Kwa hali ya Maisha ya Wabongo wengi, ukipatwa na kesi inayohitaji kulipa Faini ya TSH.500,000 wengi tutaishia jela

Opportunity Cost

JF-Expert Member
Dec 10, 2020
7,008
2,000
Directly kwenye mada.

Japo huwezi kusemea mfuko wa mtu ila huku mtaani maisha yetu tunajuana.

Leo hii mtu umepata tatizo kama kesi inayohitaji faini ya laki tano au kifuko cha mwaka nk Tulio wengi tutaishia jela maana hali ya vipato vya watu ni shida sana.

Hapa hakuna cha mtumishi wala nani maana watumishi wengi mapato yao ni chini ya laki tano hata saving hakuna,kwa dharura nani atachomoka?

Hata ukianxa kuwapigia washkaji wakupe 100k ukipata hata 1 shukuru.Yaani maisha yetu ni ya kudra za Mungu tuu ,tunaishi kwa kubahatisha.

Kila mtu akijitafakari kwamba pap anapata dharura ya pesa hiyo what next ? Huko benki watu Wana viakiba hata 50,000 havifiki , pengine angalau kwa wafanyabiashara wa Kati na wakubwa wanaweza kujimudu lakini sio kwa watumishi au mwenzangu na mimi.

Tujitahidi kuwa mabahili,kujinyima kiasi Ili tuweke akiba. Chukua hili utakuja kunishukuru.
 

RRONDO

JF-Expert Member
Jan 3, 2010
45,266
2,000
Wengi wetu tuna utamaduni wa kuchangiana, jitazame jinsi unavyoishi na watu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom