Kwa hali ilivyo sasa, familia, ukoo au kabila likiendelea kuwekeza kwenye elimu kwa lengo la kazi, basi mbeleni kuna anguko kubwa

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,026
Sote ni mashahidi wadau.

Zamani familia au ukoo au kabila likikazania elimu kwa lengo la kuoata mafanikio kupitia elimu njia ilikuwa imenyooka kabisa.

Kuna hata makabila fani akili za darasani ziliwabeba kweli na kurundikana kwenye vitengo kwasbababu walikuwa na vyeti na sifa.

Ila kwa hali hii inayoendelea sikuhizi shule zimerundikana vibaya mno hadi vijijini huko na elimu imerahisishwa, hadi kwenye vijiji ambavyo vilikuwa na hali duni utakuta sikuhizi kuna waliofaulu wengi tu (divisheni 1 hadi baadhi ya 4) kitu kinachofanya wawe na sifa za kujiendeleza vyuoni na hatimae kuwa na vyeti vya kupatia kazi.

Kwa hali hii sasa ni vyema kuwe na njia mbadala hususani biashara za watoto na wajukuu kurithi maana hivi vyeo sio vya kurithishana.

Kuna kabila naona huenda likapata anguko kubwa mno maana wao ni wao na elimu tu na kutegemea ajira, tofauti na wengine ambao wapo kote kote.
 
Aiseee...

But haya ni ya muda mfupi tu, acha watu wawekeze kwenye elimu ili tusije achwa nyuma na wengine.
 
Aiseee...

But haya ni ya muda mfupi tu, acha watu wawekeze kwenye elimu ili tusije achwa nyuma na wengine.
Kuachwa ni lazima, kama elimu zenyewe niza kisubir kuajiriwa, mtu akipata degree tu anaanza kuzunguka na mabaasha.

Sela za kupata organisation au company mpya ambazo zitatengeneza nafasi mpya za ajira, hakuna kabisa.
 
Sela ???
 
Elimu inahitajika zaidi sasa kuliko wakati wa nyuma. Suala ni elimu ya namna gani itolewe. Hii ya kumtayarisha mwanafunzi aajiriwe haifai kwa sasa
 
Huo mtazamo wako, siyo mbaya wengine tutaendelea kuwekeza kwa zaidi kwenye elimu ya vizazi vyetu..
 
Sote ni mashahidi wadau.

Zamani familia au ukoo au kabila likikazania elimu kwa lengo la kuoata mafanikio kupitia elimu njia ilikuwa imenyooka kabisa.

Kuna hata makabila fani akili za darasani ziliwabeba kweli na kurundikana kwenye vitengo kwasbababu walikuwa na vyeti na sifa.

Ila kwa hali hii inayoendelea sikuhizi shule zimerundikana vibaya mno hadi vijijini huko na elimu imerahisishwa, hadi kwenye vijiji ambavyo vilikuwa na hali duni utakuta sikuhizi kuna waliofaulu wengi tu (divisheni 1 hadi baadhi ya 4) kitu kinachofanya wawe na sifa za kujiendeleza vyuoni na hatimae kuwa na vyeti vya kupatia kazi.

Kwa hali hii sasa ni vyema kuwe na njia mbadala hususani biashara za watoto na wajukuu kurithi maana hivi vyeo sio vya kurithishana.

Kuna kabila naona huenda likapata anguko kubwa mno maana wao ni wao na elimu tu na kutegemea ajira, tofauti na wengine ambao wapo kote kote.
Aksante kwa maoni ila ninachokijua Mimi kuhusu neno "ELIMU" kinanambia bado nawewe hauna elimu juu ya neno "ELIMU" ambayo kwayo tunazalisha vitu kama circuits, color, mirror , security, seeds na vinginevyo vingi.... Ila wakoloni walitualibu akili nakutupandikiza ujinga wakuwa kwenye kiti cha kizunguuka eti ndio ELIMU. Educe inamaanisha finyanga, bumba, chonga, chomelea, Linda, Lima, simamia, fundisha.
 
Ujumbe uko clear. Ila kuelewa inahitaji elimu. Na hii maana yake elimu haiwezi kupoteza umuhimu wake ila inaweza kupoteza thamani yake kutegemea na aina ya elimu husika, malengo ya elimu hiyo na nyenzo zinazotumika kuipata elimu hiyo kwa kipindi husika (generation).

Dunia inakwenda kwa kasi ya ajabu. Hata haikupi muda wa kushangaa tu unayoyaona. Na mabadiliko yanayoendana na kasi hiyo ndio pamoja na hii unayoona sasa kuwa elimu inapoteza umuhimu, ukweli ni kuwa kinachopotea ni thamani (dependent variable) na sio umuhimu (independent variable). Tafsiri ya hii ni kuwa chochote kinachofanyika kwa weledi na ufanisi basi elimu juu ya jambo hilo inachukua nafasi kubwa. Fuatilia hata kilimo kinachfanyika kitaalam (kuelimu) utaona ninachosema hapa.
Hivyo kuwekeza kwenye elimu hakuwezi kupitwa na wakati lakini thamani na malengo ya elimu hiyo ndio inatakiwa yaangaliwe na kuwekewa sera nzuri na wezeshi hasa katika kusaidia mapinduzi na uhuru wa fikra. Kuajiriwa katika hali ya kawaida inatakiwa iendane na ujuzi (uwezo wa kuleta matokeo) na sio idadi ya A’s or GPA status. Hizi ni added advantage.

Ndio sababu hata reasoning ya maprofessor (wasomi) inakuwa questioned wanapokuwa sehemu ya kundi la watu wanaopitisha sheria mbovu na kandamizi na hawahoji chochote, kama hizi kodi kwenye miamala, usomi/elimu yao ni muhimu, lakini thamani (value yake hasa kwa jamii ikoje)
 
Back
Top Bottom