Kwa great thinkers tu

Mwalimu Nyerere ni moja wa waasisi wa Afrika, aliiona Afrika ikiwa katika umasikini mkubwa kuliko huu wa leo hii. Ni kwa sababu nguvu za imperialism ni kubwa sana ndio maana ikabidi asalimu amri, nguvu za unyama wa kibepari ni kubwa sana kuliko uwezo wa ushawishi wa viongozi wa mwanzo wa Afrika.

Viongozi waliokuja baada yake, kama mwenyewe alivyosema kwenye hiyo clip, ni waoga, hawana ujasiri wa kuwasilisha yale wanayoyaamini, wanapokuwa wamezungukwa na wazungu.

Rais mstaafu mmojawapo ambaye amekwenda nje ya nchi zaidi ya mara 400 katika miaka yake kumi ni mfano tu wa viongozi ambao hawawezi kuwa na dhamira ya kuwakilisha kile wanachokiwazia wananchi waliowapigia kura.

JPM ambaye anajaribu kusimamia katika kile anachokiamini hawezi kupendwa na wakuu wa mataifa wanaohudhuria zile round tables za viongozi wakubwa wa dunia. Viongozi waliofuatia baada ya JKN (ukiondoa mzee Mwinyi), waliona kuwa karibu na viongozi wakubwa wa dunia kama vile ni kitu cha kipekee sana.

JPM anao mtihani wa kujitofautisha kifikra na kimtazamo na watangulizi wake, haswa wale wawili ambao yeye amewafuatia. Ikulu inabidi ibakie na utakatifu wake, tabia ya udalali miongoni mwa mawaziri na yenyewe ife kabisa. Mafaili yote yaliyo ndani ya ofisi za TAKUKURU yafanyiwe kazi.

Naamini kuwa JPM ana kila sababu ya kumuenzi mwalimu Nyerere haswa katika suala zima la kurudisha thamani ya utu wetu na uwezo wa sisi wenyewe kufufua viwanda vya zamani na kujenga vipya ili tuweze kuwa na utambulisho wetu kisiasa na kiuchumi.

JKN alikuwa kama vile anatabiri udhaifu wa awamu ya tatu na ya nne, kashfa zote kubwa kubwa zilianza kuiumiza nchi hii kuanzia mwaka 1995 mpaka leo hii. JPM anayo kazi pevu ya kuyaishi hayo maneno ya busara ya JKN
 
kweli mkuu
 
Back
Top Bottom