Kwa hali hii, ni dalili ya CCM kupoteza uhalali wa kutawala | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa hali hii, ni dalili ya CCM kupoteza uhalali wa kutawala

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kibona Dickson, Mar 3, 2011.

 1. Kibona Dickson

  Kibona Dickson Member

  #1
  Mar 3, 2011
  Joined: Feb 13, 2011
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kauli,lawama na hofu, vilivyoshehen katika hotuba ya februari 28,ya rais Kikwete ambaye pia ni mwenyekit wa chama tawala CCM na kufuatiwa na kukamatwa kwa kiongozi wa mkuu wa CHADEMA pamoja na baadhi ya wanachama ni ishara ya kwamba vyombo vya dola tayari vimepokea amri ya kuanza kuwakandamiza wapinzani hasa CHADEMA.
  Haiwezekani kabisa,rais akatumia mda mrefu kukilaumu chama kikuu cha upinzani halafu kesho yake wapinzani wakatwe na kuhojiwa kwasababu za kughushi eti"UCHOCHEZI"hata ile hotuba ya kuwalaumu CHADEMA kwa kisingizio cha usalama wa Taifa inaonesha wazi kuwa ni hila ya kutafuta uhalali wa kuyazima maandamano na mikutano ya chadema,vinavyoendelea kufanyika hivi sasa kanda ya ziwa na baadaye nchi nzima.
  Kikwete na chama chake cha CCM,wametambua jambo moja.Utambuzi wao unatokana na uzoefu wa uchaguzi mkuu na matukio baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana.CCM na Kikwete wametambua kwamba kuna kila dalili ya kupoteza uhalali wa kutawala Tanzania siku za usoni.
  Wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu za mwaka jana,CHADEMAi ilitoa changamoto kubwa haijawahi tokea tangu kurejewa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 hapa Tanzania.CC waliokolewa na Uchakachuaji wa kura za urais,ubunge na udiwani.CCM mpaka walishinda kwa kutegemea uchakachuaji,walijua nguvu ya CHADEMA,kwamba kushindwa kwao kihali haiwezekani.Hi ni dalili ya kuanza kupoteza uhalali wa kutawala tanzania.
  Baada ya uchaguzi kumalizika,nguvu ya CHADEMA,iliendelea na mpaka sasa inaendelea kulitikisa bunge la kumi.CCM wakaendeleza hila zao,wakaichakachua CHADEMA kwa kushirikiana na vyama vidogo vya upinzani.Kanuni za bunge zilikabadilishwa kwasababu ya kuogopa nguvu ya CHADEMA.Kwa CCM kutegemea kuendelea kutawala nchi kwa kufanya ujanja ujanja wa mabadliko ya sheria na kupachika pachika vifungu vya sheria ni dalili ya kuanza kuaga na kuondoka kwenye enzi za utawala,ujanja ujanja una mwisho.
  Hata kule kuwakamata wapinzani CCM inaona kama kuwatisha ni mbinu muafaka ya kuwafanya waache harakati zao. wakolon wa kiingereza walifanya hivyo kwa viongozi wakuu wa TANU wakaishia kufunga vilango na kwenda makwao.Makaburu wa Afrika ya Kusini waliwakandamiza wapinzani wao wa kiafrika,baadae wakaishia kuondoka madarakan.
  UKIONA CHAMA TAWALA KINALIALIA DHIDI YA UPINZANI,KINALAUMU UPINZANI BILA SABABU NA KUKANDAMIZA UPINZANI BILA SABABU KWA SABABU TUU UPINZANI UNAANZA KUINGWA MKONO NA SEHEM KUBWA YA UMMA,JUA NI MWANZO WAKE WA KUPOTEZA UHALI WA KUTAWALA.NDIVYO INAVYOTOKEA KWA CCM HIVI SASA.
   
 2. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #2
  Mar 3, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Sisiem ilishapoteza uhalili kwenye sanduku la kura leo wapo hapo kwa sababu ndiyo utamaduni wa viongozi wengi wa Afrika, Mugabe, Kibaki, Gbagbo na Jeikei
   
Loading...