Kwa hali hii inayoendelea leo bungeni: Je Ngeleja atapona?

Esoterica

Member
Jun 18, 2011
48
11
Wakuu,

Ninaangalia mijadala ya leo bungeni tangu saa 3 asubuhi. Wabunge wengi waliochangia hotuba ya Ngeleja leo wamesema hawaungi mkono hoja; wamo Mh Naomi Kaihula, Dr Kigwangala, Shelukindo, Bulaya, Sendeka, Nasor, nk..

Vilevile kutokana na hali hii Mh Lukuvi nimemuona akihaha toka eneo moja hadi jingine kufanya mijadala na watu mbali mbali. Alianza kwa kuteta na Mh Adam Malima pamoja na Ghasia, kisha akahamia ktk eneo jingine na kuteta na kina Sendeka pia nikamuona Mh Diana Kilolo akimuacha swahiba na jirani yake EL na kwenda kuteta na Mh J Makamba huku akiwa amechuchumaa. Hatimaye Mh Pinda aliteta kwa hisia kali na Mh Wasira (Mzee wa Kusinzia).

Ninahisi vikao hivi visivyo rasmi na mashinikizo ya wabunge yanaonyesha hali si shwari. Pia Mchana huu kuna vikao vya ki-chama vya CCM na CDM ninafikiri vina lengo la kuweka misimamo ya kichama.

Je Ngeleja na serikali itapona leo?

Wakuu ninaomba kuwasilisha.................................
 
Pengine niulize nini madhara ya bajeti kupigwa chini kama inavyoelekea kwa ngeleja?
 
Sasa hivi wako kwenye kikao kwenye ukumbi wa Msekwa.Inabidi huko ndani kuwa na hot debate hadi wakitoka na maazimio ya party caucas wawae comfused.

Kwa vyovyote vile wanahaha kumnusuru leo,spika anweza kabisa kubadilisha mkakati wa wachangiaji
 
So far wapo kwenye kikao, bila shaka watakubaliana tu kwamba waunge mkono hoja. Hakuna kipya kutoka CCM. Lakini kama seriously bunge likakataa kupitisha baje what will happen? Si atarudi tu kuandaa upya na kuiwasilisha upya? Au wabunge watapiga kura ya kutokuwa na imani na rais?
 
Nionavyo kuna makundi mawili ndani ya CCM yanapambana ( huenda ni kundi la Sitta na la Lowasa), au chadema wamefanya lobbying ya kuwashawishi baadhi ya wabunge wa CCM au ni nafsi zinawasuta, natamani iendelee hivyo hivyo ili bajeti isipite.
 
Ngoja tusubiri kikao cha saa 11.00 jioni tuone itakuwaje. Sasa hivi wamepelekwa kwenye mapochopocho yawezekana ni agizo kutoka White House a.k.a Black House iliyoko Magogoni.
 
mm naombea isipite, wabunge fanyeni maamuzi magumu! Tumechoka na huu mserekali wa kifisadi. Aaaaarrrgggghhhhh
 
wa TZ nawashangaa sana, km mnategemea zuri toka ccm basi umaskini wetu tutakufa nao! ccm wapo kwa ajiri ya maslahi yao na si yenu wananchi. wakitoka huko kwenye kikao utaona wote wataunga mkono hoja. km mbunge anasimama na kusema eti km umeme hautapatika mpaka mwakani yeye hataunga hoja MWAKANI, lkn hoja hii anaiunga mkono, ss mbunge kn huyu ana msaada wowote kwetu?
 
Ikiwa kama Bajeti hii ya Nishati na Madini itapita leo, basi waheshimiwa Wabunge, wajue kuwa historia itawahukumu kwa kutetea mambo na maslahi ambayo si ya Kitaifa ila ni ya kundi fulani.

Kuwakumbusha kidogo tu, ni kwamba Rais aliyetolewa kwa nguvu za umma, Mubarak wa Misri, anatakiwa kusimama kizimbani mwezi ujao, kwa kutoa maamuzi ambayo hayakuwa kwa maslahi ya Wananchi, bali kwa kikundi cha watu wachache wakati wa utawala wake.

Bunge, tuonyesheni kuwa sasa mmekomaa.
 
Mkakati wanaokuja nao kutoka msekwa hall ni kama wa matumizi ya viagra! zimzmoto as usual
 
Tusubiri tuone,lakini kwa hali ilivyo itakuwa ni aibu nyingine kwa MP's wa Magamba kama watakubali kuipitisha bajeti hii.
 
Pengine niulize nini madhara ya bajeti kupigwa chini kama inavyoelekea kwa ngeleja?

Madhara ya kupigwa chini bajeti ya serikali yapo katika Ibara ya 90(2)(b) nanukuu:

90(2) 'Rais hatakuwa na uwezo wa kulivunja Bunge wakati wowote, isipokuwa tu: -
(a) ...
(b) Kama Bunge limekataa kupitisha bajeti iliyopendekezwa na Serikali'.

Kutokana na matakwa ya kikatiba hapo juu endapo bajeti ya Serikali haitapita leo, basi Rais anayo mamlaka ya kulivunja Bunge na kuitisha Uchaguzi Mkuu. Kwa hali ya kisiasa ilivyo hata Wapinzani hawatakuwa tayari kuruhusu Bunge livunjwe halafu wakatoboke kuhonga wapiga kura tena; CCM wao tayari walishaanza kuunga mkono hoja hata kabla ya kuchangia (Rejea mchango wa mbunge wa Kwimba).

Bila shaka Ngeleja atapeta tu bila wasiwasi wowote.
 
Mkuu,

Hili ndilo linalotugharimu.Wacha livunjwe tuingie kwenye uchaguzi mpya
 
nimekupata vzuri ndugu yangu matale makoye lkn pamoja na hayo wakati mwingine vema kustand firm kwa kutoipitisha bajeti hii maadamu imeonekana kutokuwa na umakini wowote, ningetamani iandikwe historia by the way pamoja na hofu ya both parties "kutoboka mifuko" kwa kampeni naamini ccm ndo watakuwa na hali mbaya zaidi. ngoja tusubiri na kuona jioni
 
Back
Top Bottom