Kwa hali hii mishikaki itaisha?

mende 2014

JF-Expert Member
Apr 13, 2014
763
131
Wadau wenzangu sheria inasema kuwa waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda wasibebe mishikaki na badala yake wabebe abiria mmoja lakini naona kama sheria hii haisimamiwi vizuri na wahusika kama ilivyoaagizwa.
Mfano angalia huyu hapa,.
b4ea4a56a2a00d780a9b228c91acb96c.jpg
 
Kuna wenzao walipandishwa kizimbani huku TEMEKE kwa ajili ya kubeba mishikaki na kutovaa helmet
 
Daaah mi nikajua mshkaki mshkaki...... hehehehhe. Ila mshkaki ya kule karibu na ledger plaza bahari beach hotel mitamuu. ..... nitaiibukia mwezi wa nane nikiwa off.
Uwe makini na hiyo mishikaki unayoipenda na uichunguze vizuri kama inatokana na wanyama ambao huwa unakula au wale ambao huwa hauli.Utakuja kujuta ukikuta matokeo ni tofauti na taswira ya wanyama uliyojijengea kichwani ni tofauti na wale wanyama ambao ulikua unafikiria kua ndio chanzo cha hiyo mishikaki yako pendwa.
 
Hapo Nyamongo.. kuna mtu kachonga nyuma ya boda hapo... GONGO hatari sana.. huyo kanyooka si mchezo..!!
 
Daaah mi nikajua mshkaki mshkaki...... hehehehhe. Ila mshkaki ya kule karibu na ledger plaza bahari beach hotel mitamuu. ..... nitaiibukia mwezi wa nane nikiwa off.
Ni mitamu kutokana na nature ya mnyama. Ile nyama hata uiunge na chloroquine bado itakuwa tamu tuu. Pole kwa ambao hawaitumii.
 
Hahahahahahaa umeipata eeehh mshkaki ile mitamu balaa...... shurtu mate kuntoka hapa..... mdomo ushalowa kwa kuikumbuka tuu.....:p

Nami nazidi kuwapa pole ambao hawaitumii hehehh
 
Uwe makini na hiyo mishikaki unayoipenda na uichunguze vizuri kama inatokana na wanyama ambao huwa unakula au wale ambao huwa hauli.Utakuja kujuta ukikuta matokeo ni tofauti na taswira ya wanyama uliyojijengea kichwani ni tofauti na wale wanyama ambao ulikua unafikiria kua ndio chanzo cha hiyo mishikaki yako pendwa.

Weye wala nyama ipi? .....
Ya bata....?
Ya kuku....?
Ya ng'ombe....?
Ya porini. ...?

Halafu nyama ikishatungwa mshkaki utamu wake unazidi ule wa nyama ya mchuzi.......

Kasie.
 
naona topic imeshageuka tayari na kuwa ya mishkaki ya nyama.kuna anga nilikatiza,nikaona jamaa anachoma mishkaki ya utumbo wa kuku! hawatupi kitu. all in all,mshkaki ya nyama ya watu wa jumapili na baadhi ya wa ijumaa(maana nawafahamu wachache wanaoitafuna) ni mitamu sana!
 
Wadau wenzangu sheria inasema kuwa waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda wasibebe mishikaki na badala yake wabebe abiria mmoja lakini naona kama sheria hii haisimamiwi vizuri na wahusika kama ilivyoaagizwa.
Mfano angalia huyu hapa,.
b4ea4a56a2a00d780a9b228c91acb96c.jpg
1467997608935.jpg
na Kuna bike naionaga Inabeba watoto km 7wa shule
 
Weye wala nyama ipi? .....
Ya bata....?
Ya kuku....?
Ya ng'ombe....?
Ya porini. ...?

Halafu nyama ikishatungwa mshkaki utamu wake unazidi ule wa nyama ya mchuzi.......

Kasie.
Huwa nakula nyama yoyote miongoni mwa hizo zilizoorodheshwa,lakini niwe nina uhakika kua nyama ninayokula ni nyama inayotokana na wanyama wanaotoa hizo nyama ulizoorodhesha.Sili nyama hovyohovyo kwasababu ya matukio mbalimbali ambayo nimewahikuona yanayohusu uuzwaji wa nyama ambazo huwa sili mathalani MBWA,PAKA et al. kwahiyo kua makini.
 
Asante kwa angalizo
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom