?
 
Isije ikawa Kikwete kaamua kundandia issue ya Kenya vs Al-Shabab kama walivyofanya IGP Mwema na Kova mwishoni mwa wiki ili kuleta hali ya wasiwasi nchini,ambayo itasababisha wananchi wasahau matatizo ya yanayoikabili nchi kama DOWANS,hali ngumu ya kiuchumi. Ukichukulia so far issue ya AL-SHABAB imeshasaidia kutia kapuni maandamamo ya kupinga malipo ya DOWANS.
 
Kwenye hili nipo na JK 100%. Akiwa kama amiri jeshi mkuu wa majeshi ya Tanzania ni lazima aoneshe kuwa Tanzania inaendeshwa kwa principles na siyo kwa fears. Kama Al Shabaab wakitushambulia itakuwa jambo zuri zaidi maana na sisi tutakuwa na sababu ya kuwaunga mkono Kenya kwa vitendo. Sasa si sisi bali Alshabaab ndiyo wanapaswa kuogopa kuwa kwenye Target yetu. Wakijaribu kushambulia tu nitamuunga mkono Rais kuwafuata huko walikojificha na kuutokomeza ugaidi afrika mashariki.

Ukitawala kwa woga basi ujue wewe ni failed leader. unatakiwa kutawala kwa principles. Kazi mama ya rais ni kulinda nchi kutoka kwa wavamizi si kukandamiza wananchi wako. JK aache kuwaandama wapinzani na kutarget maandamano bali awa target hawa al shabaab. aache maamdano yaendelee kama kawaida na wananchi wakipigwa tu hiyo ni vita dhidi ya Alshabaab. Marekani kila siku huwa wanatishiwa kushambuliwa lakini sijasikia kuzua haki za wananchi kwa ajili ya kuogopa ugaidi bali inahakikisha kuwa inawalinda na ikitokea wakashambuliwa basi mshambuliaji atajuta. Tunaka na JK awe hivyo.
 
kiongozi wa al qaeda ni usama ms bin laden. kiongozi wa hezbola ni nasrallah, kiongozi wa taliban ni mullah omar, kiongozi wa green gadi ni al shabab. jeeeeee, kiongozi wa al shabaab ni nani?
 
Back
Top Bottom