MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,970
Nadhani sasa ni wakati wa kuwapa watu wa aina ya Lema na LISSU Chama wafanye kazi, hawa sio watu wa mchezo, ni wapinzani wasiorudi nyuma,ni wapinzani wa kweli, wana makesi kibao ya uchochezi mahakamani.
Hawa wanaweza kuleta amsha amsha ya vijana wanamabadiliko nchini,wanayo hamasa ya kutosha katika jamii. Mambo ya kusubiri jambo kwa kuweka mikoni mifukoni hawa makamanda wawili hawana hiyo tabia.
Historia inaonesha kua katika nchi hasa za kuafrika walioleta mabadiliko ndani ya mataifa yao ni wapinzani wasiokata tamaa,waliojitoa muhanga kwa ajili ya kuwatetea wanyonge, wasiorudi nyuma, wengi wamesota sana jela.
Huwezi kua kiongozi mwanamabadiliko kutoka upinzani huijui mahabusu, huijui mahakama, hujui virungu vya polisi wala misukosuko mingi katika maisha yako ya siasa. Tusidanganyane eti watu tunafanya siasa za kisayansi, hiyo haipo Afrika na haiwezi kuwa kwa sababu ustaarabu huo hatuna! Wameweza wazungu peke yao.
Kuendelea kujipa moyo unafanya siasa za kusayansi huku unamchekelea mpinzani wako utaishia kulalamika katika maisha yako yote na hutakaa ufanikiwe.Yakumbukeni mambo ya Uchaguzi mkuu Zanzibar, walimsusia adui uchaguzi nae akachekelea akamaliza.