Kwa hali ilivyo CCM imechoka kuongoaza, sasa inatukomoa watanzania... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa hali ilivyo CCM imechoka kuongoaza, sasa inatukomoa watanzania...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by only83, Feb 22, 2012.

 1. only83

  only83 JF-Expert Member

  #1
  Feb 22, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  ....Matukio mengi yanayoendelea sasa hapa nchini yanaonyesha wazi kuwa CCM na watawala wake wamechoka,wanachokifanya sasa ni kutukomoa watanzania ili tuumie wakati wao wanapokufa taratibu.Ni kama mgonjwa wa UKIMWI ambaye anatambua kuwa atakufa na sasa anasambaza virusi kwa watu wengine ili kuwakomoa.Ona matukio haya;
  1. Mahuaji ya polisi kwa raia Mbeya na leo Songea,hivi ni nani aliyetoa hii amri ya jeshi kuua raia? Nani atalipa uhai wa watu hawa waliokuwa wakitegemewa na familia zao? Kama sio kutukomoa watanzania ni nini?
  2. Mikataba isiyokuwa na tija kwa taifa,inayotoa mwanya kwa wageni kuchimba madini yetu na kutuachia magofu na umaskini wa kutosha..kama sio kutukomo watanzania hii ni nini?
  3. Wezi wa mali ya umma wanapachiwa huru na kuendelea kutesa,na wengine kuanza kutafuta uhai wa wale wanaodhani ni vikwazo kwao bila kuchukuliwa hatua..hii maana yake nini kama sio kutukomoa watanzania? Leo nimesoma taarifa moja kwenye gazeti la habari leo kuwa sungusungu wamempiga mwizi wa kuku mpaka kumuua lakini wezi wa mabilioni ya hii nchi wanatesa na wengine wanatafuta hata uraisi..kama sio kutukomoa watanzania ni nini?
  4. Viongozi wetu kudharau mambo yanayogusa maisha yetu kwa ukaribu,angalia mgomo wa madaktari uliodumu kwa muda wa wiki moja na zaidi,lakini watawala wa CCM waliendelea kutoa kauli bungeni na kwingineko bila kuchukua hatua,na watu walikufa wao wakiendelea kusubiria safari za Appolo..Je kama hii sio kutukomoa maskini wa Tanzania maana yake nini?
  5. Viongozi na watawala wetu kuendelea kupishana kauli kwenye mambo muhimu yanayogusa maisha ya watanzania mfano Ikulu V/S pinda,Makinda V/S kashilila,Manumba V/S Mwakyembe na Sitta..nk..Je hii kama sio kutukomoa watanzania maana yake nini?
  Unaweza chambua mengi na kueleza namna ambavyo hii serikali ya CCM inatutesa na kutukomoa sisi maskini wa Tanzania.Ila siku yao inakuja na wala sio mbali.
   
 2. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #2
  Feb 22, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Wakati wa mageuzi ni sasa na kama si sasa ni sasa hivi!

  Hakuna lisilowezekana!
  Mabadiliko ni lazima!

  Hawawezi kutugeuzageuza kama ulavyo mtu samaki,Hatukubali hili!
   
Loading...