Kwa hali hii tutafika?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa hali hii tutafika??

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Comi, Jun 19, 2012.

 1. Comi

  Comi JF-Expert Member

  #1
  Jun 19, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 3,347
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 180
  Jana bungeni mh. Nasari aliuliza swali kuhusu serikali imeshachukua hatua gani kulingana na tangazo la mwaka 2009 kuwa porters wanatakiwa kulipwa dola 10 kwa siku badala ya sh.6000 na je serikali iimazichukulia hatua gani kampuni ambazo zimekaidi agizo hilo,baada ya serikali kutoa jibu mh. Nasari hakuwa ameridhika cha ajabu spika anamlazimisha nasari aulize swali lingine na mh. Nasari akaenda mbali sana kuwa majibu aliyonayo toka wizarani ni tofauti na majibu ya pale.

  Pili hivi ni lini serikali itaacha haya maneno:-
  Tuko kwenye makakati
  Tunasubiri maelekezo kutoka juu.
  Tunasubiri tume imalize uchunguzi.
  Tutaunda tume ya kufuatili n.k

  je tanzania kwa hali kama hiyo chini ya viongozi hawa mabadiliko yatakuja? Mh. Hamad alizungumzia swala la mmiliki wa mashine za madini,sitaki kwenda kiundani zaidi ila swali ni je, tanzania kuna ulinzi wa kutosha? Kama ndio huyu mbelgiji aliingiaje? Anafanyaje kazi?kibali chake kakipataje? N.k
  Je wanyama wanasafirishwaje?au intelgensia ni kwa ajili ya watu fulani wanaotaka kuweka ukweli hadharani?

  Tukija kwenye uzalendo.
  Baadhi ya Viongozi wa tanzania si wazalendo toka moyoni ila ni wataka sifa kwa mf. Katika uzalendo wa kweli ni lazima mzawa apewe kipaumbele ila kwa hapa mgeni anapewa kipaumbele zaidi. Mzawa ili apate TALA(kibali cha kampuni ya utalii) ni lazima alipe dola elfu mbili na pia lazima apeleke card za magari 5 ambayo yameandikishwa kwa jina kampuni, kwa mahesabu ya haraka ni zaidi ya mil.100, je mtanzania atamudu?
   
Loading...