Darren2019
JF-Expert Member
- Nov 23, 2019
- 1,112
- 2,379
Nimebahatika kuzunguka hii nchi mikoa kadhaa, ukipita vijijini unakutana na makazi duni kabisa, kumechakaa, watu wamepauka vibaya. Pengine hata network ya simu hakuna, redio haishiki hata moja wakati tuna vituo vya redio zaidi ya 80, kuna sehemu usafiri ni mshike mshike, kuona tu barabara ya lami unalazmika kukodi pikipiki elfu 30, bado usafiri unaotumika ni pijo 504 za miaka ya 70, nimeshuhudia sehemu nyingi tu mikoa tofauti ukiwa na safari ya halmashauri basi uandae na pesa ya gesti maana gari ni moja tu na kurudi ni kesho yake.
Nimetizama taarifa ya habari ya ITV leo kuna watoto wanne wa familia moja wamekufa njaa huko Serengeti, Nafikiri Serikali inaangalia maisha ya Mtanzania kwa kuzingatia watu wa Dar pekee ukweli mikoani umasikini ni mkubwa mno.
Utajiri wa Tanzania uko wapi?
Sent using Jamii Forums mobile app