Kwa hali ilivyo CCM Bernard Membe ametudanganya hana ushawishi mkubwa ndani ya chama, hasira ya CCM ni juu ya wahamiaji.

Dam55

JF-Expert Member
Oct 8, 2015
5,592
11,830
Ni dhahiri mh Bernard Membe ametudanganya kuwa ana ushawishi mkubwa ndani CCM jambo ambalo sio kweli. Utulivu ulio ndani ya Chama unatia mashaka na kutufanya wengi tujiulize maswali hiki kinachoitwa team Membe ndani ya CCM kiko wapi? Au ni kwamba wamempuuza?

Mbona hatuoni mgawanyiko wa chama baada ya kufukuzwa Membe kama tulivyoaminishwa.

Ni dhahiri sasa kuwa Membe si chochote kwa CCM ila hasira ya wenye chama chao ni juu ya wahamiaji na kweli wamepewa somo kuwa CCM ina wenyewe.

My take. Uchaguzi huu ndio utakuwa mwepesi zaidi kwa CCM kuliko chaguzi zote zilizopita, upinzani umekuwa dhaufi mno.
 
Ngoja uchaguzi uishe kwanza ndio tutajua

Hakuna uchaguzi chini ya awamu hii, bali kuna maonyesho ya kipimo cha ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura. Mfano mrahisi ni kura za maoni za ccm, watu walikuwa wanapewa dakika 2-3 kunadi sera. Hizo dakika unaweza kunadi sera gani? Matokeo yake walioshinda wengi ni wale waliogawa rushwa. Mtu aliyepita kwa rushwa, ikifika wakati wa uchaguzi mkuu, mwenyekiti wake wa chama ataishia kutumia madaraka yake kulazimisha atangazwe mshindi. Hapo ndio nakuambia hakuna uchaguzi, bali maonyesho ya kipimo cha ujinga wa mtu mweusi.
 
Hiyo inafahamika wazi inawezekana hata mwenyewe analijua hilo lakini atafanya nini wakati hilo jambo limepangwa kuwa hivyo
 
Hakuna uchaguzi chini ya awamu hii, bali kuna maonyesho ya kipimo cha ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura. Mfano mrahisi ni kura za maoni za ccm, watu walikuwa wanapewa dakika 2-3 kunadi sera. Hizo dakika unaweza kunadi sera gani? Matokeo yake walioshinda wengi ni wale waliogawa rushwa. Mtu aliyepita kwa rushwa, ikifika wakati wa uchaguzi mkuu, mwenyekiti wake wa chama ataishia kutumia madaraka yake kulazimisha atangazwe mshindi. Hapo ndio nakuambia hakuna uchaguzi, bali maonyesho ya kipimo cha ujinga wa mtu mweusi.
Yani we ulitaka ile siku ya kupiga kura pale ndio watu wapewe muda wa kutosha wa kutoa sera mkuu? Inamaana wewe hujui mchakato unavyokuwa hadi kufika siku ya kupiga kura?
 
Yani we ulitaka ile siku ya kupiga kura pale ndio watu wapewe muda wa kutosha wa kutoa sera mkuu? Inamaana wewe hujui mchakato unavyokuwa hadi kufika siku ya kupiga kura?

Mchakato ulikuwaje boss, wagombea wengi wanalalamikia muda wa kujieleza. Na sisi mchakato tuliouna ni wa kutia nia, kisha muda mfupi wakachukua fomu. Hakukuwa na zaidi ya wiki mbili toka kuchukua fomu mpaka kura za maoni. Hizo sera walizitolea wapi mpaka wakaeleweka, kiasi kwamba siku ya kura ya maoni wapewe dakika 2? Wakati mwingine kutetea uhuni wa wazi, ni kufanya uonekane juha tu.
 
Similar Discussions

11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom