Kuna kundi kubwa sana la vijana wasiokuwa na ajira ama wako kwenye ajira zisizo rasmi na ajira za ujira mdogo. Hawa wote wanategemea siku moja kupata kazi zenye maslahi ya kuridhisha.
Kibaya zaidi kuna watu wameajiriwa serikalini na sekta binafsi lakini sio wote walio na malengo ya kustaafu wakiwa makazini.
Wapo wengi wenye malengo ya kuacha kazi ili wakaendeleze au kuanzisha miradi na biashara za ndoto yao, Changamoto ni sera zenu za mafao (fedha) ambazo ni jasho halali za hawa watumishi sio rafiki, jambo ambalo mtu akifikiria inabidi asitishe mpango wake na kuendelea kuwa kazini.
Hakuna ulazima wa kuzuia kumpa mtu pesa zake kisa ameacha kazi mwenyewe kwa maelezo kwamba atapewa akifikia umri wa miaka 55,, hizo pesa zitakuwa na faida gani tena katika maendeleo ya huyo mtu kwa umri huo? Kijana anaacha kazi ana miaka 35 akiwa ameitumikia hiyo kazi labda kwa miaka 12, asubiri mafao yake kwa miaka 20 zaidi?.Mliwaza nini hapa
Rudisheni fao la kujitoa, Vijana waliojichanga mitaji yao wakaendeleze biashara za ndoto zao na nyie kama serikali mpate nafasi nyingi za kuajiri wapya hata huko sekta binafsi kuna watu wanashindwa kuacha kazi kwa kuhofia kutopata pesa walizozitegemea kuendesha maisha yao nje ya ajira kwenye hii mifuko ya kijamii.
Viongozi wetu sijui mnawaza nini, kwa hali ilivo sasa ya changamoto ya ajira hizi sera zenu zingetakiwa ziwe rafiki kusaidia vijana kujiajiri zaidi ya kulazimisha walioko kwenye ajira wabaki hukohuko mpaka umri wa kustaafu.
Rudusheni hili fao, tuwapishe wengine waajiriwe nao watafute mitaji. Mnahimiza tujiajiri huku mnakatalia mitaji yetu ambayo ni pesa zetu halali, mko serious na mnachokihubiri kweli?