Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 46,985
- 144,312
Ni wazi sasa watu wengi hawana tena imani na kiongozi huyu wa bunge na kwa maoni yangu ni bora akajiuzulu tu.Kwa hatua aliyofikia atakuwa na wakati mgumu kufanya maamuzi sahihi siku zijazo kuhusu mambo mbalimbali kama miongozo na mengineyo kwani kama anafuatilia maoni ya watu baada ya tukio la jana na mengine ya siku za nyuma ni wazi kwamba atakuwa hawezi tena kujiamini ktk kutoa maamuzi.
Athari ya kusemwa vibaya na watu pamoja na vyombo vya habari kiutendaji kama kiongozi ni muhusika kuanza kujiona na kuwaza kuwa kumbe mimi sifai ingawa hilo linakuwa kwenye nafsi yake ila athari kubwa ni kuathirika kisaikolojia na mwisho wake ni kujenga hofu na woga moyoni na hivyo kushindwa kumudu nafasi yako kama kiongozi kwani hutaweza tena kujiamini na utakuwa unafanya maamuzi kwa kujiuliza mara mbili mbili rohoni kwako na hivyo kuendelea kuharibu kabisa kama si kuboronga.
Kwa maoni yangu mh. huyu ni bora tu hata leo ajiuzulu huo uspika kwani hata akitoa maamuzi ya haki siku zijazo bado tu wengi watampinga kwasababu hii teyari iko kwenye vichwa vya watu na hivyo ataendelea kuona kama anasakamwa na hata kutokuwa na raha na wadhifa wake huo.
Raha na sifa nzuri kwa kiongozi ni kupendwa na watu ingawa si kila mtu atakupenda ila ni bora ukapendwa na wengi kuliko kuchukiwa na wengi kama kiongozi.