Kwa hali ilivyo sasa, ni wazi kabisa kuwa Paul Makonda atajiuzulu au atatenguliwa!

Kuna watu hawana vyeti na walikuwa wachapa kazi vzr tu offisini....kutokutolewa hapo alipo kisa uchapaji kazi sio sababu iyo....mtafutieni nyingine ...

Mkuu,

Nakubaliana na wewe kabisa kuhusu watu kuchapa kazi haswa bila ya kuwa na vyeti. Lakini hiyo ni tofauti na kuwa vyeti feki/kutumia vyeti vya mtu mwingine. Ndio maana pia hilo limewekwa katika makosa na adhabu yake ni kifungo.

Kaka ...
 
Mkuu,

Nakubaliana na wewe kabisa kuhusu watu kuchapa kazi haswa bila ya kuwa na vyeti. Lakini hiyo ni tofauti na kuwa vyeti feki/kutumia vyeti vya mtu mwingine. Ndio maana pia hilo limewekwa katika makosa na adhabu yake ni kifungo.

Kaka ...
Hujanielewa ...mm kamwe siwezi mtetea Bashite....Natamani hata leo akamatwe....
Nilichoandika hapo nilikuwa namjibu mtu aliyekuwa anasema Bashite afanya kazi nzr asitolewe...
Ndo nikawa nasema mbona kuna watu maofisini walikuwa wachapa kazi wazuri na walitolewa kisa vyeti....kwahiyo uchapaji kazi sio sababu ya kumfanya asitolewe madarakani labda wanao mtetea waje na sababu nyingine kaka...
 
Vita ya madawa ya kulevya ipo pale pale, waambieni madoni wenu wa madawa waliowatuma kupunguza makali wamefeli, tutapigana vita to our last breath


Bwana mdogo kosa la mwenzako haliwezi kukufanya na wewe utende kosa wala haliwezi kufuta kosa lingine. madawa ya kulevya ni kosa na kughushi vyeti vilevile ni kosa kwa hivyo yote ni makosa. kama wewe ni mzalendo tugawane majukumu wewe na wenzako mupambane na madawa sisi tuachie hili la vyeti tutalimudu. mwisho wa siku tutakuwa na tanzania safi usiyokuwa ya madawa na vyeti bandia. hatuwezi kushangilia wezi kupambana na wachawi na huku watakatifu tupo.
 
kesi ya kugushi vyeti ni miaka saba sijui kama atachomoka, kinachoniuma ni hawa polisi, PCCB, NECTA sijui wanasubiri nini? au hawajui wajibu wao?

labda turudi kwenye kauli ya Bashite kuwa 'katika ofisi yangu kuna watendaji 300 wanaofanya kazi ni wane tu'. na hao wane naona vilevile hawajui wajibu mpaka sasa hawajamkamata mharifu wa vyeti hiyo inamaanisha kuwa ndani ya mkoa wa Dar es salaam hakuna mtendaji hata mmoja wanakula mishahara bure.
 
Kwa kweli amedhalilisha sana watu, na mbaya zaidi amemkufuru Mungu. Muda sio mrefu Mungu wa kweli atamshusha tu. Yeye baada ya kujibu tuhuma zinazomkabili, anakimbia huku a kule na kudai anasakamwa kwasababu "anapambana na madawa ya kulevya." Nachelea kusema kwamba tuhuma zinazomkabili zingekuwa sio kweli angeshajitokeza asubuhi na mapema na vyeti vyake halali ili kuonyesha waandishi wa habari, na mjadala ungeisha, basi! Na yule Boss wake "msema kweli mpenzi wa Mungu" bado ame kaa kimnya tu, baada ya kuchukua hatua...nashangaaa ni upenzi wa Mungu gani huu unaleta upendeleo dhahiri kabisaaa!!
Hivi kigugumizi ndio stammering kwa kingeleza au?.... kama ndio hivyo, hivi ni ugonjwa au ulemavu? je kuna dawa ya huo u...?
 
