Kwa hali hii vyama vya upinzani havina nia ya kuja kuongoza nchi...Vijitathmini!

Keyboard Warrior

JF-Expert Member
Aug 5, 2014
989
1,000
Tukubali tukatae vyama vya upinzani awamu hii vimekuwa all talk and no action.

Wanasiasa na viongozi mbalimbali wa vyama vya upinzani wamekuwa watu wakulalama tu mtandaoni lakini hakuna hatua zozote wanazochukua kutokana na mambo wanayofanyiwa.

Ni kweli usiopingika kuwa katika kipindi hiki vyama vya upinzani vimekuwa vikichezewa rafu za kila aina, lakini hakuna kitu wamefanya, wanasiasa wamebaki kulialia na kulalama mtandaoni... sasa wananchi walalamike, halafu na wanasiasa waliowachagua walalamike tena, sasa nani atamsaidia mwenzake.

Kama vyama vya upinzani vingekuwa serious kweli basi tungeona haya yanafanyika, serikali ilipopiga marufuku mikutano ya siasa ambayo ni kinyume kabisa na katiba, tungeona hata vyama vya upinzani vikifungua kesi ya katiba kupiga hilo... lakini wapi, hakuna aliefanya hivyo.

Kwenye uchaguzi mdogo wa kata ulioisha hizi karibuni, vyama vya upinzani vimefanyiwa kila aina ya hujuma.. lakini mpaka sasa hatujasikia hata chama kimoja cha upinzani kikikata shauri mahakamani kupinga matokeo.

Tukubali tukatae, mahakamani ndo sehemu pekee vyama vya upinzani vinaweza vikawa na chance ya kupata haki zao. Kwasababu tumesikia mara kadhaa wapinzani wakishinda kesi za ubunge na udiwani mahakamani. So they have a chance there, lakini kama wakitegemea huruma za chama tawala watalia na kusaga meno.

Pia ni dhahiri bila mabadiliko ya kifumo na kisheria kwenye masuala ya uchaguzi, itakuwa ni ngumu kwa vyama vya upinzani kushinda au kutangazwa washindi kwenye chaguzi mbalimbali, lakini pamoja na malalamiko hayo, bado hakuna hata mwanasiasa mmoja wa upinzani aliethubutu kupeleka muswada binafsi bungeni, ili kuchochea kupatikana kwa tume na mfumo huru wa uchaguzi. Hata kama the odds zitakuwa against them, lakini hata kujaribu tu. Hakuna.

Sio siri CCM imechokwa ila vyama vya upinzani vina-disappoint kwa kutochukua hatua zozote na kuishia kulalamika tu kila siku. Inabidi vizinduke na kuanza kuchukua hatua mbalimbali za kisheria na sio kila siku kuitisha press conference tu na kutoa matamko halafu basi.

Wanasema insanity is doing the same thing and expecting different results. So its obvious approach ya sasa hivi ya vyama vya upinzani havifanyi kazi,kwa hiyo wajaribu njia nyingine.

Tunataka kusikia kesi mbalimbali za kikatiba na kisheria kupinga mambo yanayofanywa na serikali ya awamu hii, na hata kupeleka miswada bungeni kurekebisha kasoro za kimfumo na kisheria. Hata kama it wont work out ila wawe na uthubutu hata wakujaribu kufanya hayo. Hicho ndo wananchi wanataka kuona.
 

Bayyo

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,598
2,000
Wanakuja na hoja dhaifu eti wananunuliwa,,, badala ya kujichunguza wajikwaa wp wanatoa majibu mepesi kwenye maswali magumu. Hawa ndo vyama vya upinzani tz..
 

kauga JR

JF-Expert Member
Mar 4, 2015
3,513
2,000
we ndio unajua sasa toooo late.
Magu anapiga ngumi kama za tyson, wee unafikiri utapona.
 

binjo

JF-Expert Member
Feb 22, 2016
2,117
2,000
Mkuu upinzani wako imara.

Hao wavulana na wasichana wananunuliwa
 

Econometrician

JF-Expert Member
Oct 25, 2013
10,936
2,000
mkuu hata wewe ungekuwa kiongozi wa chama cha upinzani ungekuwa hivyo hivyo unaongea kwa vile hujavaa viatu hivyo huko mahakamani kote ni CCM kama ulimsikia juzi mbowe ameongelea swala hilo kwa kina sana.
na mbaya zaidi CCM wanatumia kivuli cha serikali na kodi za wananchi kudidimiza upinzania kwa njia yoyote ile wanayoona inafaa.
tatizo kubwa la nchi yetu wananchi wengi uelewa wa mambo ni mdogo-kiufupi ni wajinga na wachache wenye uelewa wa mambo werevu kidogo wamejaa umasikini hivyo kujikuta wanatanguliza matumbo yao kwanza.
kwanza upinzani wanajitahidi sana tena sana mazingira yao ya kazi ni magumu sana
 

kauga JR

JF-Expert Member
Mar 4, 2015
3,513
2,000
Mkuu upinzani wako imara.

Hao wavulana na wasichana wananunuliwa
Wananunuliwa????
Sikiliza ndg CDM ni saccos ya bwana Mbowe, watu wanaona mbali.
Wee unaakili gani yaani mtu anunue chama kizziima.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom