Kwa hali ya sasa na kwa kulitazama Bunge hili,unaaminni linaweza kuunda kamati teule kuuchunguza mhimili uliojichimbia?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,011
144,371
Najiuliza swali hili huku nikikumbuka kuwa kuanzia spika na wabunge wengi ,hasa wa chama tawala,wameshindwa kwenda kumuona Lissu aliekuwa amelazwa katika hospitali ya Nairobi n hini Kenya.

Sababu ya wao kutokwenda kumjulia hali mimi siilewi lakini hapo hapo napata swali kama kweli Bunge hili linaweza kuunda kamati ya namna hiyo.

Na hata kamati ya namna hiyo ikiundwa, kweli itakuwa huru kufanya kazi yake?

Yangu macho na masikio.

Naomba niishie hapa natumai nitakuwa nimeeleweka.
 
Muhimili uliojichimbia

Watu wasio julikana

Maagizo kutoka juu

Anaejua maana atwambie kwani sijawahi kuelewa kila ninaposikia kauli hizi
 
Salary slip wengine Tuko shamba na hatupati kujua kila linalotokea kwa wakati. Nini kimetokea? Mhimili uliojichimbia ni upi na nani ameahidi kuunda kamati; kamati ya kuchunguza nini? Yeyote anayehitaji zaidi aweza kuelezea zaidi hoja ya mleta mada ili wengi zaidi tuchangie!
 
Back
Top Bottom