Kwa hali hii ni kama CHADEMA hawajui wanachotaka

Maswali ya kipumbavu. Haya mimi ni mkristu, nikikosa kwenda kanisani jumapili ukristu wangu unakwisha??

Position yako na Mbowe katika TCD ni umbali wa dunia na jua. Hiyo hadhara ni kwa ajili yako, yeye kufahamu ajenda kama mmoja wa waanzilishi (wana katiba au taratibu za taasisi hiyo). Taasisi ya kisiasa inamwalika aliyehusika katika uchaguzi unaolalamikiwa kuwa mgeni rasmi ili taasisi imuombe mambo kadha wa kadha??!! Really??

Ni aina yako ya upumbavu ndio mambo yanayolitesa taifa hili. Hapa mbowe anatumia nguvu ya hoja kwa sababu hataki kutumia mabavu! Kukataa ni moja ya njia non-violent. Unashangaa kupingwa kwa mkutano huu lakini ni wewe hukukushangaa kupingwa kwa rasimu ya katiba ya Warioba. Ikatengenezwa nyingine ambayo imetupwa kapuni na mpaka sasa hujawahi kuuliza nini kitaipata!!! Kazi yako ni kulaumu wengine wanaochukua hatua usizoweza hata kuchukua.

Pathetic!!
Umejibu vyema sana wewe ni mkristo kutokwenda kwako kanisani hakukufanyi ukristo wako uishe lakini pia hakukufanyi kuwa tofauti na maazimio ya walioenda kanisani wakati wewe ukiwa na mambo yako.

Hivyo Chadema ni sehemu ya TCD hilo wamekiri uamuzi wa kuingia au kutoingia kwenye Vikao ni wao kwa kuwa ni haki yao.

Lakini uamuzi wa kupinga au kukana kile kilichofikiwa/kubaliwa katika Vikao walivyosusa haki hiyo hawana kwa kuwa wao ni sehemu ya uamuzi huo

Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app
 
Mantiki inanituma kuuliza kwanini kuna watu wanaogopa katiba mpya?

Kwanini mchakato ulianzishwa haujafika mwisho ukakatishwa?

Wakati ule mchakato umeanzishwa na Rais Kikwete kwanini hapakuwa na kundi la watu au mtu aliye pinga?

Hiyo katiba mpya ikipatikana itahusu kundi fulani au sisi sote?

Hofu ni nini hasa?

Ni kujisikia unyonge kukubali?

Ni kujua kabla hiyo katiba itakuaje?

Ni nini sasa?
Mchakato wa Katiba ulikwama kwenye hatua ya kwenda kupigiwa kura

Sasa tujiulize kwenye hatua hiyo tunapaswa kusimamiwa na Tume gani je ni hii hii au tuwe na tume huru kwanza?

Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app
 
Leo Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe amezungumza na waandishi wa habari na kuelezea maazimio ya kamati kuu.

Pia ametumia fursa hiyo kuelezea mazungumzo yake na Rais Samia,Pamoja na ushiriki wa Chama hicho katika kila hatua ya kuleta muafaka na maridhiano ya kitaifa.

Nami nimechukua maeneo haya.

Chadema wamesema wazi wao ni washiriki halali wa kituo Cha Demokrasia nchini wakiwa wanaingia humo kwa kuwa ni miongoni mwa waasisi wa kituo hicho.

Pili Mbowe akasema Kuna Vikao vineitishwa na TCD na wao hawatashiriki kwa kuwa agenda zilizopo hazisemi kama kutakuwa na uwezekano wa kupatikana katiba mpya.

Akaongeza kuwa wao wapo tayari kwa aina yoyote ya kutafuta njia ya kupata katiba mpya kwa maridhiano namikishindikana watachukua hatua nje ya maridhiano.

Hapa ni nini wanaongea?

Kwamba licha ya wao kuwa wanachama wa TCD Lakini pia kama chama kiongozi hawapo tayari kuhudhuria aina yoyote ya kutafuta muafaka na kitakachojadiliwa katika Vikao ambavyo wao wametangaza kususia basi hawatakiafiki kama wasivyoafiki Sasa

Kwamba hawataki nafasi ya kupeleka mapedekezo yao katika kikao hicho ili wabadilishe kile wasichokubaliana nacho sasa zaidi ya kusubiri hatua yao ya mwisho ya kuitafuta katika

Kwamba hawapo tayari kuona aina yoyote ya muafaka au maridhiano ya kisiasa yanafanyika licha ya wao kuwa chama Cha kisiasa chenye wajibu huo

Mwisho Chadema wanatuambia wao hawatahudhuria nahawatapeleka mapedekezo yao na yasipopitishwa Yale waliyo nayo mioyoni mwao basi wataenda kuitafuta katiba katika hatua yao waijuayo

Mimi wamenichanganya na sijui wanataka nini
 
Back
Top Bottom