Makonda usijali kuchukiwa na watu kwamanufaa yao, tunao kwitaji dar tupo wengi kuliko wanao kuchukia.
Sisi wazalendo hatuna ubaya na Jina. kinachotuuma na kugushi vyeti mbaya zaidi walimu wa chekechea wamefukuzwa kazi kwa kutokuwa na vyeti.
 
kwa siasa za hapa za ukada na kujuana ataendelea kuleta maajabu na matukio kila uchao na 2020 atapewa uwaziri mkuu
Mpigeni vita tu, Makonda wetu. Ila mjue hamtanusurika. Vita zidi ya ufisadi na madawa ya kulevya iko palepale!! Nasema hamtasalimika kamwe.
Makonda ni jembe sana. Hakuna tena
Yajegwa mawards tena ya ghoropha ambazo pesa zake si za budget ya ama serikali ama za manispaa.
Nani Tanzania hii anayeweza?
Anajenga Ofisi ya Sheh. Wetu Mkuu.
Anajenga viwanja vya kisasa vya michezo, vyote haviko kwanye budget.
Hivi huoni? Unafikiria unga ufusadi tu.
Makonda tunamuhitaji sanax200.
Hutitaki mizandiki
 
Haitoweza kutokea..
Kwanza japokuwa alikuwa kashatengeneza mazingira ya kugombea ubunge ni kwamba ndoto zake za kuingia bungenu zimeyoyoma...
Sifa za kugombea ubunge keshapoteza na hata akipitishwa haitakuwa rahis kuchaguliwa tena kutokana na hii kashfa!
Lakini pia ashukuru kama hiyo 2020 itamkuta uraiani, huyu mtu inabidi awekwe korokoroni!
kwa kosa gani?
 
Unajuwa katika maisha kuna njia nying sana za kupambana " kiukweli mi sion kosa la jamaa kama kweli alifanya ivyo kama tuhuma znavyoeleza " lakin kiupande mwingine jamaa ni shujaa kwa sababu alipambana mpka akahakikisha amepata njia ya kutokea maisha" kwa hiyo kila mtu ana njia yake ya kutokea maisha" issue sio vyeti hapa kwakwel tuwe wawazi tu issue ni kiti alichokalia watu kinawauma sana inamaana ni wivu na husuda tu za watu" wangapi wamefoji vyeti kwenhe makampun huko" wangapi wanatumia njia haramu za kutoka maisha watu wanawafanya misukule watoto wazazi na hata ndugu na jamaa hamuoni hao kama wanatenda dhambi" wangapi wanapesa haramu chafu katka nchii ni kwa nn awa jamaa kila cku mtu ukiingia tu kwenye mitanda kwa nni hamumuach jamaa bahat ya mwenzako usilalie mlango wazi ebu tujadilin mambo mengine kila cku jamaa tu kafanya hivi jafanya vile ## aaaaaaah mnaboa jamani mwachen jamaa wawatu
Ukisema watu wana husda na nafasi yake si kweli...mfano Mimi binafsi pamoja na wengine wengi tutakuwaje na husda kwa nafasi alonayo wakati uwezekano wa kuipata ni MDOGO sana au pengine haupo kabisa. Hapa walio wengi sana wanakerwa na MTU kuwa ama kutuhumiwa kuwa na vyeti vyenye utata halafu hataki kudhibitisha na bosi wake ambaye aliapa kutumbua yeyote mwenye vyeti bandia kakaa kimya huku watu wengine waliopatikana na kosa kama hilo waliondolewa bila kujali utendaji wao wala nafasi zao. Yeye kama mtumishi was umma anapaswa kuwajibika kwa tuhuma hizi. Habari ya kupambana na dawa za kulevya ni tofauti kwani wote tunaiunga mkono bora tu itumike njia ambayo haitaleta maswali wala lawama kama aliyokuwa anaitumia huyo Daudi Bashite ambapo ilionekana kama ya kujitafutia ujiko kwa rais pamoja na kuonyesha ubabe kwa watu wengine. MAKONDA (BASHITE) ONYESHA VYETI ACHA KUJIFICHA KATIKATI YA UWANJA UKIDHANI HUONEKANI....au kama mteuzi wako ameamua kukanyaga kauli zake mwenyewe ili akulinde basi tujulishwe ili tujuwe wazi kuwa hata rais wetu anapotoa kauli zinabagua baadhi ya watu...kwa maana hiyo imani yetu kwake itapungua kama si kwisha kabisa.
 
Back
Top Bottom