Tamu chungu
Member
- Dec 20, 2015
- 85
- 64
Kwa nilichokiona leo kwwnye mabasi ya mwendokasi nadhani ni bora daladala ziendelee kufanya kazi ili abiria uweze kuamua kama kupanda daladala au kupanda mabasi yanayoitwa ya mwendokasi.
Leo nimeenda kwenye kituo cha mabasi ya mwendokasi kukata tiketi nikitegemea kwamba nitapewa tiketi ya Tshs 800 itakayoniwezesha kufika mbezi kwamaana ya kwamba nije na basi hadi kimara kisha nishuke nipande lingine litakalonifikisha hadi mbezi lakini hali ilikua tofauti kwani mkatisha tiketi aliniambia kwamba mabasi yote yanaishia kimara na nauli ni Tshs 650.
Nililipa ile nauli ya 650 nikitegemea kwamba nikifika kimara basi nitalipa 400 nyingine ili nifike hadi mbezi ambapo jumla kuu itakua Tshs 1050.Chakushangaza hata nilipofika kimara nilimuuliza muhudumu hayo mabasi ya mbezi yapo wapi akaniambia sidhani kama muda huu yashaanza kufanya kazi na muda huo ilikua ni saa tisa alasiri.
Sasa hapa najiuliza kitu kimoja kwamba nikweli haya mabasi yana mlengo wa kuwatatulia abiria shida ya usafiri au yapo kibiashara zaidi.Nasema hivyo kwasababu gharama ya kutoka mbezi hadi kariakoo au posta inagharimu Tshs 1050 kwa mabasi haya kitu ambacho ni tofauti tulivyozoea kwamba daladala unalipa Tshs 600 unafika mpaka posta au kariakoo.
Mimi nafikiri kuba haja ya daladala kuendelea kufanya kazi ili abiria ndio aamue kama kupanda mwendokasi au daladala.
Asante.