Kwa hasara ambayo huyu mtoto ameniingizia: Nashauri Sheria itungwe iwe ni shuruti watoto kusaidia Wazazi uzeeni

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,569
15,306
Ameangusha Laptop na kuua harddisk na kupoteza data zote. Nikaiweka mbali, amedandia na kukwea kabati na kuiangusha kupasua kioo slim laptop.

Amedumbukiza simu ya mama yake kwenye ndoo ya maji. Ameshapasua simu nyingine kama mbili (anavizia ukijisahau tu).

Amechana Macover ya vitabu vyangu na kuvichorachora. Ameiiburuza decoder kamaeigeza gari hadi sasa haifanyi kazi.

Kwa sababu anapenda game, amevizia tablet na kuibomoa kioo, sasa hivi ni nyufa tu. Kila noti anaiita Buku, Kakiiona Buku mahala hata kama ni msimbazi kanalilia kakiichoka ni kuichana.

Laptop mpya ilipokuja kaliivizia na kung'oa Herufi Mbili. Radio sasa kwa kulazimisha kuweka CD kameua Dvd reader, speaker kama mbili.

Ni mdogo miaka miwili kafikisha juzi tu, hata fimbo naona kama namuonea. Mazingira tumejaribu kuficha vitu na kuviweka mbali lakini kila siku anabuni njia za kuvifikia, na hasa ukijisahau.

Hivyo basi, naoendekeza Serikali itunge sheria ya kuwabana watoto kuwasaidia wazazi wao kuwa ni lazima hasa wanapochoka maana nao hutia hasara nyingi utotoni mwao.


Updates za ushauri
1: kumnunulia makorokoro yake mengi ya kuchezea.
2:kutafuta mbinu za kisaikolojia kumsaidia fimbo sio suluhisho zuri.
....
 
spade4spade,
mkuu mbona unakuwa nabii wa mabaya tena mkuu kama mwamposa. Nimepata kesi nyingi ya vitoto vya umri huu hata huyu anaafadhali maana anapenda vitu vya umeme mdogo zaidi (electronics) hivyo vingine vya hatari hata time navyo
 
Chai ya moto hii
hahaha sio chai, ni ukweli mkuu. kuna nyumba moja nilienda nikakuta vitu karibu vyote vimeninginizwa na kuwekwa kimo zaidi ya mtoto wa hapo, hasa vya jikoni.

watoto wa siku hizi ni wajuaji sana, tangu wadogo, usipojua hilo na jinsi ya kuwanandle unaweza kuwaua kwa stiki.
 
Back
Top Bottom