kwa hali hii Kikwete ataendelea kuwa Rais baada ya 2015

scramble

JF-Expert Member
Nov 29, 2012
1,593
256
Utangulizi
tumo katika kipindi cha kupitia rasimu ya katiba ya muungano. ni bahati mbaya kuona katiba ya muungano inatangulia ile ya tanganyika au tanzania bara! hali hii itasababisha katiba ya muungano kuiburuza ile ya tanganyika. kwa upande wangu kosa limefanyika. tulikua tuanze na katiba ya tanganyika, pamoja na ile ya zanzibar kisha tujadili mambo ya muungano. nionavyo mimi rasimu hii ya katiba ya muungano kwa asilimia kubwa, ndiyo katiba ya tanganyika. katiba ya muungano ya mambo 7 au 22 haiwezi kuwa na ibara zaidi ya 200! watanzania tunaelekea wapi! mbona tumefunikwa macho!

serikali ipi itakua na nguvu? ya tanganyika, ya znz au ya muungano? kwa hali ilivyo, naona rasimu hii bado inatupeleka kwenye serikali mbili. kitakua kiroja kwenda kwenye kura ya maoni ya katiba ya muungano,kabla hatujapitisha katiba ya tanganyika! lazima katiba mbili za znz na tanganyika ziridhiwe ndiyo tukubaliane kuhusu mambo ya muungano. hayo ndiyo maoni yangu.

nini kitamfanya JK aendelee hadi baada ya 2015?
suala la katiba siyo dogo. katiba inahitaji utulivu. tukiweka papara, tutaliangamiza taifa na tutaathiri vizazi vijavyo. baada ya mabaraza ya katiba kumaliza kazi yake, tutakwenda kwenye hatua ya bunge la katiba. hapo siasa itapamba moto sana na vurugu huenda zitakuepo. baada ya bunge la katiba kutakua na kura ya maoni. kabla ya kura ya maoni kutakua na kampeni za hapa na pale. udini utapamba moto. ukizingatia kuwa katiba za kujadiliwa ni 3 (ya znz, tanganyika na muungano) kimbembe kitakua kikubwa. siyo mtabiri lkn hali halisi inaonesha kuwa Kikwete ataongezewa muda huku tukiweka sawa mambo ya katiba. nadhani ni heri kumuongezea kikwete muda (nimeweka siasa kando na kutanguliza uzalendo) ili tupate katiba inayofaa kuliko kuharakisha na kupata katiba yenye mapungufu.

naomba michango yenye tafakuri ya kina na siyo ushabiki wa kisiasa!
nawasilisha!
 
kwani kuongeza kuna gharama??? wewe muongezee hautadaiwa kukwepa kodi kama MESSI.Urais ni swala la kifamilia iweje utuulize sisi???
 
Na cha kushangaza anayesimami hii katiba mpya ni jai mstaafu pamoja na wakongwe wenzake waliobobea katika mambo ya utawala na siasa. Hii Tanzania sijuwi tunakwenda wapi jamani?
 
Back
Top Bottom